Msanii Alikiba ameshinda tuzo kubwa nyingine ya Beffta awards Uk

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,040
Msanii wa Kimataifa kutokea nchini Tanzania, ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya MTVEMA2016 @officialalikiba, Ameshinda tena tuzo kubwa ya nchini Uingereza maarafu kama [HASHTAG]#befftaawards[/HASHTAG] za Uk kama Best International African Act (Msanii bora wa kimataifa kutokea Africa.

Katika Category hiyo @officialAlikiba alikuwa akishindana pamoja na miamba mingine ya mziki Africa kama Wizkid, Casper Nyovest, Diamond platinumz, Patroranking, Korede bello, Yemi Alade na Stanley enow wa Ghana.

Kwa Mujibu wa meneja mkuu wa Alikiba, Madam @sevenMosha amesema kwamba "Tangia tarehe 28 October Alikiba alikuwa ametangazwa mshindi wa Tuzo hizo kubwa katika kipengere cha "Best International African Act" sema kutokana na ratiba kuingiliana hawakuweza kwenda kuhudhuria tukio hilo la ugawaji wa tuzo, Ila sasa wameshafanya mawasiliano na waandaaji wa tuzo hizo na pindi tuzo hizo zitakapowasili, watatangaza rasmi kupitia media mbalimbali pamoja na social media.

Written by @
 
Yani kiba tuzo zote hadi akate rufaa, kwahiyo tokea 28 October walishindwa nn kutangaza ameshinda tuzo ila bado haijafika nchini? nafurahi kuona yuko list moja na miamba ya afrika kama mond bin laden na wengine!
 
Kinachomuangusha ally kiba ni poor management , tangu tarehe 28 hakuna mtanzania anaejua lolote kuhusu kiba na hii tuzo... Si kwenye social platforms za yeye kiba au meneja wake....

Nina uhakika kama mtu anachukua tuzo mbele ya wiz kid kwa hii menejiment ambayo huwa siielewi , siku akipata management inayojielewa atafika mbali sana
 
Tangu tarehe 28 ilipotolewa hawakupost kwasababu ilikua haijafika, nini kimewafanya wapost leo huku bado haijafika?

anyway hongera zake
 
Hongera sana Alikiba, mwaka huu umestahili kupata tunzo. Ongeza juhudi zaidi mwakani upate zaidi ya hizi hasa kwenye collabo na wasanii wa mataifa mbalimbali.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom