Msamaha wa kodi kwa watumishi wa umma kufutwa. Imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha wa kodi kwa watumishi wa umma kufutwa. Imekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjenda Chilo, Jun 16, 2012.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nimeshtushwa na kitendo cha Mgimwa kufuta msamaha wa kodi kwa waagiza magari kwa wote waliokuwa wananufaika nao. Naomba tuelewane ni nani hasa msamaha huu ulikuwa unamfaidisha. Kwanza lzm tuelewe kuna Gvt officers na Gvt leaders.

  Gvt leaders hawa ni wala nchi ambao kwenye package zao wanapewa transport, housing na mishahara ya juu kwa level za kiserikali. Hawa ndo hasa wanufaika wa semina, safari lukuki za nje na ndani ya nchi na marupurupu kibao. Kimsingi hawa ni wachache lkn ndio hao wanaomiliki mahekalu huko mbezi beach, oysterbay, masaki nk. hawa kumiliki gari sio issue, wana gari la serikali la kisasa lenye service na dereva bure, wanamiliki magari binafsi kibao nk.

  Sasa hawa Gvt officers majority, ukiacha wingi wao ni wasomi wazuri tu, wengi huko serikalini, wakilipwa chini ya laki tano, wabangaizaji. Hivi kumpa ofa mfanyakazi kama huyu msamaha wa kuagiza kagari kake ka kwendea kazini tena msamaha huo ni baada ya miaka minne kuna tatizo gani? au ndo njia ya kuwafundisha wale rushwa ili wawe na uwezo wa kuagiza magari mapya?

  Wahadhiri wetu wa vyuo vyote, walimu, na maafsa wa kawaida wamenufaika na kumuona Rais Mkapa kama mtu aliyejali kuinua hadhi zao. Nina uhakika watumishi hawa kilio chao mtakisikia kama alivyokianzisha Dr. Bana, achana na itikadi zake, ila na uhakika kama serikali haitakuwa sikivu lzm iadhibiwe kwa hili. Iweje bwana mahela Barrick asiguswe niguswe mimi mla chaki?

  Ngoja tuone.
   
 2. No admission

  No admission JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi sikuafiki utaratibu walio uchukua na wabunge ambao wanapewa ma Land cruiser walishangilia sana alipo soma hii section ya kufuta msamaha na kupunguza muda wa uchakavu kutoka miaka 10 hadi nane. Hawa wabunge hawajakaa na kufikiri kwanini biashara ya nguo za mitumba inashamiri kila kukicha badala ya kufifia?

  Jibu maisha ni magumu wananchi tunateseka hata kale kadogo tulikokuwa tunaambulia wamekafunga. ETI WANAPUNGUZA MISAMAHA YA KODI. VIPULI VYA MASHINE YA KUCHIMBIA MADINI KODI ASILIMIA 0 WALACHAKI, ASKARI, NA MADAKTARI HAKUNA TAX EXEMPTION YA VIUSAFIRI VYAO.

  KWELI TUTAKUMBUKA BUSARA ZA MHESHIMIWA MKAPA. Hii serikali kila mtu anataka aonekane shupavu lakini maamuzi wanayo fanya hayatumii akili. Anyway 2015 is not far we must remove these people in power... M4C
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ni sawa tu. Utaratibu huo ulikuwa wa kibaguzi sana! Na kulikuwa na abuse kubwa tu kwenye misamaha hiyo.
   
 4. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Rudia kuusoma huu uzi kisha changia. Lazima utofautishe hawa waheshimiwa na watenda kazi serikalini. Kwa vi mishahara vyao hata mikopo benki haizidi mil kumi. stuka mku
   
 5. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjenda Chilo!

  Wewe kweli **** hivi mtu akinunua gari unasema linamsaidia au linamwongezea gharama. My take hawa wafanyakazi na Watanzania and actually most Africans are born in poverty . Zile Enzi za kuona mwenye kumlilki gari kwamba ni symbol of prosperity are gone!

  Chanzo kikubwa cha rushwa kwa watumishi wa umma ni ujinga wao wa kuingia Mkenge wa kununua Magari tena mengi yakiwa yametumika miaka kumi Huko Japan , uaarabuni na ulaya. Hawana uwezo wa kuyatumia kutoka gharama kubwa haswa mafuta na matengenezo. Matokeo yake wanaishia kuwa ombaomba.

  Mara nyingi huchukua mikopo kutoka Mabenki au Saccos na kukatwa RIBA kubwa so we have a lot of corrupt officials kuanzia wakurugenzi Hadi wafagizi.

  Serikali sio tu inatakiwa kufuata misamaha ya kodi kwa wafanyakazi hata mashirika ya dini kwani yote yanafanya biashara kuanzia Makanisa , misikitini na kuendelea . Inatakiwa neno misamaha ya kodi na Ruzuku yafutwe kwenye kamusi Bali iwe ni kosa kulitamka. Misamaha ibakie kwenye kusameheana makosa au dhambi na si vinginevyo. Hata katika msahafu mmoja imeandikwa "Kila mtu atauchukua Mzigo wake mwenyewe"

  Mzee Msuya the respected very senior citizen an economist a former finance minister and Prime Minister aliyasema hayo maneno kwa vile ni ukweli mpaka leo watu wengi hawajamwelewa.

  Nature ya misamaha ni ya kibaguzi na dhambi ya ubaguzi has no limits it's a vicious circle they come and go. To recap Enzi za Ruksa akina Malecela waliuza Magari yote as its a burden to the nation. Awamu iliyofuata ya Mkapa walinunua Magari kibao and alipo kuja Vasco Da Gamma ile fleet ya Ikulu ilibadilishwa with posh gas guzzlers na Ministers wakanunua V8 that is why expenditure is 70% and Ccm thinks they still have the mandate to rule/ lead?.. upuuzi mtupu waangalie?.
   
 6. D

  Danho Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii serikali ya CCM ilipotufikisha inatosha..! Ila 2015 sio mbali... M4C ndo kila kitu.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa nini iwe wafanyakazi wa serikali tu? Watanzania wengine hawastahili?
   
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  biashara za wakubwa bwana hizi usihoji sana..pita pita pale mitaa ya fire kama unaeleka kariakoo utaona bonge la YARD ya magari linamilikiwa na mtoto wa MUKULU...
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwahiyo walimu na madaktari hawana msamaha wa kodi!
   
 10. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana. Hili la kufuta exemption ni goligota kwa watumishi wenye mipango ya kununua magari. Nami naungana na wenzangu, muda utawahukumu wanaokubaliana na ufutwaji wa msamaha huu.

  Mtumishi huyu anakatwa kodi kibao bila kuwa na uwezo wa kujitetea. Mtumishi wa seriakali hawezi kukwepa kodi na hela yake inakatwa hata yeye hajapokea malipo ya jasho lake. hana hiari wala nafuu ya kodi sasa kwa hili mimi nafikiri ni suala la wafanyakazi tuungane na tuwe na maamuzi thabiti.

  Ukifuatilia, bajeti za Tazania hazikuwahi kumpa nafuu mfanyakazi hasa wa serikali. Mtumishi wa serikali anapata nyongeza ya chini ya Sh 10,000.00 kwa mwezi eti mshahara umeongezwa! Wakati gharama za item 1 zinaongezeka maradufu. Pengine tunaomba TUCTA itoe tamko, angalia wanatupa kidogo kwa mkono wa kushoto huku wanachukua kikubwa kwa mkono wa kulia.

  Lakini nasema ni haibu kwa serikali iliyoahidi maisha bora kwa mipango ya namna hii. Mipango yao imeshindwa kuweka mazingira mazuri bandarini ambako taifa lingeweza kukusanya fedha za kutosha kuendesha mipango yake bila kuwakamua "wavujajasho". Siyo haki. TUCTA mko wapi?
   
 11. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama ungekuwa mzalendo wa kweli ungesema misamaha yote ifutwe.
  Mtoa mada alichosema ni kuhusu utaratibu wa kuondoa msamaha kwa mfanyakazi wa serikali ambaye anapata msamaha baada ya miaka 4 na si wote wanaotumia huo msamaha.

  Lakini wakati huo huo wanaacha misamaha kwenye makampuni hasa ya madini ambayo yanapata msamaha kila siku.

  Kumbuka pia wafanyakazi ndio wanaoongoza kwa kulipa kodi ya mapato kuliko hayo makampuni.

  Ungeeleweka kama ungedai misamaha ihusishe wafanyakazi wote.

  Ila wewe kushangilia eti wafanyakazi kuondolewa ahueni ya kodi ni matatizo ya ...
   
 12. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Tathmini nzuri sana...
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Ni sawa kabisa, msamaha ulikuwa umekaa kiupendeleo, kwanini uwe kwa wafanyakazi wa serikali tu? Wamerudisha usawa.
   
 14. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Tunabishana au kuchangia kwa hoja. mambo ya u **** naomba ukamuulize bibi yako. Nani kakwambia kwamba a car is still an oestantencious good? gar ni necesity mzee. Zama za mabasi ya wafanyakazi haipo leo, na kama unajua kitu chochote kuhusu HR management, incentive ni kitu muhimu sana katika perfomance. Kwani civil servant ni mtumwa? awe na vigezo vya juu ili apate kazi yet alipwe kidogo, why? tatizo siasa uchwara kila kona.

  Tuchukie ufisadi kwenye sekta ya umma, tutambue wenye uwezo wa kufanya ufisadi, tuwamulike, then tutambue na kuheshimu kazi za watenda kazi serikalini, tuziheshimu, tutambue changamoto kali wanazozipata kwa hawa wayumbisha nchi mostly policy makers a.k.a. politians, then tutambue umuhimu wao, elimu zao na motisha zao. Tukipiga siasa kila angle hakuna mtu wala chama kitakachokuwa na uwezo wa kutawala/kuongoza. Cheap politics. lol!
   
 15. T

  Thesi JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kuwa hiyo misamaha waliokuwa wanapewa wafanyakazi wa serikali tu na si wafanyakazi wote ni wa kibaguzi na haufai. Hivi kuajiriwa na serikali ni tofauti na kuajiriwa na mashirika ya umma, makampuni ya binafsi, kwa wahindi, wazungu au waswahili?

  Serikali ni mwajiri kama waajiri wengine sasa kwanini wafanyakazi wake tu wapewe misamaha ya kuingiza magari? Ni hawa hawa wafanyakazi wa serikili ambao wanafanyakazi kwa uzembe mkubwa, kupoteza muda na mara nyingi hawapo maofisini au hawatekelezi majukumu na huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa wakati. Eti wao ndo wapewe msamaha wa kodi?

  Kwa hiyo tumesoma chuo kimoja, tumepata alama sawa, nakuzidi uwezo au unanizidi uwezo binafsi wa kutafakari na kutekeleza majukumu yangu. Wewe ukaajiriwa serikalini. Mimi nikaajiriwa kampnuni binafsi. Tukitaka kuagiza magari mimi sina msamaha wa kodi wewe unao eti kwa kuwa unafanya kazi serikalini! Ujinga na upendeleo wa wazi. Wafanyakazi wote ni wafanyakazi. si walioajiriwa na serikali tu.

  Huwezi kusema misamaha yote ya kodi iondolewe kwa kuwa kuna misamaha inayotumika kuruzuku na kuhamasisha maendeleo ya maswala yanayohitaji kipaumbele. Cha muhimu ni kuangalia vipaumbele vinavotumika kusamahehe kodi ni sahihi.

  Kwa mfano kwa sasa tanzania ilipofika kwenye uimarishaji wa uchimbaji madini hakun tena haja kusamehe kodi kwenye vifaa vya uchimbaji madini. Uhamasishaji umeshafanyika, wawekezaji watakuja iwe kuna au hakuna misamaha ya kodi kwenye sekta ya madini.
   
 16. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mshahara wa serikali unaujua au unausikia? acha propaganda wewe, laki tatu halafu class nilikuwa mkali zaidi yako. yeyote mwenye akili timamu lzm ahoji subiri kiwake hapo chuo ndo utanielewa vizuri
   
 17. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba wafanyakazi wa serikali walikuwa wananufaika na misamaha ya kodi za magari,ni sehemu ya motisha kwao kwani scale za mishahara yao siyo kubwa ukilinganisha na private firms.ukisema wafanyakazi wa serikali ni wazembe,wazururaji na wasiowajibika hii siyo kweli.wapo wachache ni wazembe kweli lakini wengine ni wachapakazi kwelikweli.kilichotakiwa ni kuweka usawa japo wa aina fulani mathalani serikalini wasamehewe kwa 40%na private firms kwa 30% ili kuweka uwiano wa kunufaika na msamaha ukilinganisha na mishahara yao.KUSAMEHE MAKAMPUNI YA DHAHABU NI UHALIFU MKUBWA NA KUISALITI NCHI.
   
 18. B

  Bob G JF Bronze Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Waache walipe kodi hawa wafanyakazi waliacha kumchagua Dr Slaa alie waahidi kuwaongeza mshahara na badala yake wakampa JK alie kataa kuwaongeza mshahara tena na kuwambia kama kura ninyimeni watu laki tatu hamtishi bado hao watumishi walishiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha anapata urais.

  Watanzania tulivo wa ajabu hata tukiambiwa na ccm tulipie hii hewa hata kama hela hatuna tungelipia 2 Mtu unajiuliza na shida zote hizi why ccm bado inatawala?
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  waondoe misamaha ya kodi sawa.......na pia waache michezo yao ya "ku-uplift".......
   
 20. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Serikali ilikuwa ina nia nzuri ya kutoa msamaha wa wafanyakazi wa serikali maana wengi wao walikuwa na kipatao cha chini lakini ukweli ni kwamba nafasi hiyo imetumiwa vibaya na baadhi ya watumishi kwa mfano waalimu wengi walikuwa wanatumiwa na wafanyabiashara kuagiza magari kupitia majina yao maana mwl wa primary huyo hana ndoto ya kuja kujipatia gari lake.

  Ukiangalia upande wa pili baadhi ya waliokuwa wanania ya kweli wamepatwa na pigo kubwa. mtazamo wangu serikali ingeangalia upya sheria hii ka mapana zaidi ili kudhibiti udanganyifu wa watu kutumia majina ya wafanyakazi wa serikali ili kupata msahama wa serikali pili kuhusu gari lenye umri wa miaka minane hapo mi kwakweli napongeza ki ukweli madhara ya magari machakavu ni makubwa kuliko tunavyofikiria kuna watu wanavyofikiria najua linatuumiza sote ila hatuna kukubali hili.

  Alternative hakikisha unafanya mapinduzi ya kweli 2015 ili upate fursa maalumu ya kutoa manung'uniko yako yote hayo usijali mkuu serikali kilichobaki ni kutukomoa tu maana miaka hii iliyobaki kila mtu anahakikisha yupo vizuri maana kuna giza nene kuanzia pale tarehe 28 october 2015 siku ya jumapili hapo kuna vumbi ambalo hakuna mtu anajua linakuja na vumbi gani.
   
Loading...