Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 988
Msajili wa vyama vya siasa nchini Bw Fransis Mutungi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuepuka kuingiza ushabiki kwenye siasa kwani kufanya hivyo licha ya kuwa chanzo cha kuhatarisha amani wanaharibu lengo la fani hiyo ambayo ina umuhimu na faida kubwa katika jamii kama taratibu na misingi yake ikifuatwa na kuheshimiwa.
Akizungumza na wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Arusha waliokusanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid kuuombea mkoa wa Arusha amani Bw Mutungi amesema amani ndio msingi wa kila kitu na haihusiani kabisa na siasa hivyo hakuna sababu ya watanzania kukubali amani iliyopo ivurugwe na watu wachache wanaosingizia siasa kwani wanaopenda amani ni wengi kuliko wanasiasa
Wakizungumza katika hafla hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo shekh mkuu wa mkoa shabani bin jumaa na askofu mkuu wa kanisa la evengelisim centre eliud wamewaomba viongozi wa kisiasa na wanaotarajia kutafuta nafasi za uongozi kuwajengea wananchi utamaduni wa kuheshimi sheria na dola iliyoko madarakani kwani wakizoea kuvunja sheria watafanya hivyo hata uongozi ulioko madarakani ukibadilika .
Mkuu wa mkoa wa arusha Bw Magesa Mulongo amesema upo uwezekano wa kuendesha siasa, kudai haki na hata kukosoa na kutoa mapendekezo bila kuvuruga amani.
Wananchi hao wakiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa ,viongozi wa dini na wa mila walikusanyika katika uwanja huo kuhubiri na kuuombea mkoa wa arusha amani unaoandamwa na heka heka za kisiasa ambazo zimesababisha kuyumba kwa uchumi
chanzo: itv