Msanii Idris Sultan afika Kituo cha Polisi Central, ahojiwa aenda, kukaguliwa nyumbani kwake. Aachiwa kwa dhamana

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Msanii Idris Sultan amefika Kituo cha Kikuu cha Polisi (Central) muda wa saa 5 asubuhi kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda

Anaendelea kushikiliwa kituoni kwa mahojiano, Inadaiwa anahojiwa kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 15 na 16

F6CE8538-CD16-49B7-91A9-746C2292ED6F.jpeg


UPDATE:
Polisi wameelekea nyumbani kwa Idris kwa upekuzi

Wakili wake, Ben Ishabakaki ameithibitishia JamiiForums kuwa ni kweli Idris anashikiliwa na sasa Polisi wameelekea nyumbani kwake Mbezi jijini Dar kufanya upekuzi

UPDATE
Msanii Idris Sultan amepata dhamana ya Polisi

Ametakiwa kuripoti kituoni kesho saa 2 asubuhi
 
Back
Top Bottom