Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nakumbuka kwangu enzi nipo Arusha miaka ya 2016 , Nlikuwa na kawaida ya kwenda club D maeneo ya Moshono.

Siku ya siku wakaja kina Mr Blue na Rommy Jons ambae alipewa u DJ.

Cha ajabu hatukuwa wengi sana, hatukufika hata 30,

Basi ikawa Mr Blue ananipa mic sana tu niwe nafuatiliza nyimbo zake maana nlikuwa nmezikariri nyingi.

Ilikuwa poa sana ile siku kwangu, Jamaa yupo peace hana makuu

Ndukusulukucho alokua anaimbaga na marehemu John walker, alinishauri niachane na masuala ya mziki.
 
Nilipanda Bajaji!! Na mwinjuma muumin tokea Gongo la mboto!!! Tunakwenda Mnaz Mmoja!!!

Kuna huyu Jamaa Dulayo '' huku Ukonga!!! Mitaa ya Banana Goms!! Anagongea K Vant Tuu!! Ana kitu:

Masanja Mkandamizaji!! Nimekutana Nae sana Ofisin kwetu hapa!!! Japo masihala yake yako vile vile!!!

Baghdad Aliwah kutubeba kweny Uber!!!! Ile siku Tumeita Uber mitaa ya Tazara.....Inakuja simama !! Dereva nikamtambua Baghdad!!!! Daa bas story ziliendelea......mpka chench yangu 7500/ Nilikuachia Mtoto wa Mexixana Baghdad!!!!!!

N.B
U-star zigo la mavi, !!!!!
 
Sikupiga nao stori lakini nakumbuka ilikuwa mwaka 2009 nipo Engusero Kiteto Manyara (nilienda kula likizo huko baada ya shule kufungwa enzi hizo nipo form one)

Basi katika kuzurura zurura pale barabarani si ndo nikaona gari imepaki njiani halafu ukicheki kama ya watalii vile (zile landcruiser nadhani mnazielewa). Walikuwa kama vijana 6 hivi halafu kama kuna kitu wanangoja vile basi mimi kuangalia vizuri si ndo nikamtambua Chege na yule mwenzake walioimba wote Dar mpaka Moro.

Basi nikawaambia machalii zangu niliokuwa nao yule pale ni fulani na fulani machalii wakawa hawaamini mara tukaanza kuwasogelea kiuogauoga sasa sijui wakatuelewa tunachoambiana nakumbuka wakasimama wawili wakafanya kidogo ule mchezo wao wa kukamua kwa kurusha miguu kama kwenye ule wimbo wa Dar mpaka Moro

Sasa muda huo wanajidhihirisha kuwa wao ni TMK na ndio wanapata mwafaka wa safari yao basi wakaingia kwenye gari fasta wakasepa zao basi nikajizolea umaarufu kwa wale waliokwepo mwanzo mwanzo pale kuna m'baba aliuliza "yaani sisi hatukuwajua muda wote wamekaa hapa wanahangaikia mtandao wewe umewagunduaje haraka hivyo?"

Basi eti nikajilaumu kweli kwamba kwanini sikuwasogelea kabisa bila uoga walau niwape hi tu halafu mpaka leo sikujua ilikuwaje maana baadae nilikuja kusikia walikuwa na shoo Kibaya sasa sijui ndo walikuwa wanatoka Kibaya au walikuwa wanaenda wakaghairi njiani maana mimi nilikuta gari imepaki imeelekea Kibaya na walikaa pale wanakula miwa muda mrefu sana huku wakionekana kama kufanya mawasiliano lakini kumaliza tu kuwasiliana gari ikageuzwa wakarudi kuelekea Narco
 
Tangu nipo mdogo (form one) nilikua nahang kwenye ofisi ya kuburn cd za muziki. Enzi hizo hamna kudownload nyimbo anakupa DJ na wateja lazima waje kuburn cd audio (siyo mp3) ni 2500.

Kutokana na hiyo ishu niliyokua naifanya wasanii wa kwanza kukutana nao ni kikosi cha mizinga walikua wanawatafuta wanyonyaji wa kazi zao. Wakanikamata huku tunapiga stori na bwana kalapina ngoma mpaka O'bay.

Wasanii wengine waliokuja kibandani ni Amini, jamaa ni mtu wa stori ila anajiona ana potential so ana ego kimtindo.

Fred wa makomando miyeyusho huyu jamaa anamvimbia kila mtu.

Cyril kamikaze enzi hizo hajaanza nyanyua chuma na ngoma inayotamba ni Tupo juu.

Ali Nipishe, aliletwa na mshkaji ambaye kwenye ile ngoma ya My anaonekana akiwa na pull ova ya drafti. Alikua kimya na stori kwa mbali.

Sister P alikuja kutoa kopi cd za nyimbo zake. Muongeaji yuko peace.

Crazy GK mtu poa hana makuu.

Bahat Bukuku na Msama walikua wanamkamata kila mwenye albam ya Dunia haina huruma.

Kama Maimartha Jesse mnamhesabia msanii na yeye alishakuja.

Na wasanii wa kundi wa Khanga Moko laki si pesa nishakutana nao pale kibandani. Miyeyusho kila utachoongea kinabinuliwa ili kimaanishe ishu ya ngono.

Davista, alikuja kutaka tumbanie ngoma yake aliyoimba na Mo Music ili aipeleke EATV.

Wengine wa Singeli (Hawa ndiyo wa miaka hii)

Anyway Tanga, Korogwe Manundu ni sehemu gani kuna pisi kali? Naona kila nilichoambiwa kuhusu Tanga ni uongo. Hamna kazi kali wala nini popo wa hapa wanazurura mpaka mchana.

Msaada
 
Jux, vanessa, janjaro, a.m recordz tandale, maproducer wakubwa wote, kuna mmoja anaimba nyimbo za dini alishika I phone yangu then anawaambia wenzake kwamba ni yake baadae aliing'ang'ania mpaka nikamuuzie kwa hasara, wanafake sana maisha, kuna dj mmoja wa clouds tulikutanaye bar flan akaja meza yetu shobo nyingi haa mm nabadili magari kla baada ya miezi mitatu mara cjui nn baadae ananipiga mzinga wa ten.
 
Tangu nipo mdogo (form one) nilikua nahang kwenye ofisi ya kuburn cd za muziki. Enzi hizo hamna kudownload nyimbo anakupa DJ na wateja lazima waje kuburn cd audio (siyo mp3) ni 2500.

Kutokana na hiyo ishu niliyokua naifanya wasanii wa kwanza kukutana nao ni kikosi cha mizinga walikua wanawatafuta wanyonyaji wa kazi zao. Wakanikamata huku tunapiga stori na bwana kalapina ngoma mpaka O'bay.

Wasanii wengine waliokuja kibandani ni Amini, jamaa ni mtu wa stori ila anajiona ana potential so ana ego kimtindo.

Fred wa makomando miyeyusho huyu jamaa anamvimbia kila mtu.

Cyril kamikaze enzi hizo hajaanza nyanyua chuma na ngoma inayotamba ni Tupo juu.

Ali Nipishe, aliletwa na mshkaji ambaye kwenye ile ngoma ya My anaonekana akiwa na pull ova ya drafti. Alikua kimya na stori kwa mbali.

Sister P alikuja kutoa kopi cd za nyimbo zake. Muongeaji yuko peace.

Crazy GK mtu poa hana makuu.

Bahat Bukuku na Msama walikua wanamkamata kila mwenye albam ya Dunia haina huruma.

Kama Maimartha Jesse mnamhesabia msanii na yeye alishakuja.

Na wasanii wa kundi wa Khanga Moko laki si pesa nishakutana nao pale kibandani. Miyeyusho kila utachoongea kinabinuliwa ili kimaanishe ishu ya ngono.

Davista, alikuja kutaka tumbanie ngoma yake aliyoimba na Mo Music ili aipeleke EATV.

Wengine wa Singeli (Hawa ndiyo wa miaka hii)

Anyway Tanga, Korogwe Manundu ni sehemu gani kuna pisi kali? Naona kila nilichoambiwa kuhusu Tanga ni uongo. Hamna kazi kali wala nini popo wa hapa wanazurura mpaka mchana.

Msaada
Huko Obay mkifika ilikuwaje?

Mkuu kwanini huwa hamuweki video zile HD za zamani huko Youtube
 
Similar Discussions

52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom