Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,989
- 2,954
[https://res]Wanabodi,
Naomba kuanza kwa declaration of Interest
Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wachache waliowahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa maandiko yangu, ya kulituhumu Bunge kujipendekeza kwa serikali, hivyo inaweza kuonekana nafurahia kinachompata Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai!. No!. Huyu ni Mkuu wa Mhimili wa Bunge wenye jukumu la kuisimamia serikali, haitakiwa Spika kujipendekeza kwa Executive, inambidi Mkuu wa Executive amuogope na kumheshimu Mkuu wa Bunge na Mahakama, siungi mkono jinsi Job Ndugai alivyodhalilishwa vile pale juzi.
Hili ni bandiko la kupinga ubatili unaendelea katika hili sakata la Spika. Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, kwanza niliuliza, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kisha nikauzungumzia msamaha batilifu, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! ambao ulikataliwa, na mara baada ya msamaha huo kukataliwa nikauliza tena Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?
Jana barua hii ya taarifa kwa umma toka kwa Spika kuwa ameandika barua ya kujiuzulu uspika
View attachment 2071447
imesambaa kote. Kama ni kweli hii ndio barua ya Spika Job Ndugai kuuarifu umma kuwa ameandika barua ya kujiuzulu uspika, na kuipeleka kwa Katibu Mkuu wa CCM, kiukweli this looks fake!, ila kama sio fake, then tumsamehe bure Mhe. Job Ndugai, huku kutakuwa ni kutokana na kuchanganyikiwa tuu, barua hii nayo ni barua batilifu!, kwasababu kujiuzulu kwake kumekuwa addressed to a wrong person and to a wrong Institution. Bunge ni mhimili, Mkuu wa mhimili wa Bunge hawezi kujiuzulu kwa barua batilifu na tukaacha tuu hivi hivi, what precedence tunaweka for records?.
Nashauri barua hii ikataliwe, Spika aandike a proper letter ya kujiuzulu kwenye a proper Bunge letterhead kama hii View attachment 2071452
Nakiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kumsoma mwana je huyu
Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist
it's true Job kachemsha!, barua ya kujiuzulu uspika ilipaswa kupelekwa kwa katibu wa Bunge, CCM ndio wanapewa copy. Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa Bunge la CCM. Usika wake ni kwa mujibu wa katiba, na kujiuzulu pia kumeelekezwa na katiba anaandika barua kwa nani, na sio kwa CCM!.
CCM ilimpendekeza tuu, baada ya kuchaguliwa, anakuwa ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM!, hivyo hata kujiuzulu, anajiuzulu kwa kumuandikia Katibu wa Bunge na sio Katibu wa CCM!. Kama Spika wa Bunge anayepaswa kuijua katiba na kuifuata, anaweza kujiuzulu kwa barua ya kienyeji namna hii, then this is a disgrace kwa nafasi ya Spika!.
Huu sio utaratibu wa kufuata wakati wa kujiuzulu kwa Spika wa Bunge. Ingekuwa anajiuzulu kwa kujivua uanachama wa CCM hivyo kupoteza uSpika hapo ndipo anapeleka barua ya kujiuzulu kwenye chama chake, hata angekuwa amejiuzulu ubunge, barua ya kujiuzulu inakuwa addressed kwa Spika wa Bunge. Japo chama ndicho kimemdhamini kugombea ubunge, na uspika lakini baada ya kuchaguliwa mbunge au Spika, umechaguliwa na Watanzania/Bunge la JMT, unawajibika kwa Bunge na sio kwa chama chako.
Kikatiba, Spika wa Bunge akijiuzulu anatakiwa kufanya kutumia Ibara ya 149(1)(c) ya Katiba ya JMT inayosema iwapo Spika wa Bunge atajiuzulu, basi taarifa ya kujiuzulu aliyoiandika na kuitia sahihi yake ataiwasilisha kwenye Bunge.
Inakuwaje anaipeleka kwenye chama na Bunge lipokee nakala kutoka kwenye chama? . Msameheni bure tuu, Spika atakuwa amechanganyikiwa, maada kwa jinsi alivyokuwa anauringia na kuutambia, "mimi ni mhimili" halafu ghafla unatakiwa kuutema uspika, hata ningekuwa mimi, lazima mtu uchanganyikiwe!
Naendelea kusisitiza Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Bunge ni mhimili, Spika anapatikana kwa mujibu wa katiba, na akijiuzulu pia anajiuzulu kwa mujibu wa katiba, hawezi kujiuzulu tuu hivi kienyeji enyeji kwa ubatili na kukubaliwa, hata kama ni kujiuzulu, then ajiuzulu kwa mujibu wa katiba, kama kifungu hiki kilivyoeleza
Mkuu Ukwaju thanks kwa kifungu hicho.
Hii tabia ya kuacha na kupuuzia mambo madogo madogo haya ya ubatili, it is now unbecoming, kuna siku tutajikuta tunatengeneza taifa la ubatili. Kama Katiba ndio sheria mama, na imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, there is no options and no negotiations katiba ifuatwe ajiuzulu properly kwa mujibu wa katiba na kujulia mafao yake manene ya 80% ya mshahara na marupurupu ya Spika.
Nakutakia Kustaafu Kwema, ndugu yangu na rafiki yangu, Job Ndugai.
Paskali
Baada ya kuibuka kwa mitazamo tofauti baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu, tumemtafuta aliyekuwa Spika wa Bunge kuanzia 1994 hadi 2005 Pius Msekwa kwaajili ya ufafanuzi.
Msekwa ameeleza kuwa taratibu zote zimefuatwa na hakuna kilichoharibika kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
''Spika amechaguliwa na bunge, kwahiyo utaratibu sahihi barua ya Spika kujiuzulu ni lazima ipelekwe kwenye bunge na isomwe ndani ya bunge'' Spika Mstaafu Pius Msekwa ametoa ufafanuzi.
Zaidi msikilize hapa