Leo nimeona kwenye tovuti msajili wa NGOs akitoa taarifa kwa NGOs zote nchini kufanyiwa uhakiki kuanzia tarehe 21 August 2017- 31 August 2017.Uhakiki huo utafanyika kwenye makao makuu kanda kwa maana ya kanda ya mashariki,kati,kaskazini, ziwa na nyanda za juu kusini.
Kwanza nipongeze nia ya selkari ya kufanya uhakiki wa mashirika yasiyo ya kiselkari ni jambo jema kwa mstakabari na maslahi mapana ya usalama wa nchi yetu.
Wasiwasi wangu nikuwa zoezi hili litawakwaza sana wadau wa sekta ya NGO ambao watalazimika kusafiri kutoka wilayani, mikoani kwenda ngazi ya kanda, ukizingatia suala zima la raslimali muda, fedha na muda uliopangwa kwa zoezi hilo utaona kuwa ni kikwazo kikubwa kwa NGOs ambazo hutegemea zaidi ya hisani ya michango ya wananchama na wabia wa maendeleo.
Zoezi hili lisiporatibiwa kwa umakini na ustadi, linaweza kutengeneza mazingira na mianya ya rushwa kutokana na idadi kubwa ya NGOs zitakazo jitokeza kwa ajili ya uhakiki ndani ya muda wa siku kumi. Watu wamekuwa wakitumia fursa ya speed ya utendaji wa Rais kwa kutengeneza mianya ya rushwa.
Nakumbuka idara ya uhamiaji waliwahi kutangaza nafasi za kazi 200 waka shortlist watu 10,000 kwa ajili ya interview. likuja gundulika baadae kuwa ilikuwa ni kutengeneza mazingira ya rushwa, naomba tusifike huko, tusimkwaze Rais wetu, badala yake tuunge mkono jitihada zake kwa dhati.
Rais Magufuri akiwa Tanga juzi ameweka bayana kuwa watendaji wa Selkari wasiwe chanzo cha kero kwa wananchi, alisema yeye yupo, mawaziri wapo, wakuu wa mikoa wapo , wakuu wa wilaya wapo ili kushughurikia kero kwa namna yeyote ile. Wiki haijapita baada ya tamko la Mhe. Rais, msajili wa NGOs anaibuka na tamko kuwa viongozi wa NGOs wasafiri umbali wote huo bila kuzingatia uhalisia wa ghalama kwenda kwenye kanda kwa ajili ya uhakiki!!
Msajili anajua fika kuwa NGOs nyingi zinaendeshwa na wananchi, ili kusaidiana na Selkari kufikisha huduma na maendeleo kwa jamii ya watanzania, anajua fika kuwa ghalama za kusafiri kula na kulala ngazi ya kanda zingeweza kuboresha huduma kwa walengwa ndani ya jamii.
Pamoja na unyeti wa zoezi lenyewe ambalo naunga mkono mia kwa mia niombe mamlaka za juu ziangalie jinsi ya kufanya zoezi hili kwa umakini na ufanisi bila ya kuzua manu`guniko, pengine ni vyema walau zoezi hili likafanyika ngazi ya mkoa, amabapo Mhe. Rais amatuhakikishia kuwa selkari ipo na ina uwezo wa kutoa huduma kikamilifu bila kulazimika kufuata huduma hiyo ngazi ya kanda. Mwisho ni vyema Msajili wa NGOs na washauri wake wajipime katika hili kisha waungane na wale wote walio omba msamaha kwa kumkwaza Mhe. Rais.