Msajili wa Siasa aibuka na Mapya Juu ya CUF

Rutaca

Member
Nov 13, 2014
94
236
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesisitiza msimamo wake kwamba Chama cha Wananchi (CUF) ni kimoja, hivyo yeyote mwenye malalamiko ayapeleke ofisini ili yashughulikiwe na si kulalamika kupitia vyombo vya habari.

Kauli hiyo imekuja baada ya mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro kueleza jinsi Profesa Ibrahim Lipumba alivyochukua fedha za ruzuku zaidi ya shilingi milioni 369 kutoka Hazina.

Mtatiro anamtaja msajili, Jaji Francis Mutungi kuwa anafahamu na kuidhinisha mchakato huo wakati Oktoba 10 mwaka jana, aliandika barua ya kusitisha utoaji wa ruzuku kwa chama hicho kutokana na mgogoro hadi hali itakapokuwa shwari kiutendaji.

Lakini mwishoni mwa juma, mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano katika ofisi hiyo ya Msajili, Monica Laurent alieleza kuwa kuna chama kimoja tu cha CUF.

“Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatambua CUF iko moja tu, Kama CUF kuna watu wana malalamiko ya msingi wayalete rasmi ofisini, huo ndiyo msimamo wetu,” alisema Laurent.

Aidha aliwataka kutumia mfumo rasmi wa kuwasilisha malalamiko hayo kwenye ofisi ya msajili, akibainisha kuwa ofisi hiyo haiwezi kujibu masuala hayo kwenye vyombo vya habari.

Hivi karibuni Mtatiro akizungumza na vyombo vya habari alieleza kuwa tangu Msajili aandike barua ya kusitisha ruzuku, chama kinadai Hazina sh. 635 Milioni, hivyo CUF haitambui utaratibu mwingine uliotumika kuigawa ruzuku hiyo hadi Lipumba akapata mgawo wake.

Alisema chama kimeibiwa fedha za ruzuku sh. 369 ambazo zilitoroshwa kutoka Hazina ya Serikali Kuu Januari 5 na kuingizwa kwenye akaunti ya NMB tawi la Temeke yenye jina la The Civic United Front, ikiwa ni akaunti namba 2072300456.
 
Mutungi, muogope MUNGU
 
Ndio maana naamini kwamba Magufuli ni fisadi na huwezi kunibadirisha Magufuli fisadi wa kisiasa kiuchumi kiutawala na kijamii anayoyafanya yanaweka usalama wa nchi mahali pa baya mno sijui huyu Kikwete alimtoa wapi huyu mtu ameletwa na amekuwa janga la ustawi wa Tanzania
 
Ajibu swali,"Kwa nini Pesa za Ruzuku za CUF amezitoa bila idhini ya Baraza la Wadhamini wa CUF ambao ndio wasimamizi wa Mali zote za Chama?"
Hii ni kwa Mujibu wa Kifungu cha 21(1) cha sheria ya vyama vya siasa.
Pesa za ruzuku Ni Mali za chama ?
 
Francis Mutungi anakaribia KUVUNJA REKODI YA DUNIA , ya kuwa msajili wa kwanza wa vyama vya siasa KUFUNGWA JELA , hawa wanaompotosha hawatamsaidia kitu .
 
Kwa kweli Msajili anatakiwa aeleze vizuri watanzania kuhusu matumizi ya Kodi zao.
Kitakachomchanganya zaidi ni kupeleka Pesa katika Akaunti ambayo haimilikiwi na Bodi ya wadhamini kama inavyopendekezwa na Sheria ya vyama vya Siasa kifungu 98(3).
 
Francis Mutungi anakaribia KUVUNJA REKODI YA DUNIA , ya kuwa msajili wa kwanza wa vyama vya siasa KUFUNGWA JELA , hawa wanaompotosha hawatamsaidia kitu .

Ni kweli anaeza fungwa kwa TZ hii? watafungwa wapinzani tu ndugu yangu......
Aliyoyafanya Jecha ni Zaidi ya huyu jamaa... Ila Jecha anakula bata bado. Natamani afungwe, Ila sioni kwa Tanzania ya sasa wala ya miaka 10 ijayo....
 
Pesa za ruzuku Ni Mali za chama ?

Naam,Kifungu cha 98(3),Cha sheria ya vyama vya siasa kinasema,
"Bodi ya Wadhamini itakuwa mdhamini pekee wa Fedha na Mali za chama pamoja na madeni na
itafanya shughuli zake kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizowekwa na Sheria ya nchi inayohusu Wadhamini."
 
Wapo kwa niaba ya kuiyumbisha CUF,kama yalitolewa maamuzi ya kusimamisha ruzuka na taharifa skate iweje aludishe luzuku bila taharifa na kuiweka kwenye account isiyo rasmi,harafu oooh serikari yangu inapinga ufisadi huku umeajiri mifisadi,moons we nine wakifanya makosa kidogo tu wana tumbuliwa kwa uyu wanasubili nini
 
Ni kweli anaeza fungwa kwa TZ hii? watafungwa wapinzani tu ndugu yangu......
Aliyoyafanya Jecha ni Zaidi ya huyu jamaa... Ila Jecha anakula bata bado. Natamani afungwe, Ila sioni kwa Tanzania ya sasa wala ya miaka 10 ijayo....
Mbele ya Mungu hakuna kinachoshindikana .
 
naona watu mnachangia kwa kuchukua upande wa kisiasa.. Mtungi ni mwanasheria mmbobezi. hawezi kufanya maamuzi ya kijinga kama haya bila kufuata kanuni. Hii suala la cuf lilikosewa na cuf wenyewe na kumwachia Lipumba loophole ya kuwavuruga.

kama kweli wanauhakika kwamba mtungi amefanya kosa kuwapatia ruzuku team lipumba, kwa nini akina mtatiro wanazungumza tu na vyombo vya habari badala ya kwenda mahakamani???
 
Back
Top Bottom