Uchaguzi 2020 Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungi awatahadharisha Wagombea

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wakati kampeni za uchaguzi mkuu zikizidi kushika kasi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mstaafu Francis Mutungi amewataka wadau wote wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa kuepuka misuguano na Serikali.

Jaji Mutungi ametoa rai hiyo leo katika kikaao cha pamoja na wadau wote wa siasa kilichofanyika Jijini Dar es Salaam akieleza kuwa yeye kama mlezi wa vyama hafurahishwi na baadhi ya kauli za vyama vya siasa kupitia wagombea wao ambazo ni dhahiri zinaenda kinyume na kanuni za maadili ya uchaguzi walizosainishwa na tume ya uchaguzi.

Amesema katika siku hizi chache za kampeni zilizosalia ni muhimu mno kuepuka migongano akishauri wadau kuwa kwa mwenye malalamiko yeyote kuhusu uchaguzi ni vyema akafika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ndiyo inaratibu masuala yote ya uchaguzi.

"Sisi hapa tukianzisha vurugu tunauwezo wa kupanda ndege habari gani kuhusu wengine ambao hawana hili wala lile Vipi kuhusu watoto na makundi mengine", amesema Jaji Mutungi.

Aidha, amesema ofisi ya msajili imekuwa ikitoa maonyo kwa baadhi ya vyama ambavyo vimekuwa vikikiuka taratibu za usajili, huku akitoa wito kwa wafuasi wa vyama kulinda amani kwa kuwa yapo maisha baada ya uchaguzi.
 
UPUUZI MTUPU! Mbona wanahangaika sana hawa wakati wao ndiyo wanaofanya uonevu kwa Lissu na Chadema wa wazi kabisa!? Wasidhani Watanzania ni wapumbavu.
Unaandika kwa hasira kali. Dawa hamasisha wafuasi kwenda ofisi za Tume kukinukisha. Bila kufanya hivyo unsjiumiza bure, mwisho wake inakula kwako.
 
Hivi wao hawaoni Magufuli kuvunja sheria za uchaguzi kila mkutano halafu hawatoi onyo , wanahangaika na Lissu.

Sisi hatutaondoka Tanzania tutafia hapa hapa wao wenye uwezo ndo watakimbilia nje kama wakimbizi kwa madudu wanayofanya na asitutishe kabisa sisi wananchi hakuna mwenye uwezo wa kukimbia nchi tutafia hapa hapa wao ndo wana wakati mgumu.
 
UPUUZI MTUPU! Mbona wanahangaika sana hawa wakati wao ndiyo wanaofanya uonevu kwa Lissu na Chadema wa wazi kabisa!? Wasidhani Watanzania ni wapumbavu.
hakuna tena electoral justice kwasasa...mkuu mimi naona kitu chakwanza ni ku boot out kwanza tume kwa mass demostrations kali ili to reboot electoral process ianze upyaa tena ...what do you think mkuu??
 
Haki ni tunda la wajibu
Ukitaka haki nawe fuata taratibu 'tii mamlaka na sheria'
Wajibu ni zao la pande zote mbili! Mamlaka inayo pokea utiifu halisi ni ile inayo heshimu jukumu lake la kutenda haki, otherwise Gadaffi mnaye mtoleaga mifano anawaita!
 
Watapanda ndege kwenda wapi,? Waache vitisho nchi hii hakuna aliye juu ya sheria wamwambie Mwenyekiti wa ccm anavunja sheria za uchaguzi waziwazi" eti msiponichagua sileti maji" NEC wapo kimya msajili wa vyama yupo kimya, ila siku si nyingi wenye mamlaka yao (wananchi) wataongea.
 
Back
Top Bottom