Msamiati mpya wa SUKUMA GANG haufai, unaweza kuleta matatizo kwenye jamii hapo baadaye. Mamlaka ziliangalie hili

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,137
2,000
Mkuu ningeweza kulike hii comment mara mia.CHADEMA wanafurahia sana umaarufu wanaopewa na Kigogo huko twitter wanachosahau 2025 huyo Kigogo hatokuja Usukumanj kuwaombea kura,pengine wameridhika na Siasa za twitter na ndizo zitawapatia ushindi kwenye uchaguzi Mkuu ujao.

Hapo paragraph ya mwisho ndiyo ukweli wenyewe. Viti Maalum 25 unakuta Wachagga 17.Wewe waache waendelee kuwasimanga Wasukuma,2025 si mbali watakuja,unless wameamua kura za Wasukuma hawazitaki tena.
Mwaka 2015 CHADEMA walipata viti 4 kati ya 6 vya Ubunge mkoani MARA lakini MARA hawakupewa mbunge hata mmoja wa viti maalum.

Na mwaka huo wa 2015 nilikuwa Kilosa, wanawake walijituma sana kupambania CHADEMA tena kwa mkoa wa Morogoro ambao haukuwahi kutoa mbunge wa upinzani lakini CHADEMA wakapata viti 3. Lakini cha kushangaza viti maalum anaewakilisha Morogoro akateuliwa mchagga Joyce Minja wakati huo alikuwa Ripota wa ITV kutokea Morogoro. Wale wanawake wa CHADEMA Morogoro wakatupwa.

Hawa watu kuwa nao makini. Cheka nao lakini ukiwa na akili zako kichwani.
 
Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
2,406
2,000
Mwaka 2015 CHADEMA walipata viti 4 kati ya 6 vya Ubunge mkoani MARA lakini MARA hawakupewa mbunge hata mmoja wa viti maalum.

Na mwaka huo wa 2015 nilikuwa Kilosa, wanawake walijituma sana kupambania CHADEMA tena kwa mkoa wa Morogoro ambao haukuwahi kutoa mbunge wa upinzani lakini CHADEMA wakapata viti 3. Lakini cha kushangaza vitu maalum anaewakilisha Morogoro akateuliwa mchagga Joyce Minja wakati huo alikuwa Ripota wa ITV kutokea Morogoro. Wale wanawake wa CHADEMA Morogoro wakatupwa.

Hawa watu kuwa nao makini. Cheka nao lakini ukiwa na akili zako kichwani.

Unakuta ni Viti maalumu Mkoa wa Mara ,Jina Ruth Owenya,unadhani pengine huyu Mzawa wa Mara,kumbe ni binti yake Ndesamburo.Na style hii wameitumia sana kote. Waache waruke ruke,hili la Sukuma Gang litawaadhibu vizuri sana kama CUF walivyoteswa na kunasibishwa na Uislam hadi chama kimejifia chenyewe. Kwa sasa vita iliyopo ni CDM vs WASUKUMA na sisi tunasema tuko tayari,2025 tutaelewana nao vizuri sana.
 
Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
2,406
2,000
Hiyo ndio nguvu ya Microeconomies, ndio maana tuna Maendeleo kuliko jamii yoyote Africa ya Mashariki. Kikubwa tuko kote.
Wakati Wasukuma wako kwenye mapori yote wakituandalia mifugo

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app

ha ha ha ha hebu acha kuchekesha watu hapa wewe. Endeleeni na harakati zenu twitter,tunawasubiri 2025,mje pale viwanja vya furahisha na sisi Sukuma Gang tuwape
 
Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
2,406
2,000
Kama halikukemewa kipindi kile why now let it be there Sukuma gang walibagua watu wengine. Hata Gwajiboy alishikwa na kuhujiwa juju bila serikali kutoa karipio kubwa lililostahili. Kwa nini sasa unaona ni tatizo kuliko waliolianzisha? Waache watu watoe dukuduku lao ili iwe fundisho kwa kabila lolote kutotumia karata hiyo tena. iwe mwiko. Naona mkuki kwa nguruwe kwa mwanadamu mchungu.

Halafu utakuja kwa Wasukuma kuwaomba kura? Au mnajitoa ufahamu? Utuambie liwe fundisho kisha uje kwetu utake ridhaa ya kura zetu uende Ikulu? CDM mmefail vibaya sana katika hili na CCM wataawaadhibu kupitia hii hii kampeni yenu ya kuwachukia Wasukuma.Waulizeni CUF walivyong’ang’aniwa na dhana ya Uislam mpaka chama kimejifia chenyewe.Uzuri hao hao viongozi wenu wanajua Ngome ya Ushindi wa chaguzi zote iko Kanda ya Ziwa. Karibuni sana twawasubiri.Proud Sukuma Gang
 
koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
574
500

Dhana sii kuchukia wasukuma ila kilichofanyika hakikuwa sahihi kuruhusu makundi haya kujitokeza kwa kisingizio cha kulinda utawala walifikiri ulikuwa wa wasukuma. Hii dhana haikuwa sahihi Serikali ilibidi ikemee kwa nguvu zote. Rais ni wa watu wote kama aliekuwa madarakani hakujua ni upotofu. Pili CDM ni chama kama CCM ambavyo vyote sii mwanachama, mimi naangalia mstakabali wa Taifa zaidi. Chama kitakacho tumia card ya ukabila nacho ni mfu kabisa. Hii itapelekea kuligawa Taifa zaidi na Tanzania kusambaratika kabisa.
 
luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Yani tumkatae Magufuli kisa tumfurahishe Kigogo na Chadema? Kwanza nani ana shida ya kura kati ya Wasukuma vs CHADEMA,nilidhani ungewashauri CDM wacheze siasa safi na waondoe hii dhana ya kuhusishwa na chuki za Kigogo vs Wasukuma,au wao kura za Wasukuma hawazitaki? JPM alikuwa ni Pure Msukuma and yes we are proud kutoa Rais Msukuma hapa Tanzania.
Akawasaidia nn? Mbona mikoa yenu ni maskin sana kitakwimu?
 
luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Mgekuwa hamna ndoto za kutawala Nchi hii msingehangaika na CDM tangu enzi za Mzee Mtei, ni kwamba The Giants wa Nchi hii wameamka,pale Ikulu kama mlishindwa kuingia enzi hizo,kwa sasa ndiyo kabisa haitokaa itokee,labda Nchi hii iumbwe upya.

Unachekesha sana wewe,endeleeni kujazana pale Makoroboi na vibanda vyenu vya Umachinga,na kuuza used spares za magari,mmeikamata Mwanza wapi wakati Watoto wa Kanda ya Ziwa wako pale wanafanya yao na yanaonekana. Kuanzia biashara zote kubwa,viwanja vya Starehe,biashara za Madini, Hospitals,Uvuvi mkubwa kote hampo. Endeleeni na harakati zenu tu lkn pale Ikulu hamtokuja kanyaga kamwe.Hili likukae kichwani mwako. Proud Sukuma Gang
Mbona hujataja na maghorofa yao?
 
luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Halafu utakuja kwa Wasukuma kuwaomba kura? Au mnajitoa ufahamu? Utuambie liwe fundisho kisha uje kwetu utake ridhaa ya kura zetu uende Ikulu? CDM mmefail vibaya sana katika hili na CCM wataawaadhibu kupitia hii hii kampeni yenu ya kuwachukia Wasukuma.Waulizeni CUF walivyong’ang’aniwa na dhana ya Uislam mpaka chama kimejifia chenyewe.Uzuri hao hao viongozi wenu wanajua Ngome ya Ushindi wa chaguzi zote iko Kanda ya Ziwa. Karibuni sana twawasubiri.Proud Sukuma Gang
Acha povu ngosha,wakati mwendazake akiwepo si mlikuwa mnajitapa kuwa nyie ni empire kubwa? Sasa mnalalamika na cdm kwa lipi? Tz nzima ilikuwa inawaona mnavyojazana ushamba na mwendazake
 
luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Unakuta ni Viti maalumu Mkoa wa Mara ,Jina Ruth Owenya,unadhani pengine huyu Mzawa wa Mara,kumbe ni binti yake Ndesamburo.Na style hii wameitumia sana kote. Waache waruke ruke,hili la Sukuma Gang litawaadhibu vizuri sana kama CUF walivyoteswa na kunasibishwa na Uislam hadi chama kimejifia chenyewe. Kwa sasa vita iliyopo ni CDM vs WASUKUMA na sisi tunasema tuko tayari,2025 tutaelewana nao vizuri sana.
Acha uzwaWa mkoa wa Mara wabunge wa viti maalumu walikuwa kina Catherine ruge,acha chuki na wachaga huwez kuwafikia kwa lolote,cha msingi endelea kupiga jembe
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,636
2,000
Wasukuma ndio kabila kubwa Tanzania ndio jamii ya watu wengi zaidi.

Ni wapole kwa asili vinginevyo hizi dharau zilizoibuka kuanzia 2015 kama wangekuwa ni watu wakorofi leo hii Tanzania ingewaka moto.

JPM ameshazikwa na hawezi kujitetea, kwa maadili ya kawaida tu sio ustaarabu kumkejeli aliyekwisha ondoka milele.

Natumaini wale members humu ndani wenye akili za kikubwa hawatachoka kuwafunza maadili wale wote wasioifahamu hatari ya kuhubiri ukabila na ubaguzi wa kikanda.

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila ktk siasa zetu.

..kiongozi wa nchi anazungumza kwa kutumia lugha ya kabila lake mlitegemea wale wasio wa kabila lake watamuelewa vipi?

..na alipokuwa akipiga kampeni kwa Kisukuma wewe ulikuwa mmoja wa wachangiaji wa hapa JF mliomtetea bila kuchoka.

..Ni matumaini yangu kwamba Watz tutajifunza kutokana na makosa ya Magufuli, na tutaazimia kuyarekebisha.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,284

Kuongea kisukuma mbele ya wasukuma haikuwa dhambi pengine kati ya hao aliyoongea nao kisukuma wapo hawajui kiswahili.

Hakuna mbunge mchagga aliyekatazwa kuongea kichagga mbele ya hadhira ya wachagga.

Hayupo mwanasiasa ambaye akiwa na wa kwao hachomekei maneno machache ya lugha ya kwao.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,636
2,000
Kuongea kisukuma mbele ya wasukuma haikuwa dhambi pengine kati ya hao aliyoongea nao kisukuma wapo hawajui kiswahili.

Hakuna mbunge mchagga aliyekatazwa kuongea kichagga mbele ya hadhira ya wachagga.

Hayupo mwanasiasa ambaye akiwa na wa kwao hachomekei maneno machache ya lugha ya kwao.
..mchagga angekampeni kilugha ingekuwa tatizo kubwa kwake na chama chake.

..vilevile tume ya uchaguzi imekataza wagombea kuzungumza kikabila.

..maelekezo ya sheria / tume ni kwamba wagombea wazungumze Kiswahili na kama kuna wasioelewa watafsiriwe hotuba na mkalimani.

..Ni bahati mbaya sana kwamba Magufuli alivunja sheria ya uchaguzi waziwazi na hakukuwa na mtu au mamlaka yoyote ya kumkemea.

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila hapa nchini. Na vita yake dhidi ya Chadema na kampeni kwamba ni chama cha wachagga matokeo yake tunayaona sasa hivi.
 
koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
574
500
Hii karata ya ukabila ukiachia mbali Rais aliepita hutumiwa hata na ccm yenyewe. CUF waliisingizia ya wazanzibar na ni waislam wanaotaka kuvuruga amani ya nchi. Cuf ikayumba. Sasa hivi CDM wanasema ni chama cha wachagga ila this time hawakufaulu kukiuwa chama hicho kipo kinachechemea. Ccm imekuwa ikichezea amani ya nchi kama kitenesi. Generation ijayo watakuwa na mtazamo mwingine na hawatachotwa na hizi propaganda hatarishi na mapinduzi ya kiutawala na kisera yatakuja ba hakuna atakae zuia.
 
..kabla ya kuitwa chama cha wachagga cdm iliitwa chama cha wakatoliki, enzi zile km ni dr.slaa.

..halafu kulikuwa na chama cha udp kilichoanzishwa na john cheyo. Chama hicho kilisingiziwa kuwa ni cha wasukuma kwasababu cheyo ni mwenyeji wa bariadi shinyanga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom