Ukweli ni kuwa hiyo misamaha waliokuwa wanapewa wafanyakazi wa serikali tu na si wafanyakazi wote ni wa kibaguzi na haufai. Hivi kuajiriwa na serikali ni tofauti na kuajiriwa na mashirika ya umma, makampuni ya binafsi, kwa wahindi, wazungu au waswahili?
Serikali ni mwajiri kama waajiri wengine sasa kwanini wafanyakazi wake tu wapewe misamaha ya kuingiza magari? Ni hawa hawa wafanyakazi wa serikili ambao wanafanyakazi kwa uzembe mkubwa, kupoteza muda na mara nyingi hawapo maofisini au hawatekelezi majukumu na huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa wakati. Eti wao ndo wapewe msamaha wa kodi?
Kwa hiyo tumesoma chuo kimoja, tumepata alama sawa, nakuzidi uwezo au unanizidi uwezo binafsi wa kutafakari na kutekeleza majukumu yangu. Wewe ukaajiriwa serikalini. Mimi nikaajiriwa kampnuni binafsi. Tukitaka kuagiza magari mimi sina msamaha wa kodi wewe unao eti kwa kuwa unafanya kazi serikalini! Ujinga na upendeleo wa wazi. Wafanyakazi wote ni wafanyakazi. si walioajiriwa na serikali tu.
Huwezi kusema misamaha yote ya kodi iondolewe kwa kuwa kuna misamaha inayotumika kuruzuku na kuhamasisha maendeleo ya maswala yanayohitaji kipaumbele. Cha muhimu ni kuangalia vipaumbele vinavotumika kusamahehe kodi ni sahihi.
Kwa mfano kwa sasa tanzania ilipofika kwenye uimarishaji wa uchimbaji madini hakun tena haja kusamehe kodi kwenye vifaa vya uchimbaji madini. Uhamasishaji umeshafanyika, wawekezaji watakuja iwe kuna au hakuna misamaha ya kodi kwenye sekta ya madini.
Na sisi wajasiriamali ambao tumesoma na nyinyi kuanzia msigi mpaka chuo! Nasi twahitaji msamaha!
Mimi siungi mkono misamaha ya kodi ambayo imekaa kibaguzi au upendeleo wowote usio na msingi.Kama ungekuwa mzalendo wa kweli ungesema misamaha yote ifutwe.
Mtoa mada alichosema ni kuhusu utaratibu wa kuondoa msamaha kwa mfanyakazi wa serikali ambaye anapata msamaha baada ya miaka 4 na si wote wanaotumia huo msamaha.
Lakini wakati huo huo wanaacha misamaha kwenye makampuni hasa ya madini ambayo yanapata msamaha kila siku.
Kumbuka pia wafanyakazi ndio wanaoongoza kwa kulipa kodi ya mapato kuliko hayo makampuni.
Ungeeleweka kama ungedai misamaha ihusishe wafanyakazi wote.
Ila wewe kushangilia eti wafanyakazi kuondolewa ahueni ya kodi ni matatizo ya ...
Nimeshtushwa na kitendo cha Mgimwa kufuta msamaha wa kodi....
Hivi kumpa ofa mfanyakazi kama huyu msamaha wa kuagiza kagari kake ka kwendea kazini tena msamaha huo ni baada ya miaka minne kuna tatizo gani? au ndo njia ya kuwafundisha wale rushwa ili wawe na uwezo wa kuagiza magari mapya?
Kama ungekuwa mzalendo wa kweli ungesema misamaha yote ifutwe.
Mtoa mada alichosema ni kuhusu utaratibu wa kuondoa msamaha kwa mfanyakazi wa serikali ambaye anapata msamaha baada ya miaka 4 na si wote wanaotumia huo msamaha.
Lakini wakati huo huo wanaacha misamaha kwenye makampuni hasa ya madini ambayo yanapata msamaha kila siku.
Kumbuka pia wafanyakazi ndio wanaoongoza kwa kulipa kodi ya mapato kuliko hayo makampuni.
Ungeeleweka kama ungedai misamaha ihusishe wafanyakazi wote.
Ila wewe kushangilia eti wafanyakazi kuondolewa ahueni ya kodi ni matatizo ya ...
Hapo hapo kulikuwa na walimu wanamagari 4 lakini wanatembelea miguu!!shule nzima inaonekana walimu wake wote wanamagari!!watumishi wa serikali walisha fanya miradi!! lakini hata mwenye pikipiki hakuna sasa hapo unaweza kuona wapi kulikuwa na sababuNimeshtushwa na kitendo cha Mgimwa kufuta msamaha wa kodi kwa waagiza magari kwa wote waliokuwa wananufaika nao. Naomba tuelewane ni nani hasa msamaha huu ulikuwa unamfaidisha. Kwanza lzm tuelewe kuna Gvt officers na Gvt leaders.
Gvt leaders hawa ni wala nchi ambao kwenye package zao wanapewa transport, housing na mishahara ya juu kwa level za kiserikali. Hawa ndo hasa wanufaika wa semina, safari lukuki za nje na ndani ya nchi na marupurupu kibao. Kimsingi hawa ni wachache lkn ndio hao wanaomiliki mahekalu huko mbezi beach, oysterbay, masaki nk. hawa kumiliki gari sio issue, wana gari la serikali la kisasa lenye service na dereva bure, wanamiliki magari binafsi kibao nk.
Sasa hawa Gvt officers majority, ukiacha wingi wao ni wasomi wazuri tu, wengi huko serikalini, wakilipwa chini ya laki tano, wabangaizaji. Hivi kumpa ofa mfanyakazi kama huyu msamaha wa kuagiza kagari kake ka kwendea kazini tena msamaha huo ni baada ya miaka minne kuna tatizo gani? au ndo njia ya kuwafundisha wale rushwa ili wawe na uwezo wa kuagiza magari mapya?
Wahadhiri wetu wa vyuo vyote, walimu, na maafsa wa kawaida wamenufaika na kumuona Rais Mkapa kama mtu aliyejali kuinua hadhi zao. Nina uhakika watumishi hawa kilio chao mtakisikia kama alivyokianzisha Dr. Bana, achana na itikadi zake, ila na uhakika kama serikali haitakuwa sikivu lzm iadhibiwe kwa hili. Iweje bwana mahela Barrick asiguswe niguswe mimi mla chaki?
Ngoja tuone.
Ni sawa kabisa, msamaha ulikuwa umekaa kiupendeleo, kwanini uwe kwa wafanyakazi wa serikali tu? Wamerudisha usawa.