Msajili wa vyama ameipandisha chati Chadema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msajili wa vyama ameipandisha chati Chadema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 6, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu, hatua ya Msajili wa vyama kukataa kukisajili Chama Cha Jamii ((CCJ) imekuwa ni baraka kwa Chadema bila kila pande kujijua. Iwapo CCJ ingesajiliwa, moto wa Chadema usingepamba kiasi hiki tunachoona -- hasa baada ya Dr Slaa kuteuliwa nafasi ya kugombea nafasi ya urais.

  Ninavyoona, hatua ya msajili ilisukumwa na utawala wa CCM kwani sote twajua ilikuwa inahofia kwamba endapo CCJ ingepata usajili, ingechota vigogo kutoka CCM. Lakini utawala ilikuwa haijui kwamba hatua hiyo imeikweza sana Chadema. Wananchi wengi waliokuwa wanangojea kukiunga mkono CCJ sasa wamekwenda Chadema.

  Aidha nadiriki hata kusema kuwa vurugu kubwa na ufisadi katika mchakato wa CCM wa kuteua wagombea umekipotezesha chama hicho maelfu ya wafuasi baada ya kuamini kuwa bila rushwa CCM haiwezekani.

  Ile methali ya "Kuchamba kwingi....." ni sahihi hapa.
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ikawa kweli ila sidhani kama kuna mwanachama wa CCM angehamia CCJ kama alivyofanya Mpendazoe,inahitaji roho ngumu sana kufanya maamuzi kama alivyofanya Mpendazoe maana hawa jamaa hawachelewi kukwambia kuwa wewe si raia wa nchi hii na makosa kibao hasa ukizingatia vigogo wengi wa CCM wana madhambi mengi na yanafumbiwa macho kwa kuwa tu wapo CCM.
   
Loading...