Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Nimesoma kwenye vyombo vya habari, Mwenyekiti wa vyama vya siasa nchini, akiwaandikia barua Chadema na kuwapa muda hadi tarehe 7/10/2019 wajieleze ni kwanini asiwachukulie hatua kutokana na kukiuka kufanya uchaguzi wa chama chao??
Ameendelea kuelezea msajili huyo wa vyama kuwa muda wa kukaa madarakani kwa Mbowe umekwisha, kwa madai yake kuwa chama hiko kilifanya uchaguzi wake tarehe 14/9/2014 na hivyo kufanya chama hiko kikose uongozi halali ilipofika tarehe 15/9/2019
Nimekuwa nikijiuliza hivi huyu msajili wa vyama anaendelea kuisakama Chadema kwa misingi ipi??
Kama ni wenyeviti wa vyama waliokaa muda mrefu kwa kuzibunja Katiba ya vyama vyao, basi ni UDP, ambayo Mwenyekiti wake John Cheyo, ameendelea kukikalia kiti hicho na kukifanya kuwa cha maisha, kwani aliteuliwa kuwa Mweyekiti, tokea mwaka 1994
Vile vile bila kusahau chama cha TLP, ambacho pia Mwenyekiti wake, Augustine Mrema, amekishikkilia cheo hicho na kukifanya kama Mali yake binafsi!
Hivi msajili wa vyama unaweza kweli kuiandikia barua ya vitisho Chadema kwa kutochagua Mwenyekiti wake, wakati ukijua kuwa chama hicho nimekuwa kikipokezana vijiti vya Mwenyekiti, kwani tokea kianzishwe, nafasi hiyo imekakiwa kwa zamu na wenyeviti watatu, ambao ni Edwin Mtei, Bob Makani na hivi sasa, Freeman Mbowe
Hivi chama cha Chadema kitakuwa na tofauti gani na CCM, ambayo nayo imekuwa na wenyeviti watatu, tokea miaka hiyo ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi, ambao ni Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na hivi sasa John Pombe Magufuli??
Hivi hii serikali mmeona haijatosha, kwa "kuwabambikia" kesi ya uchuchezi, viongozi wakuu wa chama cha Chadema na hivi sasa mnataka mtimize azma yenu ya kutaka kukifuta kabisa??
Huu ubabe wenu mnaoutembeza kwa chama kikuu cha upinzani nchini, cha Chadema, hakika msione kuwa wananchi hawaoni, Bali ni uvumilivu wao pekee ndiyo unaoifanya nchi hii iendelee kuwa na amani.
Siku uvumilivu huo utakapofika kikomo, hakika "damu" itamwagika nchi hii