Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ana ushahidi?

PAMBANA

Member
Oct 21, 2010
73
21
Katika gazeti la Mwananchi la leo juu ya habari inayohusu vurugu iliyotokea jana kwenye public hearing ya mswada wa sheria ya marejeo ya katiba kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Bw.Tendwa anasema kuwa kuna vijana waliandaliwa kufanya vurugu zilizofanyika.

Je, Tendwa ana ushahidi wa hiyo kauli yake? Au naye ni mmoja wa wanapropagangda wa CCM?

Ndugu wana JF tunaomba mtu huyu afuatiliwe ili atoe maelezo ya kina kuhusiana na hiyo kauli yake,tunaomba waandishi wa habari wamfuate ili wananchi wapate kujua ni waliwaandaa hao vijana ili wafanye fujo ikiwezekana hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao maana siamini mtu mwenye upeo mkubwa kama John Tendwa anaweza kutoa kauli kama hiyo kuwa na ushahidi.

Source: Mwananchi 08/04/2011

"TANZANIA NAKUPENDA, TANZANIA NCHI YANGU, NITAKUTUMIKIA KWA MOYO WOTE NA
SITAKUSALITI KAMWE.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA"
 
Vijana wamechoka na CCM, hata jana Dodoma mkuu wa Mkoa anadai wanafunzi wa Udom wameletwa na Lema.. Ni Ujinga, vijana wanaenda wenyewe na wamechoka na longo longo za CCM. Hata wananchi wa Tegete nao watawaita ni wa Chadema!!
 
CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEE!!!!! Endeleeni kuwajaza ujaisiri watu kusimamia, kulinda na kudai haki zao. Hata ikibidi kumwaga damu kama ilivyotokea Tegeta na Dodoma kwenye Muswada feki
 
Vijana wamechoka na CCM, hata jana Dodoma mkuu wa Mkoa anadai wanafunzi wa Udom wameletwa na Lema.. Ni Ujinga, vijana wanaenda wenyewe na wamechoka na longo longo za CCM. Hata wananchi wa Tegete nao watawaita ni wa Chadema!!

Good enough Lema admited it tena kwenye habari hiyo hiyo! Usiusemee moyo hasa hasa kama siyo mfuatiliaji mzuri wa habari...
 
Tulijitokeza kama wananchi wa dom ambao tulialikwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mdahalo wa kukusanya maoni...mambo yakusema wanfunz wamefanya fujo hizo ni propaganda tu..kuliku na na raia wa kawaida wanafunzi wa mipango,udom,st johns ambo wote kwa ujumla wao ni WANANCHI WA JAMHURI HURU YA TANZANIA WAISHIO DODOMA.
 
Jamani mpaka sasa hamjagundua tu kuwa viongozi wote hawakubaliana na suala zima la katiba mpya ila wanalazimika kufanya hivi kwa kuwa tu kuna ushawishi mkubwa toka kwa upinzani?Kwangu mimi namuona Tendwa ni mtu ambaye anapalilia shamba lake ili liendelee kuonekana zuri kwa bwana wake,ulitegemea mtu kama Tendwa aseme nini mbadala wa alichosema ambacho kingemfurahisha aliyemuweka pale?
Ukweli uanabaki pale pale kuwa viongozi wetu bado hawajajiandaa na kile ambacho wanadhani ni mabadiliko ya katiba mpya wakati huo wananchi tayari wamekwishajitambua na wanajua nini wanataka katika kujiletea maendeleo.Tngu lini maoni yakatafutiwa mamluki?Inashangaza sana!
 
Good enough Lema admited it tena kwenye habari hiyo hiyo! Usiusemee moyo hasa hasa kama siyo mfuatiliaji mzuri wa habari...

Wewe bepari ndo siyo mfuatiliaji mzuri wa habari, Lema haja admit kuwahamasisha raia kufanya vurugu, bt kwenda kuchangia mawazo yao na si kuishia kulalamika mitaani..na ni haki yao ya kikatiba kutoa mawazo yao.
 
kama kweli viongozi wa siasa wanataka amani waache kulazimisha mambo. wananchi wapewe haki yao kujadili katiba bila ya kubagua eti kuna waelewa na wasioelewa kwa maslahi ya wanasiasa. tanzania ya leo sio ya miaka hiyo ya 70 na 80 siasa za chama kimoja hazina nafasi kabisa kama kuna chama kinategemea katiba iliyopo ikilinde sijui watatawala nchi ipi??/
 
Vijana wamechoka na CCM, hata jana Dodoma mkuu wa Mkoa anadai wanafunzi wa Udom wameletwa na Lema.. Ni Ujinga, vijana wanaenda wenyewe na wamechoka na longo longo za CCM. Hata wananchi wa Tegete nao watawaita ni wa Chadema!!

Well, Lema alikiri kuwashawishi wanachuo kuhudhuri mdahalo kwa sababu ni haki yao, lakini ni kweli kuwa walikuja wenyewe!
 
Ushahidi wa nini wakati anafanya kazi ya Tambwe Hiza?huyu ni mashine nyingine ya propaganda ya CCM kwani aliwahi kusema kuwa ataifuta CHADEMA kwa uchochezi na matusi na alipotakiwa kueleza matusi gani na uchochezi gani mpaka leo hajajibu ile barua kakaa kimya , hapaswi kusiki8lizwa tena na ndio maana tunasema rais asiwe wa kuteua kila mtu .
 
Ina maana Intellejensia wako likizo? Mbona hawakugundua kutakuwa na watu watafanya fujo kama walivyofanya Arusha
 
Je kwenye ajali zinazoua watanzania huyo tendwa hajui anayehusika? Mbona kimbelembele sana kama I-n-zi Tendwa
 
Mie nilikwisha toa pendekezo ili kuleta nidhamu kwa viongozi wazandiki kama Tendwa wanapokuwa wanaleta comment zao za kinafiki wangekuwa wanafikishwa mahakamani kutoa ushahidi na kulinda amani ya nchi.

Wanazidi kujiaibisha na miswada mibovu watabana mwisho wa siku wataachia.
 
Tendwa ni kati ya vibaraka wakubwa wa CCM....watu wanapokuwa na ufahamu na haki zao wao wana-define kuwa ni nguvu ya CDM.mbona watapata shida sana hii miaka mitano...nadhani wataishia njiani.....
 
Back
Top Bottom