Msamiati mpya wa SUKUMA GANG haufai, unaweza kuleta matatizo kwenye jamii hapo baadaye. Mamlaka ziliangalie hili

Hahaha, umeandika yote Ila hiyo sentence ya mwisho umeharibu mzee. Huyo kijana Hana usafi wowote aisee kwanza sababu alikuwa member wa level ya juu sana kwenye Ile gang pia baada ya michezo yake mingi aliyopiga pasi za moja kwa moja na uncle wake....
Utakuwa unamuonea bure kijana. Yeye alikuwa ni mtu tuu wa kutumwa kama kikaragosi. Mhusika mwenyewe yaani sterling ni yule naniliu, sasa kwa vile kikawaida kwenye movie sterling hauwawi, ikitokea sterling amekufa kweli, huo ndio mwisho wa hiyo movie, lakini kwa vile sterling kafa, tusitake kuwauwa na wale wasaidizi wake wote, let them keep playing roles kwenye movies nyingine and you never know one day one of them anaweza na yeye kuja kuwa sterling.
P
 
Kama unakumbuka kilichowapata Hitler na wafuasi wake akina Himler basi hata hawa watu walipaswa kuadhibiwa vilevile.

Bahati mbaya sana sisi waafrika tumekubali wahuni kujificha kwenye defense ya kwamba nilikuwa natumwa au natekeleza amri, sasa unajiuliza huyu aliwezaje kutekeleza amri ambayo ni unlawful???? Halafu hii kitu hapa karibu ndio imekuwa defense inayokubalika tu kirahisi kabisa.

Nakumbuka wale waliomshauri Mkapa kuidhinisha malipo ya Rada na watu wa Richmond waliadhibiwa despite ya utetezi wao kwamba boss aliidhinisha, au walitekeleza maagizo maana kikwete hakuwa na huu mzaha kabisa. Siku hizi wale walitekeleza amri za Utawala wa awamu iliyopita wote utasikia wanamruka boss wao wakati walikuwa wanamjaza ujinga mpaka akanogewa kutaka kubadili Katiba bila kujua kwamba walikuwa wanataka abaki ili wao nao wabaki.

Hakuna mtu msafi labda Advocate Mnyele na yule mshkaji mwingine Wakili aliteuliwa UDAS kule Tabora wakatosa. Hao wengine kwakweli they are guilty as he is.
 
Nipo natafakari namna nchi hii imekuwa, hakuna jambo baya kama kumtambua mtu na kumponda kwa kutumia kiashiria cha kabila lake.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya watumiaji wa mitandao hasa katika maswala ya kisiasa kutumia neno SUKUMA GANG kama utambulisho wa watu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli.

Binafsi neno hili naona linaweza leta matatizo ya kijamii kama ambavyo maneno Intarahamwe, facism, na mengine ya namna hiyo yalivyopelekea matatizo kwenye jamii

Hivyo kutokana na neno hili kuwa na mlengo wa kibaguzi na chuki ni heri mamlaka kupiga marufuku matumizi ya neno hili pia niwaombe wahusika wanaotumia neno hili kuacha mara moja.
Ngoja tuwapukutishe kwanza serikalini halafu ndio tutaacha, hili ni genge haram, ni lazimu liwe eliminated completely.
 
.....View attachment 2066131
Screenshot_20220102-161121.jpg
 
Ukimrejesha Mwalimu Nyerere akikuta tunadiscuss huu upuuzi ataamua kurudi alipotoka bila kuaga. Alipambana kwa kutumia nguvu zote lakini leo tunashabikia vikundi vya kikabila hovyo kabisa.
 
Nipo natafakari namna nchi hii imekuwa, hakuna jambo baya kama kumtambua mtu na kumponda kwa kutumia kiashiria cha kabila lake.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya watumiaji wa mitandao hasa katika maswala ya kisiasa kutumia neno SUKUMA GANG kama utambulisho wa watu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli.

Binafsi neno hili naona linaweza leta matatizo ya kijamii kama ambavyo maneno Intarahamwe, facism, na mengine ya namna hiyo yalivyopelekea matatizo kwenye jamii

Hivyo kutokana na neno hili kuwa na mlengo wa kibaguzi na chuki ni heri mamlaka kupiga marufuku matumizi ya neno hili pia niwaombe wahusika wanaotumia neno hili kuacha mara moja.
JPM alitaka ku "sukumanize the Public service"alijaza wasukuma wengi kwenye utumishi wa umma,mashirika ya umma,kwenye wizara nyeti,fedha,mambo ya nje.
Ulikuwa wakati wa sukuma cartel kula nchi.Thank God,kifo kikafanya yake.
Na Hawa sukuma gang au cartel ndio wanaomsumbua mama.
Hawaamini kilichotokea.
Bora mama hana ubaguzi wa kijinga wa kabila,yeye apige tu,uzenj na ubara.
 
Nipo natafakari namna nchi hii imekuwa, hakuna jambo baya kama kumtambua mtu na kumponda kwa kutumia kiashiria cha kabila lake.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya watumiaji wa mitandao hasa katika maswala ya kisiasa kutumia neno SUKUMA GANG kama utambulisho wa watu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli.

Binafsi neno hili naona linaweza leta matatizo ya kijamii kama ambavyo maneno Intarahamwe, facism, na mengine ya namna hiyo yalivyopelekea matatizo kwenye jamii

Hivyo kutokana na neno hili kuwa na mlengo wa kibaguzi na chuki ni heri mamlaka kupiga marufuku matumizi ya neno hili pia niwaombe wahusika wanaotumia neno hili kuacha mara moja.
Naunga mkono hoja, sio limaweza kuja, tayari limeisha anza mdogo mdogo kwa watu kunyooshewa vidole na kubaguliwa kuwa ni Sukuma Gang!.
Wanabodi,
As days goes by, hizi issues za hii kitu inayoitwa Sukuma Gang is escalating to the point of unbecoming!. Sukuma gang ni itikadi siyo kabila
Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na Magufuli inayoamini katika ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.
Si kweli!. The Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!.
Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la Wasukuma. Mfano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni Sukuma gang lakini siyo Msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k.
Pia sii kweli!, bali baada ya Kigogo wa Twitter kuliasisi kundi hili fictitious, akatumia nguvu kubwa kulifanyia indoctrination kuwa hili kundi does real exist, hivyo wale watu wa Magufuli na watu wote wanaomsupport Magufuli wakawa pointed kuwa ni members wa Sukuma Gang, hata mimi ni Msukuma, na namsupport Magufuli na sio Sukuma Gang!.
Lakini wapo Wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.
Hakuna kitu kama hiki, ila kwa vile indoctrination ya existence ya uwepo wa kundi hili imefanyika na watu wenye akili fupi waliofilisika kisiasa wakaamini', kama na wewe unaamini kuwa kundi la Sukuma Gang kweli lipo and does exist in reality, ujijue ni akili fupi and muflis kisiasa kama wale muflis wengine wote wanaoamini ujinga huu!
Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa Sukuma gang ni kuchukia Wasukuma. Hili siyo jambo zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.
Hapa nakuunga mkono!.
Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia Sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni Msukuma.
Kumchukia mtu yoyote kwasababu yoyote sio jambo jema!. Dini zinatufunza hata adui mpende!. Hivyo it's not right kumchukia mtu yoyote!.

Japo hii shana ya the existence of the Sukuma Gang ni dhana tuu, na the Sukuma Gang ni just a fictitious Group that doesn't exist in reality, lakini kufuatia indoctrination iliyofanywa na yule Kigogo wa Twitter, watu wenye akili ndogo, akili fupi na waliofilisika ki fikra, wakaamini, hivyo chuki dhidi ya Wasukuma is real!. Hili sio jambo jema!.

Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa Tanzania kuliko makabila yote, zikitokea nafasi zozote za uongozi, na watu wote wako huru kugombea, obviously Wasukuma pia lazima watakuwepo.

Kulitokea nafasi fulani za uongozi ndani chama fulani, wakajitokeza wagombea 186 kugombea nafasi 8 aa uongozi. Miongoni mwa waliojitokeza walikuwepo Wasukuma wengi tuu ila mimi nawajua kulikuwa na Wasukuma wawili ambao kama wangepitishwa wangetupatia wawakilishi wazuri the best of the best.

Ikasemekana kuwa mmoja kati ya hao Wasukuma wawili ni member wa the Sukuma Gang!. Then kwenye mchujo ikaelezwa kuwa wamepewa maelekezo hatua ya kwanza kabisa ni kuwakata Wasukuma wote waliojitokeza!. Na kweli Wasukuma woote tukakatwa eti ni Sukuma Gang!. This is not fair at all!. Taifa linakosa uwakilishi wa watu wazuri kwa ubaguzi wa kijinga kabisa!.

Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma!. Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!.

P
 
Sukuma gang ni kikundi cha kihalifu. Mtu yoyote anayejumuika na wenzake kufanya, kuchochea au kushabikia uhalifu ni muhalifu.

Sukuma gang ni kama panya road tu
 
Back
Top Bottom