CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Msajili simamia sheria bila uoga
Nimeipitia sheria mpya ya usajili vyama vya siasa. Sheria hii inampa msajili mamlaka ya kusimamia chaguzi ndani ya vyama ili kuhakikisha haki imetendeka, taratibu za kupata viongozi zimefuatwa na demokrasia imezingatiwa katika kupata viongozi.
Kwa utaratibu huu wa kuchukuliana form na kuteua anayefaa kugombea nafasi fulani ni vyema msajili aufahamishe umma kama ni sahihi? Asipofanya hivyo mwakani tutaona mambo ya ajabu mno.
Ikithibitika ni kinyume cha mahitaji ya Sheria basi Msajili asisite kutengua matokeo. Nahisi wahusika watadai msajili kawaingilia! Ukweli ni kuwa wanayataka. Hili likiachwa lizoeleke ni hatari mno. Hivi 2015 tungewapa chadema kushika dola si ingekuwa balaa? Rais angetangaza TBC tumemshauri "fulani" agombee ubunge Hai na "fulani" agombee ubunge Rombo. Ewe Mungu tunakushukuru hatukufanya makosa 2015, tungejuta.
Nina hakika ingekuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye kachukuliwa form au ndiye katangaza fulani achukue form kuomba umakamu hawa hawa CHADEMA wangeenda hadi BBC na EU kulalamika.
Namshauri Msajili asimamie matakwa ya sheria bila kuona huruma wala soni. Haiwezekani tuwe na chama kinachodai ni cha kidemokrasia lakini uongozi unapatikana kidikteta.