Msamaha wa Kodi ya Uingizaji Gari kwa Watumishi wa Umma

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,401
7,307
Wanabodi Salam
Niliomba kujua utaratibu ukoje wa msamaha wa tozo za kuingiza gari kwa watumishi wa umma
Pia ni Watumishi gani wa Umma wana msamaha wa kuingiza magari
Karibuni wadau
 
Serikali iliufuta huo utaratibu msamaha wa kodi
kwa watumishi pia waliopata miaka ya nyuma
magari yao wanapotaka kuyauza lazima walipe
huo msamaha ndiyo waweze kuyauza.
 
Wanabodi Salam
Niliomba kujua utaratibu ukoje wa msamaha wa tozo za kuingiza gari kwa watumishi wa umma
Pia ni Watumishi gani wa Umma wana msamaha wa kuingiza magari
Karibuni wadau

cha kushangaza bado wabunge wanaopokea pesa nyingi wao bado wanamisamaha hii ya kodi,wapi usawa? wafanyakazi wanalipa kodi nyingi sana,kwa mfano,
1.mshahara wake unalipa kodi ya kichwa ambao hakuna mtu wa kawaida analipa
2.mshahara wake unalipa vat
3.mfanya kazi atakapokwenda kununua kitu dukani,bado analipa kodi juu ya kile kitu alichonunua
Lakini bado ananyimwa haki nyingi kwa mfano hawezi kuingiza gari toka nje lazima alipie kodi na upandishwaji wa madaraja kazini umekuwa ni tabu na hata kama ukipandishwa kupata stahili yake ni mpaka kwa mbinde.
Nchi ya srilanka,kila baada ya miaka 5 mfanyakazi wa serikali anapewa kibali cha kuingiza gari moja bure,sasa ni yeye ataamuwa kukiuza kibali kile ama anunue gari na kuliingiza kwa kutumia kibali husika.
Nini tatizo kwa Tanzania? kwanini wafanyakazi hawapewi msamaha kama ule wanaopewa wabunge?
 
Mkuu, huu msamaha haukuwa reasonable. Ni vema kama umeondolewa.

Watu walipe kodi ili kujenga nchi.
 
Wanabodi Salam
Niliomba kujua utaratibu ukoje wa msamaha wa tozo za kuingiza gari kwa watumishi wa umma
Pia ni Watumishi gani wa Umma wana msamaha wa kuingiza magari
Karibuni wadau

Upo mkuu,ni mwez uliopita tu jamaa yangu anaefanya kazi TRA namanga amenufaika,fuatilia vizuri kwa mwajili na tra watakuelekeza,ila ninachojua HAZINA watakulipia aina mbili za kodi na ww utalipa moja tu
 
Wataalam wa kodi tililiken si mmesoma kwenye importduty. Kule kwenye East Africa Customs and duties au ndio mnasahau kwavile hamvifanyii kazi ?
Nataka kujua kwa mifuko ya pension kama nayo ni mashirika ya umma
Pili ni kwa nn misamaha ni wa wale viongozi wa juu na sio wa chini?
 
cha kushangaza bado wabunge wanaopokea pesa nyingi wao bado wanamisamaha hii ya kodi,wapi usawa? wafanyakazi wanalipa kodi nyingi sana,kwa mfano,
1.mshahara wake unalipa kodi ya kichwa ambao hakuna mtu wa kawaida analipa
2.mshahara wake unalipa vat
3.mfanya kazi atakapokwenda kununua kitu dukani,bado analipa kodi juu ya kile kitu alichonunua
Lakini bado ananyimwa haki nyingi kwa mfano hawezi kuingiza gari toka nje lazima alipie kodi na upandishwaji wa madaraja kazini umekuwa ni tabu na hata kama ukipandishwa kupata stahili yake ni mpaka kwa mbinde.
Nchi ya srilanka,kila baada ya miaka 5 mfanyakazi wa serikali anapewa kibali cha kuingiza gari moja bure,sasa ni yeye ataamuwa kukiuza kibali kile ama anunue gari na kuliingiza kwa kutumia kibali husika.
Nini tatizo kwa Tanzania? kwanini wafanyakazi hawapewi msamaha kama ule wanaopewa wabunge?
Umenena vema mkuu,niliwahi kuhoji kwa wanaojua ni kwa nini mfanya kazi hapewi TIN number kama ilivyo kwa walipa kodi wengine? sikuwahi kupata majibu ya kuridhisha. Nilitamani mfanyakazi awe na namba yake ya utambulisho wa mlipa kodi,mwajiri wake apeleke yale makato yaingizwe kwenye namba ya mfanya kazi husika kama inavyofanyika kwenye mifuko ya hifadhi za jamii, utaratibu wa sasa haumtendei haki mfanyakazi.
 
Mkuu nadhani usikate tamaa,hoja yako ipo wazi na nzuri,kwanini hawawapi TIN wafanyakazi ingawaje wanataka kodi nyingi zisizo na maelezo? na kuna baadhi ya wafanyakazi unakuta mshahara mzima unaishia ktk makato ya kodi na hafaidiki na kodi hizo,ni vyema kuanzia sasa mfanyakazi akafaidika na kodi anayokatwa,maana kufanya kazi serikali si kosa na adhabu yake si kukatwa makodi mengi kama ilivyo sasa
 
cha kushangaza bado wabunge wanaopokea pesa nyingi wao bado wanamisamaha hii ya kodi,wapi usawa? wafanyakazi wanalipa kodi nyingi sana,kwa mfano,
1.mshahara wake unalipa kodi ya kichwa ambao hakuna mtu wa kawaida analipa
2.mshahara wake unalipa vat
3.mfanya kazi atakapokwenda kununua kitu dukani,bado analipa kodi juu ya kile kitu alichonunua
Lakini bado ananyimwa haki nyingi kwa mfano hawezi kuingiza gari toka nje lazima alipie kodi na upandishwaji wa madaraja kazini umekuwa ni tabu na hata kama ukipandishwa kupata stahili yake ni mpaka kwa mbinde.
Nchi ya srilanka,kila baada ya miaka 5 mfanyakazi wa serikali anapewa kibali cha kuingiza gari moja bure,sasa ni yeye ataamuwa kukiuza kibali kile ama anunue gari na kuliingiza kwa kutumia kibali husika.
Nini tatizo kwa Tanzania? kwanini wafanyakazi hawapewi msamaha kama ule wanaopewa wabunge?

Unaongelea wabunge gani? Hawa wabunge wetu wabinafsi wachumia tumbo? hawa hawa wenye kuchukua pesa za safari wakatia takoni na kutulia bila kufanya kazi? HAWANA MUDA HUO MKUU, WEWE FANYA YAKO, KIVYAKO TAFUTA NJIA YA KUPUNGUZA MAKALI YA KODI ONEVU!
 
Mkuu nadhani usikate tamaa,hoja yako ipo wazi na nzuri,kwanini hawawapi TIN wafanyakazi ingawaje wanataka kodi nyingi zisizo na maelezo? na kuna baadhi ya wafanyakazi unakuta mshahara mzima unaishia ktk makato ya kodi na hafaidiki na kodi hizo,ni vyema kuanzia sasa mfanyakazi akafaidika na kodi anayokatwa,maana kufanya kazi serikali si kosa na adhabu yake si kukatwa makodi mengi kama ilivyo sasa
Mkuu naamini humu jf wapo watu wa kada zote na wanaweza kulifanyia kazi hili kama hawajavaa miwani ya mbao
kwa faida zao binafsi.

Leo hii kuna malalamiko mengi kwamba watu wanakwepa kodi,lakini ukiangalia mfumo hauwafanyi watu kupenda kulipa kodi,kutegemeana na walipakodi wananufaika nini tofauti na wakwepa kodi,jibu ni hakuna,kama ni barabara tunatumia wote,miundo mbinu ya maji na umeme wote n.k nigeshauri kama walipa kodi wote watatambuliwa kwa namba ya mlipa kodi iwe aliyeaajiliwa au mjasiliamali na wakapewa upendeleo maalum ikiwa ni pamoja na hili la kuingiza gari walau moja kama kuwaenzi walipakodi waaminifu hata kama wataweka viwango maalum,hili lingehamasisha watu kulipa kodi wenyewe bila kulazimishwa.

Kwa sasa inasikitisha kusikia kwamba wazee wamepewa msamaha nawaziri mkuu kutibiwa bure bila kujali ni nani alichangia ujenzi wa taifa enzi za ujana wake na ninani alikuwa anacheza bao wakati wote,kundi kubwa la waajiliwa ndio wanakuwa victimized maana wenzao wafanya biashara wana TIN mfanyakazi hana TIN na ukistaafu kitambulisho cha kazini unarudisha na hivyo kuonekana mtaani kama mtu aliyekuwa anazurura wakati wa ujana wake.

Natamani wahusika,watunga sera na sheria viongozi wa vyama vya wafanya kazi waliangalie hili kwa maslahi ya wafanyakazi wote na wakulima watakaolipa kodi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom