KAMPUNI ya Udalali ya Yono, imetangaza kuanza operesheni ya kukamata na kufilisi mali za wafanyabiashara wa Zanzibar, waliokwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuanzia kesho.
Kesho ndiyo siku ya 14, miongoni mwa muda waliopewa wafanyabiashara waliokwepa kodi kujisalimisha kwa mamlaka hiyo na kulipa kodi stahiki.
Kampuni hiyo imsema itaanza kukamata magari yote ambayo hayajalipiwa kodi visiwani humo pamoja na maduka, hoteli na biashara mbalimbali.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo, Stanley Kevela wakati akizungumzia maendeleo ya zoezi la kurejesha kodi ya serikali iliyokwepwa.
“Tumewatangazia vya kutosha na tumewapa notisi ya siku 14 ambayo imeshaisha tangu Mei Mosi,” alisema Kavela.
“Sasa baada ya hapo kazi itakuwa moja tu, kukamata mali za wadaiwa ili kuhakikisha fedha za serikali zinapatikana.”
Aliwataka wafanyabiashara waliokwepa kodi ya TRA na kukimbia kujisalimisha kwani watawasaka kokote waliko ili walipe kodi ya serikali.
Kampuni hiyo imepewa zabuni ya kuhakikisha mali za wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kwenye bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi wanakamatwa na kurejesha Sh. bilioni 18.
Kevela alisema zoezi hilo linaendelea vizuri ingawa kumekuwa na wafanyabiashara wachache ambao wamekuwa wakitaka kukwamisha zoezi hilo kwa kugoma kujitokeza kwa hiyari yao.
Alisema kuna kampuni tisa ambazo zimekataa kujisalimisha na kwamba Yono itahakikisha inawasaka kila.
“Wakiendelea kukataa kutoa ushirikiano, tumeshazungumza na polisi. Tutatafuta namna ya kuwakamata wao na mali zao na tunaandaa orodha yao ambayo hivi karibuni tutaiweka kwenye vyombo vya habari,” alisema Kevela.
Aidha, Kavela alisema kuna kampuni mbili za kichina zilizokwepa kulipa kodi ya jumla ya Sh. bilioni 6.5 lakini moja ya kampuni hizo imesharejesha Sh. bilioni 1.5 ilizokuwa inadaiwa.
Alisema Yono itaendelea kuwatafuta wafanyabiashara waliokwepa kodi na ambao wamejificha lakini wasipopatikana kampuni za Bakhresa zitawajibika kulipa madeni yao.
“Mzigo ulipita kwenye bandari kavu ya Azam, wao ndio walikuwa na dhamana ya kuhakikisha mzigo kabla haujatoka kodi ya serikali imeshalipwa hivyo kama hawa wafanyabiashara watakwepa basi mzigo utamwangukia yeye Azam,” alisema
Chanzo: Nipashe
============
Suala langu lipo hapa hivi hawa ZRB inafanya nini Zanzibar na mbona haifanyi kazi Bara???
Eeee Mwenyezi Mugngu tusaidie kwenye Muungano huu usiokua na maslahi ya Zanzibar