Msajili wa vyama vya siasa awajibu BAVICHA

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,279
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amejibu tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) waliodai kuwa watamfungulia mashtaka endapo hatachukua hatua dhidi ya CCM ikiwa ni pamoja na kukifuta chama hicho kwa kuonesha ujumbe wa chuki na ubaguzi katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema kuwa hawezi kuwazuia Bavicha kumpeleka mahakamani kwani hiyo ni haki yao. Lakini akawashauri kuwa kabla hawajazungumza walichozungumza ni vyema kwanza wangemuuliza na kuwa na uhakika kwani tayari ameshachukua hatua za kisheria dhidi ya CCM.

“Wanatakiwa kuwa na uhakika kwanza,” alisema Jaji Mutungi. “Mimi nimeshawachukulia hatua CCM, tena hatua kwa mujibu wa sheria. Nimewaandikia barua nikiwataka wajieleze kuhusu ujumbe huo ulioonekana,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Jaji Mutungi alisema kuwa tayari ofisi yake imeshaingilia mgogoro wa uchaguzi unaoendelea visiwani Zanzibar kwa kuwa unawahusu wadau ambao ni vyama vya siasa. Alisema amezungumza na pande mbili zinazozana ili kusaidia katika kupata maridhiano ya amani.
 

Attachments

  • Mutungi2.jpg
    Mutungi2.jpg
    59.5 KB · Views: 65
hizi ni porojo ingekua ni chadema angeshakimbilia kwenye tv na magazeti kutangaza adhabu! anaposema amewachukulia hatua ni zipi izo? mbona kimya kimya?
 
kitengo kimoja cha chama kiwajibishe kiingine ccm hii au. Mmesahau hapa kazi tu aliomba kura kwa wasukuma kwa kisukuma mwanzo mwisho, msajili hakiwezi?
 
Porojo za kitoto hizo CCM ni kinara wa ubaguzi wa wazi wazi hatujawahi kuona wala kisikia hatua zozote zikichukuliwa zidi ya hicho chama cha kibaguzi
 
Tawi la CCM linataka kuchukua hatua against HQ yake.Hata yule Balozi Karume pia hajampa onyo maana alisema anataka sheria itakayozuia vyama vya upinzani kugombea nafasi ya URAIS anataka CCM tu ndiyo chama cha kuchukua form za kugombe nafasi hiyo.

Nimeamini ukilewa sana madaraka unaropoka chochote bila kufikiria impact yake kwa jamii
 
Huyu ni jipu liloiva .anazungumzia kwamba ameshachukua hatua .lakini ni baada ya bavicha kuhoja .kama bavicha wasingehoja ingekua ndio imetoka .mbona gakuweka hadharani jambo hili.hakuna kitu chochote kutakachobadilika
 
hizi ni porojo ingekua ni chadema angeshakimbilia kwenye tv na magazeti kutangaza adhabu! anaposema amewachukulia hatua ni zipi izo? mbona kimya kimya?


Mkuu hawa wamezoea kuwadanganya Watanzania. Huyo Mutungi angeonesha basi huo ushahidi wa maandishi ya kuwanonya CCM tukauona!
 
Back
Top Bottom