Msanii Chameleon ajirusha ghorofani, avunjika miguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msanii Chameleon ajirusha ghorofani, avunjika miguu

Discussion in 'Entertainment' started by Mtaalam, Oct 6, 2008.

 1. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,276
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  MSANII maarufu wa Uganda, Jose Chameleon amejirusha kutoka ghorofa ya tatu ya Hoteli ya Impala mjini Arusha na kusababisha kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika miguu yote.

  Chameleon ambaye amekuwa akitamba na nyimbo za ‘Jamila’, ‘Mama Mia’ na nyingine alijirusha kutoka chumbani kwake katika ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo alfajiri ya saa 11 kuamkia juzi.

  Imeelezwa msanii huyo alishituka akiwa chini amevunjika miguu hiyo na walinzi walikimbilia eneo aliloangukia baada ya kusikia kishindo na kumkuta akiwa hawezi kuinuka.

  Hata hivyo haikueleweka kilichomfanya msanii huyo ajirushe, baadaye wenyeji wake ambao ni Clouds FM waliokuwa wamemualika kwa ajili ya shughuli ya Fiesta ya Tanga juzi walibidi kufanya utaratibu wa kumpeleka hospitali.

  Lakini baadaye walitakiwa kutomtibu na baba yake aliagiza ndege ambayo ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA na kumbeba na kumpeleka Uganda ambako amelazwa katika hospitali moja ya nchini humo akipata matibabu.

  Kuumia kwa msanii huyo kulisababisha ashindwe kufanya shoo katika tamasha la Fiesta ambako kulikuwa na wasanii wengi wa Tanzania na yeye ndiye alikuwa mgeni aliyetakiwa kuongoza shoo hiyo.

  Henry Mdimu, Tanga
   
 2. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,276
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  naombeni pia wenye more info za huo ugonjwa wa sleep walkin watupage hapa maana ishaanzwa kusemwa semwa kuwa yawezekana ni uongo huo umetungwa faster faster ku cover mabo flani flani!

  wenye habari zaidi watupage na wajuao anaendeleaje watutonye juu ya huyu msanii wetu wa africa mashariki
   
 3. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,276
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  further more wasanii wetu wapate somo from tukio hilo,wenzetu sanaa ni kazi kweli kweli n they get mijihela humo ndani yake in such a way hata kukodi private jet kuja kumleta mkewe na kumbeba yeye it is possible sasa sie pale kwetu bongo kuna wasaniii wenye kuweza afford nyodo hiyo?au twaishia kuvaa tu na kujiita ma selebriti??wakati hata kukodi tax mbinde?mtu mzimaaaa lakini bado anakaa kwa parents!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,127
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  Karushwa huyo !!!!!kaparamia mizoga ya ar.....

  Wakashindwana bei!!!!watu wakamng******************
   
 5. P

  Paullih Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hebi tufafanulie Mama Mia! Yaelekea habari unayo weye. Nampa pole Jose Chameleon! namtakia apone haraka.
   
 6. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mama Mia,
  Kweli yawezekana kwa nini hawataki kutuambia yaliyomsibu? na sisi tunajua mizogo nje nje pale AR. Huenda ni kwa sababu zinazofanana na hizo labda mwenye details atuambie
   
 7. M

  Mage Member

  #7
  Oct 6, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fiesta ilikuwa Tanga yeye Arusha kulikoniiii?Jamani hapa kuna uwalakini...........
   
 8. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Lazima jamaa alikuwa bwii akaona ajaribishe kama anaweza ruka kama kipepeo.....
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh si mchezo jamaa wanadai alikuwa anaota sijui alikuwa anaota anaigiza picha??
  Au alikuwa na mzigo ndani wakashindana dau basi ndo hivyo tena ... ngoja tutapata tu dot kwa wahudumu wa hiyo hotel.
   
 10. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35


  hapana kaka ni bangi tu hiyo
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Bange tu hiyo...au isije ikawa kama mtu kupata ajari ya gari harafu...unakatika mkono tu.
  Hakuna hata jeraha kichwani,mguu,mgongoni etc na gari tunaambiwa imeharibika vibaya sana...

  Kuna ka walakini hapa..if not bange tu hizo.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh kweli dada Naima mambo ya bangi nibangue...........zimemvunja miguu sasa.
   
 13. I

  Incognito Member

  #13
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kulikoni Arusha?tupeni yaliyojiri
   
 14. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  watu mnatuboa ummu mbona mnaongea kwa mafumbo simweke mambo wazi aaaah! maana najua mnafahamu tu ukweli wa mambo :)
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Alikuwa na mwanamke anayeitwa lily mwenyeji wa arusha walitoka nae nairobi mpaka wakati huo wa tukio sasa haileweki kama lily anahusika na tukio hilo au la lily ni mwanamke wa wakili maarufu hapo mjini arusha anayekaa karibu na chuo cha uhasibu
   
 16. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The truth about the scene in different sources:

  Source 1(Spoti starehe)
  Superstar,Jose Chameleone was on Saturday admitted in Nsambya Hospital, Kampala, after sustaining crash fractures on both his calcenus bones of both his lower legs according to hospital reports. The singer is said to have fallen unconsciously from the third floor of a hotel in Arusha, Tanzania.

  The singer who had travelled to Arusha in Tanzania for his routine regional performances, sleepwalked through the window from his room on the 3rd floor at Impala Hotel and hit his torso down on the ground.

  he woke up sorrounded by people who called the air ambulance and was airlifted to Kilimanjaro airport where he was immediately flown to Entebbe airport and transferred to Nsamya Hospital where is under intensive medical attention.

  Check it here Jose Chameleone still in Hospital « Spoti na Starehe

  Source 2(Ego Image Kenya)
  Jose Chameleone a.k.a Joseph Mayanja last Friday night, survived death narrowly when he sleepwalked through the window of his hotel room on the third floor of Impala Hotel in Arusha.

  Chameleone who had traveled to Tanzania for weekend music shows in Arusha and Tanga; broke both lower bones of his legs.

  ‘He got injuries on the lower legs; it is a crash fracture of calcenus bones of both legs,” explained Kenneth Obwot, a doctor who airlifted him from Kilimajaro Airport.

  Obwot said that Chameleone walked up from his dreams and went through the windows. The singer was alone in the room and the door remained closed. He landed from the third floor of Impala Hotel in Arusha, Tanzania, but was lucky; he had no other injuries apart from the bone fractures.

  Chameleone says he went safely to his hotel room after his music show; changed clothes to boxers and slept. But he was shocked to find himself surrounded by people hours later; others were calling him a thief! He was in pain; but one of the onlookers identified him and rushed to call promoters who had taken him to Tanzaina.

  As soon as the promoters arrived; they rushed him to Arusha Hospital; where he immediately contacted his wife to charter a plane which airlifted him from Kilimajaro Airport to Entebbe International Airport. He was admitted to Nsambya Hospital at 10:00pm on Saturday 4th October 2008.

  cHECK IT HERE Egoimagekenya » Hot Gossip » Chameleone survives death

  Source 3: African Press

  Ugandan singer injured in Tanzania
  Uganda\’s celebrated musician Joseph Mayanja aka Jose Chameleone, famed for his Kiswahili songs understood throughout East Africa and the Democratic Republic of Congo, is admitted in a Kampala hospital following a limb injury at the northern Tanzania town of Arusha on Saturday.

  According to his promoters and local media, Chameleone was flown to Kampala with injured limbs after falling off the third floor of Impala Hotel in Arusha.

  The singer had reportedly traveled with his younger brother Emma Mayanja, also a singer, to Tanzania to perform at a music show.

  Chameleone told his local fans and the media from his hospital bed on Sunday that he could hardly remember the events that led to his falling from the hotel room.

  \”I remember going to my bed that night and slept. But the next time I opened my eyes, I was on the floor surrounded by several people. I cried because I was feeling a lot of pain and I could neither stand up nor turn my body,\” he said.

  Sources said that the hoarse-voiced singer is believed to have sleepwalked through the window of his hotel room.

  The hotel management rushed him to AICA Hospital in Arusha where he was first admitted before he called his wife, Daniella Atim, who later organized for the singer to be flown to Kampala in a private chartered plane.

  According to hospital sources, Chameleone broke both his ankle joints and would undergo another scan.
  —————
  API/Source.apa

  Check it here Chameleone the Uganda-singer-hospitalized « African Press International (API)

  Uki-tally the 3 posts above uta-sense the truth..
   
 17. m

  mgiriki Member

  #17
  Oct 7, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari nilizonazo ni kwamba Leo sasubuhi majira ya saa 1:00 ajali mbaya na yakusikitisa imetokea maeneo ya UNGA LTD Arusha Haisi iligonga watoto wawili na kufa hapohapo. Pamoja na watoto hao kufa dereva aliekuwa anaendesha haisi hio nae yuko mahutiuti baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.

  HABARI ZAIDI NITAWALETEA.
   
 18. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa jamani Mgiriki na wewe kwanini umeweka habari ya kusikitisha namna hii kwenye "entertainment forum"? Pia licha ya kusikitisha haihusiki na celebrities.
  Mods........
   
 19. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo Chameleon ana harufu zote za fumanizi.
   
 20. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aisee halafu ukicheki hiyo picha kwenye link mbona jamaa amepauka namna hiyo? Duh, jamani miguu iko "ashy" ile mbaya, aibu
   
Loading...