Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI) Salum Msangi
INASHANGAZA PALE MSANGI ANAPOKIRI KUWAKAMATA WAHALIFU NA ANAPOSHINDWA KUKIRI KUA HALI YA AMANI YA ZANZIBAR NI TETE.
Leo Msangi alihojiwa na kukiri kua jeshi la Polisi limewashkilia wafuasi na viongozi wengi wa chama cha wananchi CUF kwa visingizio kua ni wahalifu na wamefanya vitendo vya hujma ikiwa ni pamoja na kukata mikarafuu na kuharibu mali za wananchi.
Katika mahojiano hayo Msangi alisema kua wakati huu ni wakati mgumu kwa wahalifu na sio wakati mgumu kwa Wazanzibari na kuendelea kusema kua wataendelea kuwakamata wale wote wanaofanya na walioamrisha watu hao kufanya vitendo hivyo.
Pamoja na hayo Msangi alionekana kama hajui maana ya uhalifu na hajui vitendo vya uhalifu na athari zake katika taifa ndipo muandishi wa habari alipoamua kumuuliza kua “kwa hiyo hali ya amani visiwani Zanzibar kwa sasa ni mbaya?”
Ajabu ni kwamba Msangi kajibu swali hili huku akisahau kauli yake ya nyuma aliyosema kua wamewakamata wahalifu wengi sana na kujibu kwa kusema kua hali ya amani ni mzuri na imetulia.
Hiyo ni sawa na kusema kua Msangi kadanganya kusema kakamata wahalifu au kadanganya kusema kua hali ya amani ni mzuri na imetulia kwani kawaida na historia nyingi duniani zinaonyesha kua taifa likigubikwa na uhalifu kama anaodai Msangi katika taifa hilo huwezi kusema kua amani ipo vizuri.
Hii ndio athari ya viongozi wa Jeshi la Polisi kutumika kisiasa, Msangi analazimika kusema pumba na uongo kwasababu ya kutaka kuwaridhisha wanasiasa.
Kwani Msangi hafahamu kua kama ni uhalifu basi Jecha, Balozi Seif, Haji Omar Kheir, Moh’d Aboud na Shein ndio wahalifu wakuu?
Ivi Msangi anadhani nani hajui kwa nini anawahukumu wanaokabiliana na tatizo na kuwaacha waliosababisha tatizo?
Msangi hatutokosea tukisema kua ni mwanachama kindakindaki wa CCM kwani ameonyesha kwa vitendo ukada wake lakini lazima afahamu kua kama kudai haki ni uhalifu basi wahalifu sio tu wale anaowakamata au aliokwishapanga kuwakamata bali wahalifu ni Wazanzibari wote kwani wanaodai haki sio CUF tu bali ni Wazanzbari wote.
Tunamwambia Msangi kua tumechukizwa sana na kauli yake ya kuwaita Wazanzibari wahalifu lakini akumbuke kua kauli hiyo na vitendo vyao vya kukamata watu kwa visingizio uchwere havitoturejesha nyuma hata kidogo katika kudai haki zetu.
Pia asisahau kua Zanzibar kaikuta hivi hivi na ataicha hivi hivi na ajue kua Zanzibar ina wenyewe na watu wa kutumwa kutoka Tanganyika kama yeye wameshakuja na kuondoka wengi tu na hatimae wameshindwa na kuicha Zanzibar kama ilivyo.
Punzi zisimdanganye wala asidhani kua yeye ndio atafanikiwa kukikamilisha kile alichotumwa na Watanganyika wenzake.
# Zanzibar itabaki kua ya Wazanzibari wenyewe#