Buyungu ni CCM iwezayo kuleta maendeleo

Msakila KABENDE

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
510
314
Wanajf, salaam!!

Nachukuwa fursa hii kuwapa habari nyepesi na nzito za kuelekea uchaguzi mdogo jimboni Buyungu baada ya kufanya tathmini kwa vyama vilivyojitokeza kuomba ridhaa ya kuchaguliwa.

(i). Mhe Eng Chiza (CCM) - napewa kipaumbele kikubwa cha kushinda uchaguzi huo kwa kuwa ana mambo mengi aliyosaidia wakati akiwa Mbunge (miundombinu ya kilimo, afya, elimu, umwagiliaji, barabara, na wilaya mpya nk. Huyu pia ana nafasi ya kushinda kwa kuwa wana Buyungu wanapenda kuona rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anafanya kazi na mtu mwenye mtizamo chanya na wababaishaji,

(ii). Eliya (CHADEMA) - huyu ni mtu mwenye uzoefu katika udiwani hana sifa nyingi zinazompa nafasi ya ushindi. Hakuna jambo alilowahi kuanzisha kwa fikra na ubunifu wake. Ikiwa huyu atachaguliwa huenda jimbo la Buyungu likapata Mbunge asiyeweza majukumu ya kibunge kwa kuwa hata mbuzi huanzia nyumbani kula mazao - lakini pia diwani huyu hana agenda iwezayo kupimwa badala yake anajijenga ktk kutumia nafasi ya uchaguzi wa kura ya maoni iliyofanyika ndani ya CCM kitambo.

Binafsi namuona mtu huyu akiwa na udhaifu wa kuwa agenda yao ya zamani ya kupambana na ufisadi ndiyo kwa kasi kubwa hufanywa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli - hivyo wanaingia ktk uchaguzi wakiwa hawana agenda muhimu,

(iii). Wasiwasi Kasigara (ACT Wazalendo) - huyu ana hasara kwa kuwa chama chake pekee hakina mizizi kokote jimboni. Lakini pia ni mtu aliyekuwa na historia yoyote katika jimbo la Buyungu. Kwa haraka huyu ni mtu ambaye hata shughuli za kibunge hawezi wala hazifahamu vizuri. Kwa ujumla CCM bado kinaonekana kung'aa kwa wapiga kura kutokana na jinsi kinavyojipambanua kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimboni.

Natumaini kuwa kama wananchi hawatadanganyika basi CCM inashinda katika uchaguzi huu - hata hivyo haimaanishi kuwa kazi ya kupata ushindi ni ndogo. Remains to be my observations.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Msakila Mussa KABENDE
Shuhuda jimboni Buyungu 2018
 
Maoni au uchambuzi wa kipuuzi kama wa kutumwa. Ni kwà sababu hujaingiza matakwa ya wapiga kura
 
Halafu magelemwa mbona unaficha jina?? Halafu usiwe na hasira na uweke akiba ya maneno
 
Biased analysis yaani uchambuzi ulioegemea upande....Mgombea mmoja unaonyesha ubora wake was kuwa mbunge pasi na kutoa madhaifu yake huku mwingine ukizungumzia madhaifu yake kana kwamba hana mazuri....Huu sio uchambuzi
 
Yaani unafanya uchambuzi wa nani bora kati ya ccm,cdm,na Act halafu una declare interest kwamba wewe ni ccm die hard,kisha unafanya lunatic conclusion kuwa ccm ndiyo bora! Unamalizia na Kidumu----zi!! Na hapo kwenye Pp yako unaonekana kabisa umevaa shati na kofia na fulana ulivyopewa bure na ccm!!! Hahahaaaaaaa!!what do we have to expect from you puppet?
 
Ankoo asiyeshaurika wala kufata mawazo ya wengi alikua na uzoefu na uraisi?
 
Chadema hawawezi kwenda Na kasi ya Mh. Rais wapumzishwe Kama hawataki kupumzika
 
Niaminini, siasa za Kakonko zina uelekeo huo. Eng Chiza ameshashinda kwa Matokeo ya tathmini ya awali
 
Siasa za upinzani ili uendelee nazo lazima ujifanye hamnazo - kumbukeni wakati wa kuaga marehemu Kasuku Bilago lisikika Mbowe akimwita Zitto na kumwambia kuwa uchaguzi mdogo lazima waungane:-
(i). Mbona leo ACT ana mgombea Ubunge (wasiwasi Kasigara)??

(ii) Lakini pia mbona Chadema wana mgombea ubunge jimbo hilo hilo (Mr Eliya)??

In short wapinzani hawa ni wepesi wa kudanganya majukwaani lkn si wepesi wa kutenda kadri ya sauti zao
 
Yaan unazi ndo umefanya uongee hvyo vitu na bila kupima uzito wa jambo unasema chiza atashinda. Je kutakuwa na uamuzi kupitia ballot box au ubabe as kinondoni utatumika? Free and fair election ccm haishindi popote zaid ya Dodoma.
 
Yaan unazi ndo umefanya uongee hvyo vitu na bila kupima uzito wa jambo unasema chiza atashinda. Je kutakuwa na uamuzi kupitia ballot box au ubabe as kinondoni utatumika? Free and fair election ccm haishindi popote zaid ya Dodoma.

Tatizo kuu kwako ni generalization - jmn fanya tathmini mwenyewe kisha tuambie mtaji wa CHADEMA kwa sasa ni upi kisiasa?? Ufisadi JPM kapiga kufuli, rushwa JPM anapigana, miradi mikubwa JPM, madege JPM, barabara JPM
 
Back
Top Bottom