Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu? ikuli ilishiriki kumbena Dr Ulimboka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu? ikuli ilishiriki kumbena Dr Ulimboka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 20, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][​IMG][/h]
  [​IMG]
  Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 11 July 2012

  [​IMG][​IMG]ULIMBOKA ni neno la Kinyakyusa lenye maana ya Mungu uniponye. Neno hilo ndilo linatumika kama jina na ukoo wa Dk. Steven.
  Mtu akiwa kwenye matatizo, shida, mashaka au mateso huomba huruma ya Mungu amponye. Kwa huruma na upendo, Mwenyezi Mungu ndiye aliwashika wasamaria wema, kwa mkono wake wa miujiza, akawaongoza, bila kujijua kwenda kumwokota na kumfikisha hospitalini Dk. Steven Ulimboka aliyepigwa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande akaachwa afe.
  Mungu aliyewaongoza wasamaria wema kumwokoa na kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI), ndiye amemtia nguvu, anazungumza sasa kwa ‘ufasaha’ alivyopigiwa simu na ofisa wa ikulu, alivyotekwa, alivyoteswa usiku kucha na alivyookotwa.
  Hivi sasa anapata matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, akisubiri ubuponyi yaani uponyaji kamili kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.
  Katika mkanda wa mahojiano maalum akiwa MOI, Dk. Ulimboka haachi chembe ya shaka kwamba mkasa huo ulipangwa na kuratibiwa na kikosi maalum cha ‘mauaji’ ambacho kina maslahi na mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa wiki tatu sasa.
  Sehemu ndogo ya maelezo ya Dk. Ulimboka ni kama ifuatavyo….
  …Kazi yao ilikuwa siyo kufanya kazi kama askari, eeh its like they acted under instructions.
  Eeh, yaani unajua, kwa muda kama siku tatu mfululizo, huyu bwana alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumwona.
  Nilishawahi kumwona zamani, kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course alikuwa serious akinitafuta akisema kwamba anataka some hearing ili aweze kushauri. Huyu bwana anafanya kazi ikulu.
  Aah, mimi kwa sababu namfahamu kutokana na incident ya kwanza sikuwa na muda. Lakini jana aka-insist sana na akakaa Hugo pale muda mrefu sana, sisi tulikuwa tumekaa Leaders Club.
  Baadaye nikamwambia Deo kuna jamaa mmoja – ambaye Deo anamkumbuka sana kwa sababu mara zote huwa tunakwenda naye – anataka kutuona. Basi tukawaacha wenzetu wanafanya kazi nyingine, tukaondoka mimi na Deo around saa tano, ilikuwa na robo (5.15).
  Naye akatuarifu kuwa pale Hugo alipokuwa amekaa wanafunga, akawa ameenda kule juu sehemu inaitwa Stereo, akaniambia yupo pale. Mimi nikawasha gari hadi pale, nikaangalia meza ya kwanza pale sikumwona. Tulipoingia pale hatukumwona. Nikazunguka sikumwona, nikampigia simu akaniambia, nakuja hapo sasa hivi.
  It took like twenty to thirty minutes tangu aliposema anakuja. Tukaamua kuwasha gari ili kurudi pale Leaders lakini tukaona kama hilo haliwezi kuwepo. tukaishia pale Tunisia Road kuna kontena, tukakaa pale. Sasa akawa anapiga simu akisema anakuja kuna vitu anamalizia; tukawa tunawaza ni vitu gani?
  Basi tukiwa tumekaa, ghafla tukamwona anafika, kwa gari. Akasema uko na Deo, nikasema eeh. Basi tukaanza mazungumzo.
  Kitu ambacho nili-notice, while tukiwa tuna-discuss naye, akitaka kujua namna gani tuweke understanding; matatizo yetu ni yapi, which are the priority areas, eeh kama alivyosema yeye mwenyewe ili aweze ku-advise, kwa sababu wakati mwingine…
  Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu, akawa anaandika kwenye diary yake, kwa hiyo pia alikuwa very bussy communicating, unaona.
  Kwenye simu yake sasa, tukafika kwamba tumemaliza. Ila sisi tulikuwa tuna vinywaji kwa sababu ilikuwa siyo rahisi sana tumwache yeye aondoke sisi tuendelee kubaki. Yeye alikuwa anakunywa maji akasema bwana mi naondoka.
  Kwenye ile line ya yeye kusema anaondoka tu, hapo hapo wakatokea watu kama wanne watano hivi, wakasema, wakaja straight kwenye meza yetu, as if they were directed. Wakasema upo chini ya ulinzi, yaani mimi hapa. Kama mtu hakujui hawezi kuja saa 5 usiku kuja kukukamata.
  They came direct towards me, nikauliza kwani kuna kosa gani? Wakanipiga mtama nikaanguka barabara ya lami. Nilichokifanya kitu cha kwanza ni kutoa simu na kumpa Deo. Sasa they pushed me na kufanikiwa kuchukua simu moja na wallet yangu.
  Nilichowahi ni kuchomoa simu yangu kumpa Deo. Wakaniburuza huku wakini-push again na kuvuka barabara hadi kwenye gari ile, ilikuwa haina namba ile, ni kama Starlet hivi. Nikaamua tu kubaki patient.
  Wakafungua lango la nyuma wakanitupa huko. Wakaja wakanitupa huko. Basi mmoja akaingia upande wangu wa kulia mwingine wa kushoto. Wakaanza kunipiga ngumi, wakanipiga ngumi; mwingine akanipiga vichwa, naona, wengine wana kama dude fulani kama la plastiki hivi, wananipiga kichwani. Wananiambia tulia tutakuua sisi. Kama una ndugu zako aga kabisa kwa sababu leo hurudi.
  Unatuletea usumbufu sana wewe… sasa nikawa najiuliza usumbufu gani? Kwa sababu hata hapo usumbufu, wewe unajua unachokifanya kwa hiyo tunataka kukomesha hiyo tabia. Wakanipiga kwenye gari hiyo huku inakwenda, ilikuwa inaenda mwendo wa kasi sana. Nikafanikiwa kuchungulia hivi nikagundua tuko maeneo ya Victoria…
  …Hata na ile miguu wakafunga sana. Basi wakaendesha gari, wakaendesha this time muda mrefu sana. Sikuwa najua wanaenda wapi. Walipokuja kunishusha, wakaanza kunipiga tena.
  Sasa kwa sababu I was helpless nimefungwa, basi nikawa napigwa nageuka hivi, nikigeuka hivi, nikaona wananipiga kwa sikio la huku, wengine wakawa wananipiga sikio la huku walinipiga sana kama half an hour hivi, and then I think I lost consciousness.
  Unaona na nilikuwa na-bleed sana wakati ule. Kwa hiyo nilichofanya nikawa napata feelings hawa watu they are carrying me somewhere.
  Nikafika mahali nikaona kama vile wamenitupa kwenye shimo hivi. Sijui kama wanataka kunifukia? Unaona, nikawaambia why I are you burring me alive?...
  Katikati ya mateso kama aliyopata Dk. Ulimboka kuna uponyaji. Kwa kuteswa kwake Yesu Kristo binadamu wamepona (biblia).
  Kwa kujichoma moto, mmachinga wa Tunisia baada ya mgambo na polisi kuvuruga biashara yake, nchi nzima iliwaka moto na Watunisia wakapata demokrasia.
  Kutokana na maandamano katika viwanja vya Tahrir na serikali kujibu kwa risasi, Misri iliwaka moto, hatimaye imefanya uchaguzi huru.
  Watu wote wasio na hofu ya Mungu, ndio wanaweza kujisikia raha kuteka watu wasio na hatia na kuwatesa, wakati mwingine, kwa kufurahia vipande vya fedha.
  Yuda Isikarioti alifurahia vipande 30 vya fedha kwa kazi ya kumsaliti Yesu. Aliishia wapi? Kwa kuteswa kwake Dk. Ulimboka, Mungu atawatia adabu walioratibu mpango huo.
  Gazeti toleo lenye makala hii

  Chanzo Mwanahalisi
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 809
  Trophy Points: 280
  abdulahsaf sawa kabisa hii thread ipo humu ndani ya Jukwaa la siasa na tumeshaichangia pia kuna YouTube nyingi hata za MM Mwanakijiji, si mbaya wakizirudia wasiochangia, kwa leo nasisitiza Mgomo wa Madaktari ulishaisha kwani waliambiwa wasioridhika waache kazi na wamesharejesha Leseni zao, tunachooangalia sasa ni ajali ya meli na matatizo ya bei za mazao yetu.
  Sanasana hao MaDr kama hajaenda huko kusini mwa jangwa la Sahara kutafuta kazi, si vibaya wakarejeshwa kazini (kwenye Hospital za Rufaa, Muhimbili, Ifakara, KCMC, Bugando, Mbeya, Amana na Temeke) baada ya kusamehewa na Mwajiri lakini wapitie JKT kwanza kabla ya Wabunge wakajifunze Uzalendo
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa safarini umerudi lini..... mjadala huu uliletwa na kajadiliwa kwa kirefu tangu makala hiyo ilipotoka gazeti la mwanahalisi
   
Loading...