Lengo la msajili wa vyama vya siasa ni kusajili na kuvilea vyama vyote kwenye misingi ya sheria bila kuleta ubaguzi wa aina yeyote.
Msajili wa vyama anatakiwa atambue kuwa chama cha upinzani kipo kisheria 'is a government in waiting', atambue pia vyama ni watu wenye mawazo tofauti, kwahiyo haiwezekani wote wakawa chama kimoja. Inapotokea mlezi anakwenda kinyume na malengo ni dhahiri watu hawatakubali na matokeo yake ni kusababisha uvunjifu wa amani.
Hadi sasa Msajili ameonyesha wazi na dalili ziko wazi kuwa hayuko kwa ajili ya kuvilea vyama bali kuua vyama hasa vinavyoonekana kutokubaliana na matakwa ya watawala. Angekuwa mlezi asingekubali sheria mpya ya vyama vya siasa inayokwenda kunyonga uhuru na haki ya vyama. Ameiua CUF sasa anataka kuiua ACT Wazalendo bila kuwa na sababu za msingi.
Msajili asijidanganye hakuna chama kikubwa chenye usajili wa kudumu kitakachokubali kufutiwa usajili kwa utashi wa mtu mmoja pasipo kosa kuthibitishwa na mahakama. Mfano msajili atajilidhisha vipi watu wanaochoma bendera ni wafuasi wa chama fulani kama hana chombo cha kufanya upelelezi.
Tuendako ni giza, inabidi zitumike nguvu za ziada kumzuia as soon as possible, vyama vya siasa vikiendelea kumchekea vitaumizwa viungane kukemea, wanaharakati wakemee, wazee na viongozi wa dini wakemee, jumuiya za kimataifa zijulishwe, na wananchi wote wazalendo wanaoitakia mema nchi hii wamkemee msajili mapema kabla hajaliletea taifa vita ya wenyewe kwa wenyewe kutokana na ubaguzi anaouonyesha waziwazi.