Msako kali wa polisi mkoani tanga wafanikisha upatikani wa baadhi ya vitu vya sharo milionea

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,842
2,000
MSAKO KALI WA POLISI MKOANI TANGA WAFANIKISHA UPATIKANI WA BAADHI YA VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOKUWA VIMEIBIWA
Watu wasio na huruma walishindwa kutoa msaada kwa marehemu sharomilionea katika kumuokoa na kuona ni bora vitu alivyokua navyo wavichukue .....

Lakini uchunguzi wa polisi kwa kushirikiaana na wananchi naumeweza kupitisha msako mkali baadhi ya vitu vilivyochukuliwa katika tukio hilo vimepatikana.

AKIONGEA kwa njia ya simu na blog hii, aliekua rafiki wa karibu wa sharo milionea KITALE amevitaja vitu vya marehemu vilivyopatikana ni pamoja na SPEAR TYERE,RADIO YA GARI,BETRI YA GARI,SAA YA MKONONI,na pia kwa masaada ya jeshi la polisi uliweza kusaidia kupatikana kwa simu yake ya mkononi yaSHAROMILIONEA huku vitu vingine ikwemo SURUALI AINA YA JINSI NA T-SHIRT YAKE BADO HAVIJAWEZA KUPATIKANA na polisi jijini tanga wanaendelea na msako wa kuvikamata vitu vingine vilivyopotea katika eneno la tukio 

Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
15,046
2,000
Wakiamua wanaweza. Ila kiukweli Mzizi Mkavu kuwapata polisi wenye maadili 100% haiwezekani na kazi ipo.
 
Last edited by a moderator:

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,811
2,000
Kweli kabisa PoliCCM warudishe kamera ya Mwangosi...wasifanye mambo kuwa double standard,Kwa RPC msako mkali sana hadi wakapatikana,kwa Sharo pia,ingawa najua zile 6m hazitapatikana kamwe,labda nguo na radio ya gari....
 
Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,807
2,000
Tunashukuru kwa taarifa mkuu, kumbe waliiba hadi SPARE TYRE

Huko njia hiyo ni washenzi! mimi mwenyewe nilipata ajali hapo nikanasa ndani ya gari,wakaja wanakiji na mapanga nikadhani wanakuja kuniokoa kumbe wakaniamuru nitoe kila nilichokuwa nacho la sivyo wanimalizie kwa nyundo na mapanga! kwa kuwa nikuwa nimenaswa mguuni na kibini ya gari sikuwa na ujanja walikomba kila kitu hadi waleti yangu! hawana utu njia ile,huo ndio uchumi wanaoutegemea!
 
mwakaboko

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,916
2,000
polisi wakiamua kutenda wezi , vibaka wote watakuwa lupango na watafutika mitaani mwetu, tatizo ni rushwa
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Huko njia hiyo ni washenzi! mimi mwenyewe nilipata ajali hapo nikanasa ndani ya gari,wakaja wanakiji na mapanga nikadhani wanakuja kuniokoa kumbe wakaniamuru nitoe kila nilichokuwa nacho la sivyo wanimalizie kwa nyundo na mapanga! kwa kuwa nikuwa nimenaswa mguuni na kibini ya gari sikuwa na ujanja walikomba kila kitu hadi waleti yangu! hawana utu njia ile,huo ndio uchumi wanaoutegemea!

nahisi hata wanakijiji wale,watakua walimmalizia tu,
 
Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,201
2,000
Huko njia hiyo ni washenzi! mimi mwenyewe nilipata ajali hapo nikanasa ndani ya gari,wakaja wanakiji na mapanga nikadhani wanakuja kuniokoa kumbe wakaniamuru nitoe kila nilichokuwa nacho la sivyo wanimalizie kwa nyundo na mapanga! kwa kuwa nikuwa nimenaswa mguuni na kibini ya gari sikuwa na ujanja walikomba kila kitu hadi waleti yangu! hawana utu njia ile,huo ndio uchumi wanaoutegemea!

Alihojiwa kijana mmoja wa hapo akasema hapo kijijini kwao hakuna hata mwenye pikipiki!. Ila inasemekana vijana wengi wa hapo ni wavivu na si wabunifu wa shughuri halali za kujipatia vipato ukichukulia ardhi ipo ya kutosha. Polisi waanze na hao waliorudisha hivyo vitu,wawabane watataja mpaka hao waliochukua millioni sita.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom