Msamaha wa kodi kwa wafanyakazi SERIKALINI.

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Wanajamvi habrini.

Kuna jamaa ni ofisa mkubwa serikalini, sasa katika pitapita zangu, nimeifuma barua yake, akimwandikia katibu mkuu wake ili amwidhinishie aingize gari free bila kulipia zile kodi za kuingiza gari nchini.

Lakini nimekumbuka katika mawasilisho ya bajeti ya dr. Mgimwa, alifuta hiyo ofa ambayo baadhi ya maofisa waliona ndo njia ya kutokea, kwa kuingiza magari halafu wanakuja kuyauza.

Sasa swali ni, je, waziri mgimwa katika kuhitimisha, aliamua kuachana na mpango wake wa kuwafutia wafanyakazi wa serikali?

Au mimi sikumwelewa vizuri waziri mgimwa?

Naombeni majibu yenu wanajamvi
 
Ukipata majibu ya marufuku ya matumizi ya mashangingi serikalini iliyowekwa na Nyooka (Tafuta kinyume), utakuwa umepata na majibu ya Ngimwa
 
Wewe umeliona hilo la kusamehewa kodi kwa huyo mtumishi anayeaagiza starlet !!!! Nenda TRA wakwambie kiasi kinachosamehewa. Masharti ya kuuza gari lililosamewa kodi ni kukaa na hilo gari kwa muda wa miaka mitano au kama unaliuza kabla ya muda huo kumalizika, unapaswa kulipa kodi uliyosamehewa au anayelinunua alipie kodi hiyo. Ni sawa kama ukinunua gari kwenye taasisi ambayo ilisamehewa kodi.
 
duh, mtihani mkubwa. Nisaidie tafadhali....
Kuna mahali unaweza ukaona kuwa mtu anamanisha anachosema.
Lakini hapo kwa wote Nyooka na Ngimwa ni KEKUNDU wala hawamanishi wasemayo.
Aliikuwa anaipaka rangi bajeti yake ivutie kwa Wabunge na Wapuuzi wenzake!.
 
kuna mahali unaweza ukaona kuwa mtu anamanisha anachosema.
Lakini hapo kwa wote nyooka na ngimwa ni kekundu wala hawamanishi wasemayo.
Aliikuwa anaipaka rangi bajeti yake ivutie kwa wabunge na wapuuzi wenzake!.

una maana msamaha uko pale pale?
 
una maana msamaha uko pale pale?
Kifupi nimebofya
likex.png
kwenye hii post.
 
duh watu humu wana maneno mengi badala ya kumsaidia wanaongea mambo ya ajabu tu
 
Mkuu hiyo si kweli. Lazima ulipe kiasi fulani ya kodi baada ya kufanyiwa depreciation, hata kama utakaa nalo miaka 10. Sema baada ya muda mrefu unacholipa kinakuwa kidogo sana.
 
nyie naona hamelewi misamaha ya kodi kwa watumishi wa umma alafu mnaendelea kupiga bla bla tu,jaribu kuwa cheki watu tra taxpayer services and education piga 0786 800 000 bure kabisa
 
Back
Top Bottom