msamaha kwa baba tu kwanini

Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,968
1,470
nimesoma post nyingi humu ndani zinaonyesha kama mwanamke anapokosa mfano amecheat haitaji msamaha hapo hapo nikiwasoma wanaume wanavohalalisha kuwa na mahusiano nje ya ndoa zao kwanini wamama tu ndo hawaitaji msamaha lakini wanaume kwao ni sawa wafanyayo
 

Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,968
1,470
naona wakaka mnaikimbia post yenu kwanini mbona hamtaki kunipa majibu
nimesoma post nyingi humu ndani zinaonyesha kama mwanamke anapokosa mfano amecheat haitaji msamaha hapo hapo nikiwasoma wanaume wanavohalalisha kuwa na mahusiano nje ya ndoa zao kwanini wamama tu ndo hawaitaji msamaha lakini wanaume kwao ni sawa wafanyayo
 

vegule

Senior Member
Dec 17, 2010
121
3
naona wakaka mnaikimbia post yenu kwanini mbona hamtaki kunipa majibu
Ngoja nijitolee kukujibu chauro. Mimi naamini msamaha unatakiwa utoke pende zote ila si katika makosa ya kucheat. Kwa mfano kama mke wangu akicheat na mimi najua nilishamcheat, sioni tatizo la kutomsamehe nikitambua udhati wa nia yake. Ngoja nimalizie valeur yangu kwanza.
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,567
2,805
I have yet to hear a man ask for advice on how to combine marriage and a career
 

klorokwini

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
8,662
5,031
mimi nitajibu kama lawyer mzoefu katika hii sekta.

vipengele vinavyofanya wanaume kuwa wazito kusamehe kuliko wanawake ni kama vifuatavyo:-
-mwanamke akicheat, anauza hisa zote za ndani ya nyumba na mamlaka anakuwa nayo bwana wake wa nje so mipango ya nyumbani kwako itakuwa inapangwa na njemba hostel baada ya kutoana kijasho na waifu wako. tafauti na mwanaume akicheat anakuwa yeye anangonoka tu lakini mamlaka ya nyumba yanakuwa kama kawa
- wanaume naturally wameumbwa kutokutosheka na mwanamke mmoja, hii haina ubishi kabisa. sasa limwanamke kucheat ni against nature kabisa yaani.
- mwanamke akicheat anapoteza confidence kwa mume wake, lazima maraha ya nyumbani yatapungua tu, lakini mwanaume anaweza akawa na wanawake sita na still wote wanaweza wakapata dozi na wakakimbia kwa dozi kali (reference marehemu akuku danger)
- mwanamke ameumbwa na extra uvumilivu na upendo ndio maana anabeba mimba na kulea, mwanaume ameumbwa na ukatili by nature, ndio maana wanaume wanapelekwa vitani.

konklusheni: sikatazi watu kusameheana lakini najaribu kuonesha kwamba ni ngumu kusamehe mwanamke kuliko kusamehe mwanaume kwenye hii sekta.

hehe acha nisubiri mashambulizi kwa wana beijing
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,725
104,908
nimesoma post nyingi humu ndani zinaonyesha kama mwanamke anapokosa mfano amecheat haitaji msamaha hapo hapo nikiwasoma wanaume wanavohalalisha kuwa na mahusiano nje ya ndoa zao kwanini wamama tu ndo hawaitaji msamaha lakini wanaume kwao ni sawa wafanyayo

Nitajiongelea mwenyewe kwenye hili.

Kwangu mimi uzinzi ni kosa ambalo halisameheki. Kama nimezini mimi basi mwenzangu ana haki zote za kuniacha. Na nikibaini kuwa mwenzangu naye kazini nje basi uhusiano wetu unakuwa historia papo hapo. Hili ni kosa lisilo na mjadala kwangu.

Mwisho wa siku ni juu ya mhanga mwenyewe kuamua afanye nini. Akiamua kusamehe na kuendelea kubaki kwenye uhusiano basi huo ni uamuzi wake na wengine hamna budi kufunga midomo yenu. Akiamua kufungasha vyake na kutimua, hiyo kwangu ni sawa pia.

Ila pia wapo wanaume wanaosamehe na kuendelea kubaki kwenye huo uhusiano na ndio maana hapo juu nimesema inategemea na mtu na mtu. Mimi nina mifano mitatu ya wanaume ambao wanawake zao walizini na wakawasamehe na kuendelea nao.

Ila kwangu mimi hapana kabisa na nina msimamo. Vilevile kwa vile sipendi mwenzangu azini nami sizini. I am a big subscriber to the 'golden rule' when it comes to that aspect of a relationship. Do as would be done.
 

RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,933
1,951
Msamaha unatoka kwa mkosewa....sioni mantiki ya wanawake kulalamika kwamba kwa nini wao wanasamehe kirahisi (tena wengine hutoa msamaha wa kudumu, kwa maana kosa ni la kila mara).
its all a natural way.
nawapongeza wanawake kwa roho zao za huruma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom