Msamiati mpya wa SUKUMA GANG haufai, unaweza kuleta matatizo kwenye jamii hapo baadaye. Mamlaka ziliangalie hili

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Mkuu ningeweza kulike hii comment mara mia.CHADEMA wanafurahia sana umaarufu wanaopewa na Kigogo huko twitter wanachosahau 2025 huyo Kigogo hatokuja Usukumanj kuwaombea kura,pengine wameridhika na Siasa za twitter na ndizo zitawapatia ushindi kwenye uchaguzi Mkuu ujao.

Hapo paragraph ya mwisho ndiyo ukweli wenyewe. Viti Maalum 25 unakuta Wachagga 17.Wewe waache waendelee kuwasimanga Wasukuma,2025 si mbali watakuja,unless wameamua kura za Wasukuma hawazitaki tena.
Mwaka 2015 CHADEMA walipata viti 4 kati ya 6 vya Ubunge mkoani MARA lakini MARA hawakupewa mbunge hata mmoja wa viti maalum.

Na mwaka huo wa 2015 nilikuwa Kilosa, wanawake walijituma sana kupambania CHADEMA tena kwa mkoa wa Morogoro ambao haukuwahi kutoa mbunge wa upinzani lakini CHADEMA wakapata viti 3. Lakini cha kushangaza viti maalum anaewakilisha Morogoro akateuliwa mchagga Joyce Minja wakati huo alikuwa Ripota wa ITV kutokea Morogoro. Wale wanawake wa CHADEMA Morogoro wakatupwa.

Hawa watu kuwa nao makini. Cheka nao lakini ukiwa na akili zako kichwani.
 
luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
8,162
2,000
Yani tumkatae Magufuli kisa tumfurahishe Kigogo na Chadema? Kwanza nani ana shida ya kura kati ya Wasukuma vs CHADEMA,nilidhani ungewashauri CDM wacheze siasa safi na waondoe hii dhana ya kuhusishwa na chuki za Kigogo vs Wasukuma,au wao kura za Wasukuma hawazitaki? JPM alikuwa ni Pure Msukuma and yes we are proud kutoa Rais Msukuma hapa Tanzania.
Akawasaidia nn? Mbona mikoa yenu ni maskin sana kitakwimu?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,725
2,000
Wasukuma ndio kabila kubwa Tanzania ndio jamii ya watu wengi zaidi.

Ni wapole kwa asili vinginevyo hizi dharau zilizoibuka kuanzia 2015 kama wangekuwa ni watu wakorofi leo hii Tanzania ingewaka moto.

JPM ameshazikwa na hawezi kujitetea, kwa maadili ya kawaida tu sio ustaarabu kumkejeli aliyekwisha ondoka milele.

Natumaini wale members humu ndani wenye akili za kikubwa hawatachoka kuwafunza maadili wale wote wasioifahamu hatari ya kuhubiri ukabila na ubaguzi wa kikanda.

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila ktk siasa zetu.

..kiongozi wa nchi anazungumza kwa kutumia lugha ya kabila lake mlitegemea wale wasio wa kabila lake watamuelewa vipi?

..na alipokuwa akipiga kampeni kwa Kisukuma wewe ulikuwa mmoja wa wachangiaji wa hapa JF mliomtetea bila kuchoka.

..Ni matumaini yangu kwamba Watz tutajifunza kutokana na makosa ya Magufuli, na tutaazimia kuyarekebisha.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,754

Kuongea kisukuma mbele ya wasukuma haikuwa dhambi pengine kati ya hao aliyoongea nao kisukuma wapo hawajui kiswahili.

Hakuna mbunge mchagga aliyekatazwa kuongea kichagga mbele ya hadhira ya wachagga.

Hayupo mwanasiasa ambaye akiwa na wa kwao hachomekei maneno machache ya lugha ya kwao.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,725
2,000
Kuongea kisukuma mbele ya wasukuma haikuwa dhambi pengine kati ya hao aliyoongea nao kisukuma wapo hawajui kiswahili.

Hakuna mbunge mchagga aliyekatazwa kuongea kichagga mbele ya hadhira ya wachagga.

Hayupo mwanasiasa ambaye akiwa na wa kwao hachomekei maneno machache ya lugha ya kwao.
..mchagga angekampeni kilugha ingekuwa tatizo kubwa kwake na chama chake.

..vilevile tume ya uchaguzi imekataza wagombea kuzungumza kikabila.

..maelekezo ya sheria / tume ni kwamba wagombea wazungumze Kiswahili na kama kuna wasioelewa watafsiriwe hotuba na mkalimani.

..Ni bahati mbaya sana kwamba Magufuli alivunja sheria ya uchaguzi waziwazi na hakukuwa na mtu au mamlaka yoyote ya kumkemea.

..Magufuli ndiye aliyeuchochea ukabila hapa nchini. Na vita yake dhidi ya Chadema na kampeni kwamba ni chama cha wachagga matokeo yake tunayaona sasa hivi.
 
koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
670
500
Hii karata ya ukabila ukiachia mbali Rais aliepita hutumiwa hata na ccm yenyewe. CUF waliisingizia ya wazanzibar na ni waislam wanaotaka kuvuruga amani ya nchi. Cuf ikayumba. Sasa hivi CDM wanasema ni chama cha wachagga ila this time hawakufaulu kukiuwa chama hicho kipo kinachechemea. Ccm imekuwa ikichezea amani ya nchi kama kitenesi. Generation ijayo watakuwa na mtazamo mwingine na hawatachotwa na hizi propaganda hatarishi na mapinduzi ya kiutawala na kisera yatakuja ba hakuna atakae zuia.
 
..kabla ya kuitwa chama cha wachagga cdm iliitwa chama cha wakatoliki, enzi zile km ni dr.slaa.

..halafu kulikuwa na chama cha udp kilichoanzishwa na john cheyo. Chama hicho kilisingiziwa kuwa ni cha wasukuma kwasababu cheyo ni mwenyeji wa bariadi shinyanga.
 
koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
670
500
..kabla ya kuitwa chama cha wachagga cdm iliitwa chama cha wakatoliki, enzi zile km ni dr.slaa.

..halafu kulikuwa na chama cha udp kilichoanzishwa na john cheyo. Chama hicho kilisingiziwa kuwa ni cha wasukuma kwasababu cheyo ni mwenyeji wa bariadi shinyanga.
Nakubaliana na wewe. Unajua ukikosa hoja unaishia kuingia kwenye mbinu chafu. Naona sasa mbinu imebadilika ni vita juu ya wasukuma na wachagga. No hizi ni siasa sio makabila tumepoteza direction completely.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,357
2,000
Nipo natafakari namna nchi hii imekuwa, hakuna jambo baya kama kumtambua mtu na kumponda kwa kutumia kiashiria cha kabila lake.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya watumiaji wa mitandao hasa katika maswala ya kisiasa kutumia neno SUKUMA GANG kama utambulisho wa watu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli.

Binafsi neno hili naona linaweza leta matatizo ya kijamii kama ambavyo maneno Intarahamwe, facism, na mengine ya namna hiyo yalivyopelekea matatizo kwenye jamii

Hivyo kutokana na neno hili kuwa na mlengo wa kibaguzi na chuki ni heri mamlaka kupiga marufuku matumizi ya neno hili pia niwaombe wahusika wanaotumia neno hili kuacha mara moja.
Naunga mkono hoja, na leo ndio the Gang has officialy been disbanded kwenye huu uteuzi mpya.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,357
2,000
Bado aisee usitudanganye msomi, kunanakina Dotto hawajatoka wote waziri na KM, halafu kuna Mwigulu and the likes. So bado wapo
Japo the Sukuma gang ni just fictions, sio kila Msukuma aliyekuwa top was a member na pia japo jina ni Sukuma Gang, sio kila aliyepo ni Msukuma !.

The Sukuma Gang ni kile kikundi kidogo cha watu waliofanya siri kuugua kwa naniliu, na hata alipo nanilii, hawakutoa taarifa on time kuwa naniliu amaisha nanilii, wakitafuta jinsi ya kuzuia nanii asiwe ni yeye. Wasukuma wengine walikataa na aliyewadhibiti the Sukuma Gang, pia ni Msukuma.
Wasukuma ambao hawakuguswa, hawahusiki. Ile hoja ya kuchota mihela kwenye kibubu chetu ilikuwa ni uongo tuu na uzushi wa yule mzushi wa Twitter.
P
 
Sumve 2015

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
3,774

Jitu Zuma ovyooo...
 
Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,052
2,000
Japo the Sukuma gang ni just fictions, sio kila Msukuma aliyekuwa top was a member na pia japo jina ni Sukuma Gang, sio kila aliyepo ni Msukuma !.

The Sukuma Gang ni kile kikundi kidogo cha watu waliofanya siri kuugua kwa naniliu, na hata alipo nanilii, hawakutoa taarifa on time kuwa naniliu amaisha nanilii, wakitafuta jinsi ya kuzuia nanii asiwe ni yeye. Wasukuma wengine walikataa na aliyewadhibiti the Sukuma Gang, pia ni Msukuma.
Wasukuma ambao hawakuguswa, hawahusiki. Ile hoja ya kuchota mihela kwenye kibubu chetu ilikuwa ni uongo tuu na uzushi wa yule mzushi wa Twitter.
P
Well nakubaliana nawe lakini kumbuka nami namaanisha hao wachache niliowataja wapo kwenye hiyo gang especially huyo KM aliplay directly wakati wa maficho ya kifo Cha nanihii ili waweze kunanihii zile nanihii kule BOT na wakaendelea kumpanga nanihii ndio awe nanihii walihakikisha nanihii hapewi nafasi kwa kutumia hoja dhaifu za kikatiba ambazo zilikataliwa na msukuma mwenzao ambae alistukia huo mchezo wao na akawatosa.

So bado wapo although wanazidi kupungua nguvu maana jina linabeba wengi waliokuwemo humo pamoja nakubaliana nawe kwamba wapo ambao hawapo kwenye hiyo origin ya hilo jina kama bwana yule aliyepandishwa kutoka kuwa mwalimu wa chuo mpaka kufikia kuwa mtumishi namba moja🤷
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom