Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 131
Hivi mmeona wapi steji ya kuperform ambayo haina taa? Hivi inawezekana vipi flash ya wasanii inagoma kusomeka?
Hayo yametokea jana kwenye kwenye Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Msama Promotions pale Uwanja wa Taifa.
Katika harakati zangu za kuendelea kutafuta mlango wa kurudi kundini, jana nikasema ngoja nikaburudike na wasanii wa Injili pale Uwanja wa Taifa. Watu walikuwa ni wengi na wamejaa shamrashamra za sikukuu ya Pasaka.
Mshangao wangu wa kwanza nikaupata kutoka kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa ni waziri wa Mambo ya Ndani. Kaka yangu Mwigulu akaanza kuleta stori za siasa kwenye Tamasha la Kidini. Akatumia kama takribani dakika 45 kusifia serikali na kupiga vijembe vya hapa na pale vya kisiasa. Mpaka watu wakachoka na kuanza kupiga matarumbeta mfululizo wakiashiria kuwa wamechoka kumsikiliza na wanataka wasanii waanze kuperform..."wacha maneno, weka muziki." Wanasiasa bhana.....wanapiga ramli hata kama kuna njiwa weupe kibao wanaruka angani kwa furaha. Anyway, ya ngoswe tumuachie ngoswe...
Sasa basi, haikuchukua muda mwingi tangu wasanii waanze kuperform, baada ya Waziri kumaliza ufunguzi, giza kuanza kuingia. Doh kumbe steji haina taa bhana. Sasa sijui haikutarajiwa kuwa Tamasha lingeendelea mpaka zaidi ya saa 12 jioni au la! Lakini niliambiwa kuwa Tamasha kama hili huwa linafungwa saa 2 usiku. Anyway, ikabidi wasanii waikache steji na kushuka kwenye majani ili wavizie mwanga wa taa za uwanja.
Haya, ikafika zamu ya Kwaya ya Barabara ya 13 (kama sijakosea jina) kuperform. Ile moja ya Kwaya anzilishi ya nyimbo za Injili nchini, kwenye miaka ya 90. Ile iliyoimba nyimbo za Samsoni, Noah na kadhalika. Basi wakapeleka flash yao kwa Dj ili aiweke. Doh flash isigome kusomeka saa ngapi! Nikasikia MC anashauri wanakwaya wakapande stejini (gizani) na wakaimbe laivu kwa kutumia vifaa vya bendi. Masikini wanakwaya wakawa hawajiandaa na kupiga laivu. Ikashindikana! Basi, MC ikabidi atumie busara ya kuiita Kwaya inayofuatia...Kwaya ya Olyankuru (spellings). Toba...flash yao nayo si ikagoma kusomeka!! Nikajiuliza...hivi kwani hizi flashes huwa haziwi-tested kabla ya shughuli kuanza? Kwanini Dj hasi-test na kukusanya nyimbo zote kwenye flash/kifaa kimoja na kuzipangalia kulingana na performance za wasanii? Hii ni fedheha!
Anyway, nashukuru lakini nilienjoy kumuona Rose Muhando. What an electrified performance!! Rose, baby, hakika wewe bado ni Diamond Platnumz wa Bongo gospel music. Mpaka push-ups ulipiga...hats off!
Oh kidogo nisahau hii....si ikafika zamu ya msanii mwalikwa kutoka South Africa (jina nimelisahau). Msama Promotions si wakaenda kununua bulbs za majumbani na kuzifunga stejini bhana....hehehehe kazi kwelikweli!