Uchaguzi 2020 Msajili wa Vyama ameionya CHADEMA kwa kuongeza ubeti wa 3 katika Wimbo wa Taifa jana katika Mkutano wa Baraza Kuu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,454
3,418
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi ameionya CHADEMA kutokana na alichokiita uvunjifu wa sheria kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Ameeleza kuwa kitendo hicho kilifanywa jana wakati Baraza Kuu la CHADEMA lilipokuwa likimpendekeza atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais.

Msajili amesema, "Nimesikitishwa na kitendo cha kuvunja sheria kwa makusudi kilichofanywa na CHADEMA cha kuchukua wimbo wa Taifa na kuongea aya"

Amesisitiza, "Kwa hili ambalo limefanyika na CHADEMA ni kama kunajisi wimbo wa Taifa. Nataka kuwaonya wakati wanaendelea na mikutano yao, waheshimu sheria za nchi."
 
Jaji kuna mengi ya kuongea ili uweke mambo sawa ila cha ajabu anakuja na mambo ambayo sio kipau mbele kwa Taifa!
 
Du huu wimbo umetohelewa kwenye nyimbo za kwaya ,wengine huwa wanachanganya aya moja kwenye nyimbo zao...kumbe ni kosa! Kweli bata siku zote anaharisha ....!
 
Back
Top Bottom