The lost
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 2,695
- 8,209
Nipo natafakari namna nchi hii imekuwa, hakuna jambo baya kama kumtambua mtu na kumponda kwa kutumia kiashiria cha kabila lake.
Hivi karibuni kumezuka tabia ya watumiaji wa mitandao hasa katika maswala ya kisiasa kutumia neno SUKUMA GANG kama utambulisho wa watu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli.
Binafsi neno hili naona linaweza leta matatizo ya kijamii kama ambavyo maneno Intarahamwe, facism, na mengine ya namna hiyo yalivyopelekea matatizo kwenye jamii
Hivyo kutokana na neno hili kuwa na mlengo wa kibaguzi na chuki ni heri mamlaka kupiga marufuku matumizi ya neno hili pia niwaombe wahusika wanaotumia neno hili kuacha mara moja.