Msajili wa Vyama vya Siasa awaandikia barau nyingine CHADEMA, ataka wajieleze

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Aiandikia Chadema barua nyingine na kuwataka wajieleze Kwa Maneno aliyoyasema Kiongozi wa Baraza la Wazee na ametumia Maneno ya mtaani yenye kumaanisha hukumu tayari imeshatolewa. Manano kama "mwana kulitafuta, mwana kulipata " na "mtoto asipolelewa na wazi atalelewa na Ulimwengu"

Aidha Msajili amenukuu kifungu cha 9(2)(f) cha sheria ya vyama vya siasa ambacho kipo mahususi Kwa ajili ya vyama ambavyo vina usajili wa Muda na havijapata usajili wa kudumu ndio anataka kuitumia kuihukumu Chadema ambayo ina usajili wa kudumu.

Msajili anatafuta njia ya kuifutia Chadema usajili , atakuwa anafanya haya Kwa maslahi ya Nani au ndio Ile Gang unataka kuitumbukizanchi kwenye machafuko?

Nimeambatanisha barua husika kutoka ofisi ya msajili wa Vyama!
 
Attachments

  • Kwenda Chadema0001.pdf
    2 MB · Views: 42
Barua inasema "CHADEMA kuchukuliwa hatua kwa mjibu wa sheria".

Maana ya maneno hayo ni nini?

Msajiri kuifuta sheria kwa kutumia vifungu hivyo vya sheria bila kufikishwa mahakamani? Yeye ndiye mahakama? Au kuna utaratibu wa kwenda mahakamani na CHADEMA kupata nafasi yake ya kujitetea mbele ya mahakama?

Haya yote tunayoyashuhudia sasa ni sehemu ya ukombozi wa nchi yetu, ni mchakato unaoendelea hadi tutakapo ondokana na ukoloni wa CCM.
 
Hizi ni project za waganga njaa waliopewa vitengo, zinatengenezwa ili wawe bize kuziandikia madokezo ya kuomba pesa kwa kigezo cha mapambano na chadema.

Ndio walivyosomea huko vyuo vikuu....watu wazima inasikitisha....ndio wasomi serikalini wajanja janja wa kuandika madokezo...njia mpya ya upigaji....kuanzisha vikesi kesi....project za kukamatakamata. Allah Waangalie hawa
 
Mbona hakuiandikia barua CCM wakati ule wa kampeni za urais ambapo Samia alisema "hata ukipigia kule kwingine ccm itaunda serikali?"
Huyo Msajili wa vyama vya siasa, moja kwa moja, amethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa ame-side upande wa CCM.

Yeye anatambulika kama mlezi wa vyama vya siasa, sasa ni kwanini atoe kauli ya vitisho vya aina hiyo kwa chama cha siasa cha Chadema pekee??

Mbona hatujamuona atoe kauli kama hizo kwa CCM, pamoja na "madudu" yake mengi inayoyafanya??

Aifute Chadema, kama anao huo ubavu!
Full Stop
 
Aiandikia Chadema barua nyingine na kuwataka wajieleze Kwa Maneno aliyoyasema Kiongozi wa Baraza la Wazee na ametumia Maneno ya mtaani yenye kumaanisha hukumu tayari imeshatolewa. Manano kama "mwana kulitafuta, mwana kulipata " na "mtoto asipolelewa na wazi atalelewa na Ulimwengu"

Aidha Msajili amenukuu kifungu cha 9(2)(f) cha sheria ya vyama vya siasa ambacho kipo mahususi Kwa ajili ya vyama ambavyo vina usajili wa Muda na havijapata usajili wa kudumu ndio anataka kuitumia kuihukumu Chadema ambayo ina usajili wa kudumu.

Msajili anatafuta njia ya kuifutia Chadema usajili , atakuwa anafanya haya Kwa maslahi ya Nani au ndio Ile Gang unataka kuitumbukizanchi kwenye machafuko ?

Nimeambatanisha barua husika kutoka ofisi ya msajili wa Vyama !

IMG_20211004_150742_609.jpg
 
Kifutwe tu hicho chama cha wahuni wakilala wanawaza uhuni wakiamka wanawaza Fujo sasa chama kilikuwa kinageuzwa cha kigaidi

Tanzania bila ugaidi inawezekana
 
Back
Top Bottom