Nay wa Mitego: Ntaurekebisha Wimbo Wangu Kama Rais Alivyoshauri Lakini Sitavuka Mipaka

Donep

Member
Feb 22, 2017
35
53
Saa chache baada ya kuachiwa huru kutokana na amri ya Rais John Magufuli, Rapa Nay wa Mitego amesema kuwa atayafanyia kazi maoni ya Rais kuhusu kuboresha wimbo wake kwa namna ya pekee.

Rapa huyo alitiwa nguvuni wikendi iliyopita kwa tuhuma za kusambaza wimbo wake wa ‘Wapo’ ambao Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) liliweka wazi kuwa haufai na una lugha za matusi, lakini mambo yalibadilika baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kueleza kuwa amezungumza na Rais Magufuli na amesema anaupenda wimbo huo na kwamba ameagiza aachiwe huru na aufanyie maboresho kwa kuongeza mambo mengine bila kupunguza alichokiimba.

Akizungumzia suala hilo, Nay wa Mitego amesema kuwa ataufanyia marekebisho wimbo huo lakini atahakikisha havuki mipaka.

“Ninalifanyia kazi, mheshimiwa amesema anaupenda wimbo wangu na anausikiliza, yeye mwenyewe amewekwa kwenye huu wimbo ni jambo ambalo hawezi kupuuzia na hiki kinachoendelea labda amefurahishwa, hivyo nitaifanyia kazi kwa kuongeza mengi makubwa na kwa mapana zaidi bila kuvuka mipaka,” Nay wa Mitego anakaririwa.

Msanii huyo aliwataka wananchi na vyombo vya habari kuendelea kuzungumza ukweli na kutoa maoni yao lakini wazivuke mipaka.

‘Wapo’ haukuwa wimbo wa kwanza kumuweka matatani Nay wa Mitego kwani baadhi ya nyimbo zake kama ‘Pale Kati Patamu’ na ‘Shika Adabu Yako’ ziliwahi kufungiwa na Basata na kupewa onyo kali.
 
Miongoni mwa vitu vilivyonikera kwa ney ni hili aisee nimemuona ni bonge moja la falaa halafu ni muoga muoga kama yale mandege yanayoitwa ndege john

Yani kalainishwa kidogo tu huyo kalainika kama mlenda
 
Habari za muda huu wakuu,

Inafahamika kwa wengi msanii ni kioo cha jamii uwepo wake ni kwa ajili ya kuelimisha, kuasa na kuelekeza kuhusu maadili mema kwa jamii.

Msanii Emannuel Elibariki (Nay wa Mitego) anatia aibu, sio mtu wa kumfumbia kwa anayoyafanya. Amekuwa mchango mkubwa katika kuharibu fikra za vijana wetu ni mtu ambae anashambulia wasiokuwa na hatia bila kuwa na ushahidi.

Ningependa kumshauri huyu kijana katika kufanya kazi zake asitumie lugha ya kukerehesha ikiwemo matusi, anaowazungumzia katika sanaa yake awe na ushaidi na mwisho kama ana dhamira ya kweli.

ambo ya kuwasilisha katika jamii ni mengi ningependa asaidie serikali yetu tukufu kupambana na dawa za kulevya, rushwa na mengineyo ila akiwa na ushaidi.
 
Inaelekea vijana wa rika lake wanapenda kutiwa aibu ndio maana wanampenda. Asingekuwa anapendwa angepotea siku nyingi. Hiyo ndio miziki yao kiongozi. Ngoja vijana wenzake waje watueleze.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Saa chache baada ya kuachiwa huru kutokana na amri ya Rais John Magufuli, Rapa Nay wa Mitego amesema kuwa atayafanyia kazi maoni ya Rais kuhusu kuboresha wimbo wake kwa namna ya pekee.

Rapa huyo alitiwa nguvuni wikendi iliyopita kwa tuhuma za kusambaza wimbo wake wa ‘Wapo’ ambao Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) liliweka wazi kuwa haufai na una lugha za matusi, lakini mambo yalibadilika baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kueleza kuwa amezungumza na Rais Magufuli na amesema anaupenda wimbo huo na kwamba ameagiza aachiwe huru na aufanyie maboresho kwa kuongeza mambo mengine bila kupunguza alichokiimba.

Akizungumzia suala hilo, Nay wa Mitego amesema kuwa ataufanyia marekebisho wimbo huo lakini atahakikisha havuki mipaka.

“Ninalifanyia kazi, mheshimiwa amesema anaupenda wimbo wangu na anausikiliza, yeye mwenyewe amewekwa kwenye huu wimbo ni jambo ambalo hawezi kupuuzia na hiki kinachoendelea labda amefurahishwa, hivyo nitaifanyia kazi kwa kuongeza mengi makubwa na kwa mapana zaidi bila kuvuka mipaka,” Nay wa Mitego anakaririwa.

Msanii huyo aliwataka wananchi na vyombo vya habari kuendelea kuzungumza ukweli na kutoa maoni yao lakini wazivuke mipaka.

‘Wapo’ haukuwa wimbo wa kwanza kumuweka matatani Nay wa Mitego kwani baadhi ya nyimbo zake kama ‘Pale Kati Patamu’ na ‘Shika Adabu Yako’ ziliwahi kufungiwa na Basata na kupewa onyo kali.
Nonsense, bila kuvuka mipaka ni nini? Define what is bila kuvuka mipaka
 
Miongoni mwa vitu vilivyonikera kwa ney ni hili aisee nimemuona ni bonge moja la falaa halafu ni muoga muoga kama yale mandege yanayoitwa ndege john

Yani kalainishwa kidogo tu huyo kalainika kama mlenda
Naongeza, ..........." Mawaziri watakaofanya sherehe baada ya kuacha uwaziri".... WAPOOOOOOOO
Waliokula hela Za wahanga wa tetemeko wapo.
Wanaowapiga wake zao pia wapo
Wanaoingilia muhimili wa bunge Na mahakama wapo
Waliodanganya kuboresha maisha ya watanzania wakati wa kampeni wapo
Wanaodharau watoto wa maskini kwa Kuwaiti Vilaza pia wapo.
 
Wewe sasa umepitiliza mipaka, Ney keshasema hatapitiliza mipaka. Mimi nimenukuu kauli tu wakati anawateua.
 
Waliokula hela Za wahanga wa tetemeko wapo.
Wanaowapiga wake zao pia wapo
Wanaoingilia muhimili wa bunge Na mahakama wapo
Waliodanganya kuboresha maisha ya watanzania wakati wa kampeni wapo
Wanaodharau watoto wa maskini kwa Kuwaiti Vilaza pia wapo.
Kitendo cha ney kusema ataongea bila kuvuka mipaka amenikera sana

Hii kwa sababu hatoweza kuzungumzia mambo yale nyeti na pia hatoweza kumchana hicho ki magu
 
Waliokula hela Za wahanga wa tetemeko wapo.
Wanaowapiga wake zao pia wapo
Wanaoingilia muhimili wa bunge Na mahakama wapo
Waliodanganya kuboresha maisha ya watanzania wakati wa kampeni wapo
Wanaodharau watoto wa maskini kwa Kuwaiti Vilaza pia wapo.
Waliodanganya kuna meli 30 Za MIZIGO bandari Huku wakijumlisha mpaka boti Za bakharesa WAPO
 
Miongoni mwa vitu vilivyonikera kwa ney ni hili aisee nimemuona ni bonge moja la falaa halafu ni muoga muoga kama yale mandege yanayoitwa ndege john

Yani kalainishwa kidogo tu huyo kalainika kama mlenda
anza wewe kutunga wa kwako! alipokamatwa mlikuwa wa kwanza kusema amezidi wacha akaisome namba sasa hivi kaachiwa mnajisikia vibaya hivi unadhani ney ni nani mpaka ashindane na dola?
 
Back
Top Bottom