Msajili wa vyama Jaji Mutungi amwambia Spika kuwa hawezi kuingilia mambo ya CHADEMA kwa kuwafukuza uanachama wabunge

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amesema hawezi kuingilia suala la wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufukuzwa uanachama wa chama hicho hadi pale atakapopelekewa malalamiko.

Akizungumza kwa simu na Nipashe, Jaji Mutungi amesema kila taasisi ina taratibu zake na hivyo yeye kama msajili hawezi kuingilia hadi pale atakapoletewa malalamiko na kuona kuwa kuna uvunjifu wa sheria za nchi katika suala husika.

“Sasa si muwaache wafanye kazi yao ,ndio huwa mnasema msajili akiingilia mnasema anawaingilia, wahusika hawajaja kwetu kulalamika kwa hio wao wanaheshimu taratibu za chama chao ,wakija kwetu kulalamika sisi ndio tutaingilia hilo suala” amesema Jaji Mutungi.

Jana Spika wa Bunge, Job Ndugai alimuomba msajili wa vyama vya siasa kukiangalia chama hicho kikuu cha upinzani na namna kinavyoendeshwa kwa madai kuwa kinafanya maamuzi ya kibabe dhidi ya wabunge wake.

Wabunge waliofukuzwa ubunge katika chama hicho kwa kile kilichodaiwa ni utovu wa nidhamu ni Mbunge wa Momba, David Silinde, Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

Aidha wapo waliotakiwa kujieleza ambao ni Wabunge wa Viti Maalum, Suzan Masele, Joyce Sokombi ,Rose Kamili, Latifa Chande, Lucy Mlowe, Sware Semesi ,Sabrina Sungura na Anne Gideria.

Wengine ni Mbunge wa Moshi mjini, Jaffary Michael, Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali na Mbunge wa Karatu William Kambalo.

Soma: "Siwezi kuingilia suala la wabunge wa Chadema kufukuzwa"-Jaji Mutungi
 
Mabaya haya yote yanayofanywa na viongozi wa chama tawala yataandikwa kwenye historia. Historia haijawahi kudanganya naendelea kukisoma kitabu kipya kuhusu Mwl. Nyerere najiuliza pamoja na uadilifu wake wote bado kuna maswali. Huyo ni Mwl. ambaye ni kielelezo cha uadilifu.

Tusibiri vitabu vitano vitaandikiwa tutavilinganisha na vitatusaidia kupata muelekeo chanya baada ya kujisahihisha tulipotoka na kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
 
Back
Top Bottom