Msanii Cheed ajitoa kwenye lebel ya Ali Kiba Kings Music

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,439
12,294
Ameandika alfajiri ya leo kwamba ameamua kufanya hivyo bila ubaya wowote na kwa hiari yake.

Kuishi na kulea vijana kama hawa yataka moyo sana.

=============

IMG_20200414_052046_060.jpg
Naitwa Rasheed almaarufu kama cheed nikijulikana kama msanii wa @kingsmusicrecords. Napenda kuwajulisha fans wangu watu wangu wote waliokuwa wakisupport mziki wangu na wanaoendelea kussuport kazi zangu na hata wasiosupport pia ni kwamba kuanzia leo hii napenda kutamka kuwa mimi sio tena msanii wa @kingsmusicrecords nimeamua hili kwa akili yangu timamu kabisa bila kushawishiwa na mtu wa aina yeyote ile na sijatumia kilevi chochote kile ni maamuzi yangu tu binafsi na ni kwa ajili ya muendelezo wa mziki wangu.

Ali Kiba amekuwa ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu amekuwa ni mtu ambae amenionyesha njia na kuniaminisha mimi pamoja na mziki wangu mbele ya jamii Inshallah mwenyezi mungu amlipe kwa kila alichonifanyia na kujitolea kwa ajili ya mziki wangu namshkuru sana sana sana nasitoacha kumshkuru siku zote za maisha yangu naumia 😭😭😭ila sina budi @officialalikiba nakupenda sana my brother nakupenda mnooo na unajua hilo,

Cha zaidi napenda nikushkuru kwa kunielewa nikiwa kama mdogo wako bado nahitaji baraka zako bado ntahitaji support kutoka kwako kwa namna moja ama nyingine ama kwa kile ambacho kitakuwa na umuhimu kuwa supported na ningeomba pia uniombee dua safari yangu iwe njema na yenye mafanikio popote pale ntakapokuwa as long as najua hatujaachana kwa ubaya na wala hatujawahi kuwa na ugomvi labda NO.

Pia ningependa kuwashkuru waliokuwa wakisimamia kazi zangu ili ziweze kuwafkia kwa haraka mashabiki zangu na kuweza kufika kwa haraka kwenye media tofauti tofauti nazungumzia managers wangu @beingaidancharlie @suleshsulle @rehemavisuallab @esilovey1 nawapenda sana nashkuru sana kwa time yenu kwa yote mazuri mlioweza kunifanyia sitoweza kusahau nyakati zote tulizopitia bado nyinyi mtabaki kuwa watu muhimu kwenye career yangu.

Love you all ❤❤❤

Asanteni sana 🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Tukiacha unafiki vijana wa king music wanajua sema hawajapata mtu wakuwasimamia, yaani unawachukua watu uwafuge ndani kwako ka mabinti wa kazi?

Huyu jamaa anawashika mkono kinafiki ila hataki wafike popote, japo viswaswadu wake bado watakaza mishipa ya shingo kumtetea.
 
Huo ndio ukomavu, kijana ana guts. Ameona mbali, ameamua ajitegemee mwenyewe sasa, kaanzishe kampuni na wewe ili utoe ajira kwa vijana wengine.

Wadogo zetu hawa wanatufundisha hata sie wakubwa zao sio kung'an'gania kwenye ajira, miaka inaenda tu, kuacha tunaogopa, hatutengenezi fursa kwa wengine.

Kama hatuwezi kuanzisha shughuri zitakazo leta ajira,kwa wengine,tunataka nani afanye?
Dogo ametupa shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_9212.JPG

Pia mbona huyu anayeitwa sijui Killy naye kaandika kitu kinachofanana. Kwa hiyo hawa wote wawili wamejitoa kings record.

Hawa itakuwa kiki aisee, maana hawajulikani kabisa! Watakuja soon na kusema account zao zimekuwa hacked!

Haiwezekani muandiko ufanane hivyo aisee.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
tukiacha unafiki vijana wa king music wanajua sema hawajapata mtu wakuwasimamia, yaani unawachukua watu uwafuge ndani kwako ka mabinti wa kazi??

huyu jamaa anawashika mkono kinafiki ila hataki wafike popote, japo viswaswadu wake bado watakaza mishipa ya shingo kumtetea
Wanajua baada ya kuskia wamejitoa? Nahisi unajinsia mbili bro siyo kwa unafki huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom