Frey Cosseny
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 1,984
- 1,405
Muda sasa mrefu umepita ofisi ya msajili wa vyama haifanyi kazi zake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa na wao wamegeuka kufanya kazi kisiasa. Kwa muda mrefu vyama vya upinzani zimekuwa zikiminya demokrasia ndani ya vyama vyao huku baadhi wa wafuasi wa vyama ivyo wakilalamika lakini ofisi ya msajili imeziba sikio kwa pamba, kuna baadhi ya vyama tangu kuanzishwa kwao toka mwaka 1992 havijawai kufungua ofisi zanzibar na watendaji wa upande wa znz wanafanyakazi zao bara lakini ofisi hiyo imekaa kimya kuna baadhi ya vyama vimewai kutuhumiwa kuendesha mambo ya kihualifu na ht kupoteza maisha ya wafuasi wao na sasa pamezuka baadhi ya viongozi wa vyama kumtusi mh Rais kwa kisingizio wanatekeleza sheria ya vyama vya siasa lakini ofisi ya msajili imekaa kimya hivi ni sheria ipi ya vyama vya siasa inayoruhusu mh Rais kutukanwa na vyama vya siasa? Na mbona ofisi ya msajili imelalala bila kutolea maelezo? Muda umefika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuwajibika kwa mujibu wa sheria ofisi isipofanya kazi yake tutakuwa na vyama vya siasa vinavyoleta uchochezi na kufanya siasa za harakati zinazofanywa na NGOs na siyo vyama vya siasa. Vyama vya siasa vinapaswa kufanya siasa kwa kutangaza sera, itikadi na falsafa lkn siyo haya tunayoyaona. Msajili km kazi imekushinda tupishe apatikane mwingine bila kusimsmia msingi wa kuanzishwa kwa vyama vya siasa na kuachia siasa hizi za kipuuzi nchi hii iko hatarini kugawanyika na kupoteza amani iliyodumu kwa muda mrefu
Na: Frey Cosseny
Na: Frey Cosseny