Msajili wa vyama aburuzwa kortini ...................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Msajili wa vyama aburuzwa kortini Wednesday, 08 December 2010 20:14

Mussa Mkama
CHAMA cha Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi (TUPSE), kimemfikisha mahakamani msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, Dalia Owiso kwa madai ya kuingilia masuala ya utendaji wa chama hicho.

Kesi hiyo namba 83 ya mwaka huu, imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi ya Kanda ya Dar es Salaam.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tupse Abdalah Msagama, mhasibu wake Augostine Lupia na msajili wa vyama vya wafannyakazi.

Kesi hiyo ilitajwa tena jana mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama ya Kazi, Shalmila Sarwatt, na itatajwa tena Januari 11 mwakani.

Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa, wakili wa Tupse, Mohamed Tibanyendara, alisema sababu ya kumfikisha msajili wa vyama mahakamani ni kitendo chake cha kuingilia masuala ya ndani ya utendaji wa chama hicho, jambo alisema linapingana na katiba halali ya chama.

“Kitendo cha msajili kuingilia masuala ya utendaji wa chama ni ukiukwaji wa sheria na hali hiyo imewafanya wateja wangu kupoteza mwelekeo na mapato ya chama kufujwa kwa kuwa wanaoshikilia pesa si wahausika,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Tupse, Edison Kivelege alidai kuwa msajili wa vyama ameingilia uhuru wa wanachama, waliochagua viongozi kupitia mkutano mkuu wa wa chama.

“Katiba inasema viongozi watachaguliwa na mkutano mkuu wa chama, lakini cha kushangaza wanaodaiwa kutambuliwa na msajili wanadai walichaguliwa na kikao jambo lilnaloonyesha kuwa msajili ana ajenda ya siri," alisema Katibu mkuu huyo.
 
Back
Top Bottom