Msanii Grand P penzi lake na bi Eudoxie waachana

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,524
News updates

News toka Pande za afrika magharibi zinasema Penzi la mwanadada Matata Eudoxie Yao na Grand P limefika ukomo baada ya mwanadada huyo kuvunja uhusiano wao

Eudoxie ndie ametangaza kuwa wameshindwana, huku sababu ikidaiwa ni tabia ya Grand P kupenda kuchepuka na kinadada wengine hali ambayo imekuwa ikimnyima raha Eudoxie na sasa kuamua kuachia ngazi kwa jamaa huyo mwenye kamwili ka kitoto

Eudoxie ni pisi kali maarufu wa Ivory Coast wakati Grand P ni mwanamuziki wa Guinea, kuwa wapenzi kulifanya wajizolee mashabiki lukuki mitandaoni

Mwaka jana penzi la wakali hawa liliingia mdudu pia baada ya Grand P kudai kuwa Eudoxie amesepa na Profesa wa muziki Mcongomani Koffi Olimide, Mzee kofi Olimide Alishiriki Kurekodi muziki na mwanadada huyu matata na baada ya Kofi kuondoka kurudi kwao ndipo Grand P akadai Koff kaondoka na mpenzi wake kabla ya Baadae kumaliza tofauti zao

Picha hizi zilipigwa wakati wakiwa penzini pamoja

Wanaume ni balaa yaani pamoja na pisi kali hivi bado kamwamba kamechepuka
FB_IMG_1627207605881.jpg


FB_IMG_1627207585247.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom