Msajili wa Vyama angesubiri tu CHADEMA na ACT-Wazalendo viungane ili avifutilie mbali badala ya kulalamika lalamika kila siku!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,754
141,616
Huu sasa umekuwa kama mwimbo kila siku msajili wa vyama vya siasa analalamika Chadema na ACT wazalendo kutaka kuungana kinyume cha sheria.

Kwanini Dkt. Nyahoza asisubiri tu hivyo vyama viungane kisha avifutilie mbali.

Ni simple tu badala ya kuwa anatuimbia daily tunachoka bhana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wa kung'ata ni wa kung'ata. Hauwezi kuwa wa kubweka halafu ukawa wa kun'gata. Huyo atabweka tu hadi mwisho. Kuna precedent ya vyama kusapoti vyama vingine tayari. It does not make sense vyama vingine kuruhusiwa kusapotiana na vingine vikatazwe. Tuache mapenzi ya kijinga. Tushindane kwa mambo ya msingi.
Dr Nyahuza ng'ata!
 
Huu sasa umekuwa kama mwimbo kila siku msajili wa vyama vya siasa analalamika Chadema na ACT wazalendo kutaka kuungana kinyume cha sheria.

Kwanini Dkt. Nyahoza asisubiri tu hivyo vyama viungane kisha avifutilie mbali.

Ni simple tu badala ya kuwa anatuimbia daily tunachoka bhana.

Maendeleo hayana vyama!
Those ar last kicks of dying horse.
FB_IMG_1601425432271.jpg
 
CCM katika uchaguzi wa mwaka huu, kama kuna kitu kinawatia hofu kubwa, basi si kingine zaidi ya "synergy" ambayo itavihusha vyama vya CDM na ACT Wazalendo kwa namna iwayo yoyote ile. Najua wanalisikilizia na kulifuatilia kwa umakini tamko la Zitto kuwa ACT. Wazalendo watatoa msimamo wao kamili siku ya tarehe 03-10-2020.

Natumbua vyama hivi viwili vimejaa watu wengi walio wabobezi wa mambo ya sheria. Natambua kuna "loopholes" zipo ambazo zinaweza kutumika kutokana na "legal technicalities" hatimaye "synergy" hiyo ipate kupatikana.

Issue kubwa hapa ni jinsi ya CCM ya kuweza kuwathibiti kwa pamoja, Maalim Seif kule Zanzibar, na Tundu Lissu kwa huku Tanganyika. Hapo ndipo unaona ni kwa CCM inatumia matawi yake muhimu ili kutaka kuthibiti moto wa upinzani unaowaka kwa kasi sana. Matawi haya, yaani viongozi wasiokuwa na maadili ya kazi wa Jeshi la Polisi, msajili wa vyama na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi wameanza kupiga jalamba ili kuleta uchafuzi.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya KUUNGANA (COALITION) na kuungana mkono (support). Wew TAGA hunaweza kuungana na mama mkwe wako ili mzae? Unaweza kumsapot tu. COALITION inahusisha ku merge mpk SERA, hawa hawatojadili wala kufumua sera za ilani zao. Wanaunga mkono sera na manifesto ya chadema. Ni tamko tu sio makubaliano.
 
Sheria inasemaje?
 
Huu sasa umekuwa kama mwimbo kila siku msajili wa vyama vya siasa analalamika Chadema na ACT wazalendo kutaka kuungana kinyume cha sheria.

Kwanini Dkt. Nyahoza asisubiri tu hivyo vyama viungane kisha avifutilie mbali.

Ni simple tu badala ya kuwa anatuimbia daily tunachoka bhana.

Maendeleo hayana vyama!
Hana ubavu huo, mtu mwenyewe wa kukimbizana na bodaboda!
 
Kwani sheria inazuia kutamka kuwa unamuunga mkono mpinzani wako!
Mbona jana Magufuli alimuomba Sugu ampigie kura na kumsugua, kwa nini Nyahozya asimkaripie?
Haha Dah aisee Magufuli anawapa wakati mgumu sana hawa jamaa
 
Back
Top Bottom