~^^*^^~ msaliti ~^^*^^~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~^^*^^~ msaliti ~^^*^^~

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 11, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  MSALITI

  Na. M. M. Mwanakijiji


  Nilihisi kuna mtu amesimama karibu na kochi nililokuwa nimejilaza. Ni ile hisia ambapo bila kuangalia nyuma unahisi kuna mtu anakunyemelea au kuna mtu anakuangalia na unapogeuka unakuta ni kweli. Nilikuwa nimejilaza chali kwenye kochi kubwa la rangi nyeusi huku Radhiya akiwa bado amekaa juu yangu. Shanga zake zikiwa zinaning’inia na kugusa kiuno changu. Kiunoni mwake alikuwa amejifunga kanga tu, tulikuwa tumeloa jasho, miili imechoka huku usingizi ukitupitia taratibu. Ilikuwa ni mara ya pili ndani ya saa moja tulifanya mapenzi ya nguvu.

  Hisia hiyo ya mtu kuwa karibu ilinishtua mimi na kabla sijafanya lolote Radhiya naye alishtuka pia. Tulipofumbua macho yetu tulipigwa na butwaa la mwaka. Mke wangu Husna, alikuwa amesimama pembeni ya kochi tulilokuwa tumejilaza. Mkononi alikuwa ameshika kisu kikubwa chenye ncha kali kilichokuwa kinameremeta. Alikuwa amekunja uso wake, huku machozi yakimtoka na midomo ikimtetemeka. Kabla sijapata nafasi ya kusema Radhiya alijiondoa kwa nguvu na kuruka pembeni huku akishikilia kanga iliyokuwa ikimning’inia. Hakufanya ajizi alinyakuwa mkoba wake uliokuwa mezani na funguo za gari lake na kukimbilia mlangoni huku akijaribu kujisitiri na kanga yake. Alitoweka.

  Nilijaribu kuinuka haraka kumuwahi Husna kabla hajafanya uamuzi atakaojutia milele, lakini sikuwa na bahati hiyo. Husna alikiteremsha kisu chake kwa nguvu zake zote za kikike, kama vile mkulima anavyoshusha jembe kwenye ardhi ngumu. Ncha ya kisu ilipenya upande wangu wa kushoto wa kifua changu. Kama vili pini inavyopenya kwenye karatasi, ncha ya kisu ilikita ndani ya moyo wangu. Nilijaribu kupiga kelele, hata hivyo nilichoweza kusema ni “Ahhhh”. Maumivu makali yaliingia katika kila kona ya mwili yangu. Nilijaribu kuuzuia mkono wake asikandamize hicho kisu. Sikufanikiwa kwa hilo pia. Husna alikuwa amepania. Alikichomeka kisu kwa nguvu zaidi huku akikitingisha juu na chini.

  Damu ilianza kunivuja kwa wingi, mwili wangu uliokuwa umeloa jasho sasa ulikuwa kama ardhi iliyokuwa tepe kwa mvua. Damu ilisambaa kifuani na ilitiririka kwenye kochi na sakafuni. Kiza kilianza kuniingia. Nilijaribu kujitahidi kufumbua macho kumwomba Husna msamaha, sikuweza. Husna alibakia akiniangalia jinsi uhai ulivyokuwa ukinitoka taratibu. Nilijuta kumsaliti mke wangu, nilijuta kuwasaliti watoto wangu, nilijuta kuisaliti dini yangu na ndoa yangu. Sikuweza kuomba msamaha kwa mke wangu wa miaka minne. Nilitamani muda urudi nyuma na malaika ashuke kuniokoa. Swala zangu hazikujibiwa. Mauti yalinifika taratibu.

  Kwa mbali nilisikia sauti za watu zikisogea karibu na nyumba yangu iliyoko eneo la Isamilo Mwanza karibu na Maghorofa ya NBC. Neno la mwisho nililolisikia ilikuwa ni sauti ya Husna:

  “Utangulie kuzimu!”


  * * * ​
  Husna alifikishwa kwenye kituo cha Polisi cha Kati kilichoko kando ya Ziwa Victoria karibu na jengo la makao makuu ya CCM Mwanza. Aliingizwa katika chumba cha kutolea ushahidi ili aandike maelezo yake kabla ya kupelekwa rumande ambapo atasubiri kufikishwa mahakamani. Maelezo ya Husna yalikuwa yakichukuliwa na mpelelezi Richard Fundi, mmoja wa wapepelezi vijana wa Idara ya Upepelezi ya mkoa wa Mwanza. Richie (kama alivyojulikana mtaani) alikuwa ni mpepelezi aliyehitimu mafunzo yake huko Uingereza kwenye chuo cha New Scotland Yard.

  “Jina lako tafadhali” Aliuliza Mpel. Richie
  “Naitwa Husna Mohammed Ali” Alijibu Husna huku akimtaza mpelelezi huyo aliyekuwa akiandika majibu yake hayo. Pembeni kulikuwa na kaseti rekoda, iliyokuwa ikirekodi mahojiano hayo.
  “Tafadhali tueleze ilikuwaje uamue kumuua mumeo Bw. Mohammed Ali” Aliuliza mpelelezi huyo.

  Husna alianza kusimulia kisa kizima cha mkasa huo.

  * * * ​
  Nilipigiwa simu na rafiki yangu ambaye alinidokeza kuwa anafahamu kuwa mume wangu alikuwa na mwanamke mwingine aliyekuwa akimleta nyumbani kila mara nyingi ninapokuwa kazini hasa wakati wa mapumziko ya mchana. Mara kadha wa kadha nilijaribu kukanusha madai hayo kwani nilijua mume wangu asingefanya vitendo kama hivyo na alinipenda kwa dhati. Kila kitu nilichotaka alinipa na mimi nilijitahidi kwa kila hali kuwa mke mwema na mama mzuri kwa watoto wangu.

  Nilikuwa ni mzuri wa kuzaliwa kwa tabia na kwa umbo. Niliurithi uzuri huo toka kwa mama yangu. Nilikuwa ni mahiri kitandani na sikumnyima mume wangu mahaba ya kweli na nilikuwa na uhakika kuwa na yeye alikuwa haninyimi kitu. Alinipa nami nikampa. Tulijaliwa watoto wawili Husein na Rehema. Tulijaliwa nyumba nzuri na miradi kadha wa kadha ambayo mimi niliisimamia. Hakuna kitu nilichotaka ambacho hakunipa. Hivyo tetesi za kuwa mume wangu kuwa hakuwa mwaminifu nilizitupilia kando. Niliita ni wivu wa jirani.

  Hata hivyo miezi michache iliyopita, mume wangu amepunguza hamu yake kwangu. Nimejaribu kuweka kila aina ya vikolombwezo ili kutia sukari zaidi katika penzi letu na ndoa yetu bila mafanikio. Nimejaribu kumpa penzi la kushitua, kama akiwa hana hili wala lile nilijaribu kumpa vitu. Zamani alikuwa hapotezi muda alikuwa akinirukia utadhani jogoo liliachiliwa bandani. Hii miezi michache hata hivyo ameanza kunisukuma kando. Zimeanza kupita wiki bila ya mimi kupata “mkuno wa nguvu” wa kuniridhisha roho yangu. Hii ikaanza kunitia wasiwasi, kwani nakumbuka ndoa nyingi huanza kuvunjikia chumbani. Niliamua kufanya uchunguzi wa kina nijue ukweli wa mambo.

  Siku ya tukio, nilimwambie mume wangu kuwa nitaenda huko Kijerezi kumtembelea rafiki yangu na sitarudi hadi jioni. Niliondoka nikiwa nimefungasha vitu vichache kabla yeye hajaondoka kwenda kazini. Sikwenda mbali. Nilijificha nyumbani kwa jirani yangu (aliyekuwa akinipigia simu kunitahadharisha) hadi nilipomuona mume wangu ameondoka kwenda kazini. Nilirudi nyumbani na kujifungia kwenye kabati lililokuwa sebuleni kusubiri ni nini kitachotokea. Kwa vile nilikuwa nimechoka kwa kupanga mipango hiyo, nilipitiwa na usingizi nikiwa nasubiri humo kabatini.

  Sikusikia ni wakati gani waliingia ndani au mambo waliyoyasema na kuyafanya kabla ya mimi kushtuka. Kilichoniamsha katika usingizi wangu humo kabatini ni sauti ya malalamiko ya kimapenzi. Nilifungua mlango wa kabati hilo ili kupata upenyo wa kuweza kuona kilichokuwa kikiendelea. Niliweza kumuona mume wangu akiwa amelala chali, mikono yake ikiwe imezunguka ****** ya mwanamama mmoja ambaye alikuwa amemkalia juu. Huyo mwanamama alikuwa amevalia chachandu za rangi mbalimbali. Niliweza kuona kwa uzuri kabisa mgongo wa mama yule na eneo zima la ajali. Niliweza kumuona jinsi alivyokuwa akimkatikia mume wangu na kumwendesha kama farasi! Masikini mume wangu. Uume wake ulikuwa ukiingia na kutoka ukiwa umeloa na unang’ara kama sime iliyopakwa mafuta! kwa nguvu, huku jasho likiwatoka. Nguo zao zilikuwa pembeni sakafuni. Kulikuwa na kanga kwenye ukingo wa kochi. Ilikuwa ni kanga yangu yenye maandiko “wazuri na wabaya ni walewale”.

  Waliendelea kufanya mapenzi, miye nikiwa nimeshikwa na butwaa na sikujua nifanya nini. Kifundo cha uchungu kilinishika. Walipeana Walipofika kilele yule mwanamke alimuangukia mpenzi mume wangu kifuani. Aliivuta ile kanga na kujifunika kiunoni. Mume wangu aliileta mikono yake kumkumbatia huku akiwa bado ndani yake bila shaka akifurahia masalio ya mlipuko wa volkano. Machozi yalianza kunitoka, nilitamani niruke toka nilikojificha na niwasute hadharani. Nilitamani ulimwengu mzima uje kushuhudia jinsi yule niliyempenda alivyonisaliti. Nikiwa nawaza hayo niligundua kuwa mume wangu ameanza kusinzia (ulikuwa ni udhaifu wake mkubwa akishafanya mapenzi). Na yule mwanamama naye alianza kukoroma kwenye kifua cha mume wangu.

  Nilihakikisha kuwa wamesinzia nilipotoka kwa kunyata na kuelekea jikoni. Nilitamani nichemshe mafuta ya moto niwamwagie. Baada ya kufikiri sana niliamua kuwa anayestahili kuadhibiwa ni mume wangu na siyo yule mwanamke. Huyo mwanamke sikuwa namjua na yeye hakunijua. Niliamua kuchukua kisu cha kukatia nyama na kuamua kulipiza kisasi. Moyo ulinidunda kwa kasi, machozi yalinitiririka upande mmoja, na viganja vyangu vilikuwa vimelowa jasho. Mikono na midomo ilinitetema. Niliapa kwa mizimu ya mababu zangu wa kichaga, nitampa somo la milele. Nilinyemelea taratibu hadi niliposimama karibu ya wapenzi hao wawili. Nilikusudia kuikata shingo ya mume wangu mbele ya mwanamke huyo. Sikutaka kumgusa mwanamke huyo. Niliinua kisu, nikavuta pumzi, na nilikuwa tayari kukiteremsha. Mume wangu alifumbua macho. Kabla sijakiteremsha kisu, yule mwanamke naye alizinduka, akaniangalia usoni. Sikuamini macho yangu! Kabla sijasema chochote na kabla yeye hajasema chochote alikurupuka, akachukua hiyo kanga tu, na mkoba wake akakimbilia nje.

  Mume wangu alitaka kukimbia, sikumpa nafasi. Nilikiteremsha kisu haraka kwenye kifua chake na nilikishindilia kuhakikisha kuwa hataamka milele. Nilisimama karibu kuhakikisha kuwa amekufa. Nilimtakia heri ya kuzimu. Nilikuwa hapo hadi polisi walipotokea.

  * * *​
  “Asante kwa maelezo yako” Mpel. Richie alisema baada ya kuhitimisha kile alichokuwa akiandika.
  “Hata hivyo nina swali moja” Alisema kabla ya kuizima ile rekoda.
  “Uliza” Husna alijibu.
  “Kwanini hukuamini macho yako ulipomuangalia yule mwanamama? Unamjua?” Richie aliuliza akimbulia macho Husna, binti wa miaka ishirini na miwili ambaye licha ya mambo yote yaliyokuwa yakiendelea uzuri wake haukufichika.

  Husna alivuta pumzi ndefu, aliifikicha mikono yake, na alimwangalia mpelelezi huyo kwa muda. Hatimaye alisema,

  “Ndiyo namjua; huyo mwanamke alikuwa ni mama yangu mzazi!”

  Chumba kizima kiligubikwa na ukimya uliokatishwa na kanda ya kurekodia ilipofika mwisho na kujizima. Hawajawahi kusikia kisa cha usaliti wa namna hiyo.


  MWISHO
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Thanks Mwanakijiji hadithi yako ni fupi lakini nzuri sana ina mafunzo ..
  sijaamini kuona mama mkwe nakula tundi na mkwewe...!!!inasikitisha
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mzee Mwanakijiji did it again...

  Dah... Hadithi nzuri, lakini huyu mama.... hata sipati picha...:mad:
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ulikuwa na kamera gani?digital au zile za analogy and manual?:bounce:
   
 5. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  huu ni wazimu wa kiwango cha ushetani!
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kuna watu hawana adabu hata kidogo hivi mpaka mnafikia hatua ya kutongozana na mama mkwe unaanzaje ?
   
 7. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mbona jana sijakuona kwa Msindima??... we nae siku hizi unaongoza kwa sound...

  Nilikuwa natumia manual, nimejaribu ku-zoom kila engo imegoma...
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  SI UNAANZA TU ''...mama,how are you?can i please take you to dinner/club/INDOOR OUTING...!''
  HEHEHEHE!mchakato unaanzia hapo
   
 9. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  In most cases FL1, ni mama mkwe ndo huwa anaanza... mara comment za ajabu, mara mikao ya ajabu, etc
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hehehe!UNANIDHALILISHA SANA,UNANIONEA SANA,UNANISEMA SANA KWENYE JAMBO HILI,NA KWAKWELI HUNITENDEI HAKI KABISA,najua tatizo ni huu uwaziri(sore) ni ukatibu wa kamati

  hivi ulikaa engo gani?mbona mi sikukuona pia?
   
 11. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  He he heee.... zea we go again....
   
 12. JS

  JS JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante MMKJ ni hadithi nzuri sana. Huyo mama mkwe hajatulia kaona mwanae anafaidi sana ikabidi na yeye asikilizie hapohapo.............:A S-eek:
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ndo zako hizo
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kama kawaida!kwani nini bwana!
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Iliyo Mara nyingi anaaanzaga mama mkwe!
   
 16. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hadithi nzuri sana, dah! mshikaji aliamua kula kuku na mayai yake, ila ndo hivyo MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.
   
 17. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  asante kwa hadithi nzuri,ila huyo mama mmhh balaa
   
 18. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,509
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Mkuu MKJJ Ahsante kwa hadithi yako tamu pamoja na ile ya KUMBATIO LA MWENYE HATIA. Kwa hadithi ya leo whether it comes from a true story or just fictious, kwangu napata dhamira mojawapo katika dhamira za Hadithi zote kuwa WANAWAKE WA KICHAGA wanaover react kwenye situation kama hizi kana kwamba Uchagani haya mambo hayatokei.

  Pia naweza kusema kwa uhakika kuwa dhamira nyingine iliyokusudiwa ni kuonesha namna gani WANAWAKE WA KICHAGA WANAVYOWEZA kupanga njama za kumtoa uhai mwanaume kwa lengo la kurithi mali zake kwani isingekuwa hivyo, baada ya Husna kubaini kuwa yule mwanamke alikuwa ni mama yake mzazi, ni kwa nini naye hakumuadhibu..
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  duh.. yaani kutoka kwenye hadithi umepostulate kwa jamii nzima ya watu with no qualification whatsoever? yawezekana msingi wa mahitimisho yako hautokani hata chembe na kisa cha masimulizi.
   
 20. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji!  Annina
   
Loading...