Msajili wa Vyama Vya Siasa Francis Mutungi awataka wana Arusha kuacha ushabiki wa kiasi unaohatarish

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
988
Francis%20Mtungu.jpg


Msajili wa vyama vya siasa nchini Bw Fransis Mutungi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuepuka kuingiza ushabiki kwenye siasa kwani kufanya hivyo licha ya kuwa chanzo cha kuhatarisha amani wanaharibu lengo la fani hiyo ambayo ina umuhimu na faida kubwa katika jamii kama taratibu na misingi yake ikifuatwa na kuheshimiwa.

Akizungumza na wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Arusha waliokusanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid kuuombea mkoa wa Arusha amani Bw Mutungi amesema amani ndio msingi wa kila kitu na haihusiani kabisa na siasa hivyo hakuna sababu ya watanzania kukubali amani iliyopo ivurugwe na watu wachache wanaosingizia siasa kwani wanaopenda amani ni wengi kuliko wanasiasa

Wakizungumza katika hafla hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo shekh mkuu wa mkoa shabani bin jumaa na askofu mkuu wa kanisa la evengelisim centre eliud wamewaomba viongozi wa kisiasa na wanaotarajia kutafuta nafasi za uongozi kuwajengea wananchi utamaduni wa kuheshimi sheria na dola iliyoko madarakani kwani wakizoea kuvunja sheria watafanya hivyo hata uongozi ulioko madarakani ukibadilika .

Mkuu wa mkoa wa arusha Bw Magesa Mulongo amesema upo uwezekano wa kuendesha siasa, kudai haki na hata kukosoa na kutoa mapendekezo bila kuvuruga amani.

Wananchi hao wakiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa ,viongozi wa dini na wa mila walikusanyika katika uwanja huo kuhubiri na kuuombea mkoa wa arusha amani unaoandamwa na heka heka za kisiasa ambazo zimesababisha kuyumba kwa uchumi

chanzo: itv
 
Pichaza waliohudhuria uwanjani wakati mulongo akihutubia NA sio za redio safina tafadhali
 
Magesa mulongo naye pia anaombea amani. This is a joke kwani yeye ndiye ambaye amekuwa akituma askari uusiku wa manane kuvuja milango ya watu wakiwa wamelala. Amekuwa kinara wa ku abuse power kwa kulitumia jeshi la polisi/ffu kutunishia misuli. Thanks to the new constitution we are about to get rid of them soon.
 
ITV Wahuni hao, futa haraka Uzi huu...

Usilete malalamiko ya Ukabila ka wanaCCM wanavyolialia ka watoto.... kiiilakitu "ukabilaaaaaaa....!"

ITV imeajiri watu na siyo "wahuni" sifa ya uhuni wao inatokana na nini?
 
Hayo maneno angeyasema wakati dr. Slaa akiwa ziarani kigoma angeeleweka vizuri, lakini anayasema mahali ambapo ccm ina/imekataliwa kinomanoma ni ishara ya kuibeba ccm isiaibike angalau kwenye vimikutano vyake ARACHUGA ingawa matokeo ya kura iwe usiku iwe mchana, inyeshe mvua liwake jua kwa arusha wanayajua.

peoples power will triumph
 
Polisi na matumizi yao ya nguvu zilizozidi badala ya busara ndo chanzo cha uvunjifu wa amani na wala sio siasa! Kama Polisi watatoa haki kwa watu wote na vyama vyote bila upendeleo, siasa haiwezi kusababisha vurugu! Ilifika mahali ambapo wakikusanyika Chadema hata wakiwa na kibali cha mkusanyiko lazima mabomu ya machozi yatembee! Na wenyewe ni wanadamu lazima wajitetee, tayari vurugu. Ila kwa ziara ya Dr. Slaa, naona Polisi wanaanza kuelewa somo. Kazi yao ni kulinda raia wote na mali zao bila kujali itikadi!
 
Back
Top Bottom