MSAJILI WA HAZINA: Simon Group inamiliki 51% ya Hisa UDA na Serikali 49%, Jiji halina hisa

Siku zote nimekuwa nikijiuliza iwapo Mafuru ni mtu sahihi kuwa msajili wa hazina. Uhusiano wake na wapiga dili wa serikali ya awamu ya nne unatia shaka sana.
 
Mafuru unaogopa nini kusema UDA iliuzwa na Masaburi ( Didas binafsi , na wala si Didas Meya ) ambaye inadaiwa ana hisa SGL ? usipoangalia hata wewe utakwenda na maji .
Huyu ni jipu namba moja, naona mambo mengi hajui yanavyo endelea. hajui yupo pale kulinda masilahi ya nani.
 
...
...
...
...
Kubenea amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu

“Watu hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa,” amesema Kubenea.
51% za UDA hazikua zikimilikiwa na Dk. Didas Masaburi, Mwanasheria wa jiji Isaac Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa peke yao, bali wakazi wa jiji kupitia kwa madiwani wao waliokuwepo kipindi hicho. Mafuru asibariki wizi huo eti kwakua ulifanywa na meya wa jiji, huyo meya nae alikua ana mipaka yake ya kufanya maamuzi.
 
Watu wanne tu!
 
"Msajili wa Hazina katika hili ameonekana wazi kuwa sio mlinzi tena wa mali za umma ambazo zimewekwa chini yake Bali ni mwizi au anayeshirikiana na wezi.
Magufuli ajue wazi kaachiwa mchwa eti utunze ghala la nafaka, na asipomshughulikia asije kuta anaambiwa serikali yake inalipia kodi majengo ya Ikulu kwani yalishauzwa kisheria siku nyingi" -Chakaza
 
Huko bungeni kuna madai ya baadhi ya wabunge kuhongwa enzi zile ili waridhie uuzwaji wa UDA na wengine walichomekea kuwa ni bora mzawa SGL apewe kuliko Quality Group.
Nakumbuka kamati za bunge zilikuwa zinapingana, LAAC kwa upande mmoja na PAC kwa upande mwingine, kila moja ikituhumu kamati nyenzie. Waziri wa Fedha Mkuya na Naibu Malima wakawa wanapinga kuwa serikali haijauza hisa zake na Jiji halikuwa na mamlaka ya kuuza hisa za serikali ndani ya UDA bila ruhusa ya serikali.

Ila kauli ya Mafuru kama ilivyoripotiwa hapo juu inajichanganya....kama mwandishi hajakosea.

Hapa kuna hoja mbili:
1. Je SGL wanamiliki UDA kwa 100%
2. Je SGL wana hisa 51% na Jiji 49%

Kuna SGL, JIJI na SERIKALI. JIJI lilikuwa luna miliki 51% na SERIKALI ilikuwa inamiliki 49% ya hisa za UDA. JIJI likaiuzia SGL hisa 51%. Hivyo kwa sasa UDA inamilikiwa na wabia wawili ambao ni SGL (51%) na SERIKALI (49%).
Swali ni je, taratibu zilifuatwa katika kuuza hisa za JIJI?
 
Kwa maoni yangu: HAZIKUFUATWA! Na ilivyo sasa ina maana Jiji halina chake UDA!
 
Kama Halmashauri ya Jiji ya sasa itajiridhisha kuwa taratibu hazikufuatwa iungane na wananchi wa Jijini Dar wafungue shauri mahakamani kuwashitaki waliokiuka taratibu. Upande wa utetezi hapa waweza kuwa viongozi wa jiji waliokuwepo pamoja na SGL. Nadhani hapa mahakama itatusaidia.
 
Kisena amenukuliwa akisema SGL inamiliki 77% za UDA, tafuteni uzi wa BAK muone jinsi SGL ilivyopata hizo asilimia 77. Haya mambo ya 51 kwa 49 sijui yanatoka wapi?
 
SERIKALI imetetea uuzwaji wa hisa za Shirika la Usafirishaji nchini (UDA) kwa Kampuni ya Simon Group naKwa ufupi
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugezi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Alex Mamtei alisema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kutatua tatizo la uchakavu wa miundombinu na kuongeza kina cha maji
By Suzan Shayo Mwananchi; Mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Wizara ya Uchukuzi kwa niaba ya serikali na Benki ya dunia, Trade Mark East Africa na Department For International Development (DFID) zimetuliana saini ya makubaliano ya shillingi trilioni1.5 kutekeleza mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam.

Fedha hizo zitasaidia uboreshaji wa miundombinu ya Bandari na uhamishaji wa gati la mafuta la KOJ pamoja na mabomba ya mafuta katika eno la ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugezi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Alex Mamtei alisema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kutatua tatizo la uchakavu wa miundombinu na kuongeza kina cha maji pamoja na lango la kuingilia kwenye meli.

“Bandari ilivyo sasa kina cha maji ni kifupi mno na miundombinu inatisha kwa uchakavu wake, hivyo wizara ya uchukuzi kwa niaba ya Serikali imeamua kuungana na wadau tajwa ili kufanya marekebisho ya haraka kunusuru Bandari na mapato yake,” alisema Mamtei.

0.3k 0 0 0 0 0 0.3k
kwamba, kampuni hiyo inamilika hisa hizo kihalali.

Lawrance Mafuru, Msajiri wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliiuzia UDA hisa kihalali.

Utetezi huo unawapa pumzi Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Ridhwan Kikwete, mtoto wa rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa Mbunge wa Urambo Magharibi ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa wana hisa kwenye kampuni hiyo.

“Bodi ya UDA iliyokuwepo muda ule ilikiuka taratibu za uuzaji wa hisa za serikali bila ya Baraza la Mawaziri ambalo lenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya uuzwaji wa hisa kuamua kuuza hisa hizo,” amesema Mafuru.

Anaeleza kuwa, Bodi ya UDA iliamua kuuza hisa kwa Kampuni ya Simon Group baada ya kuona shirika hilo linayumba hivyo lilihitaji muwekezaji ili kulifufua.

“Baraza la Mawaziri chini ya mwenyekiti wake ambaye ni rais halikukaa kikao cha kufanya maamuzi ya kuuza hisa na kwamba, baada ya bodi kuona serikali inachelewa kutoa maamuzi ikaamua kuuza hisa za serikali,” anasema.

Amefafanua kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ndilo lililouza hisa zake kupitia Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji hilo kwa kushirikiana na wajumbe wenzake watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji.

“Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na jiji, lilipokea fedha kutoka Kampuni ya SGL kwa ajili ya manunuzi ya hisa zake na kwamba kwa sasa jiji halimiliki UDA, ” amesema.

Amedai, UDA linamilikiwa kihalali na Kampuni ya SGL ambayo inahisa asilimia 51 iliyouzwa na jiji pamoja na serikali ambayo ina hisa ya asilimia 49.

“Aliyeuza hisa za UDA kwa SGL ni Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wajumbe wengine watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji, sasa kama Masaburi hakuwa Meya halali wa jiji basi hisa hazikuuzwa kwa kampuni ya SGL,” ameeleza.

Akieleza mwanzo wa ugawaji wa hisa za UDA kutoka kwa serikali kwenda Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema, serikali iliona bora igawe hisa za asilimia 51 kwa jiji hilo ambalo UDA linapofanya kazi zake.

“Mnamo mwaka 1974 serikali ilianzisha shirika la UDA, mwaka mmoja baadaye serikali iliamua kugawa hisa ya asilimia 51 kwenda kwa jiji la Dar es Salaam na yenyewe kubaki na asilimia 49 ambazo inazo hadi sasa,” amesema.

Hivi karibuni Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Baraza la Halmashauri ya Jiji hilo lilikana kuitambua Kampuni ya SGL kuwa, mmiliki halali wa UDA.

Kwa mujibu wa maelezo yao, Masaburi alichukua jukumu la kuuza hisa za jiji kwa Kampuni ya SGL bila kulishirikisha baraza la madiwani la kipindi ambacho uuzaji ulipofanyika.

Siku tatu zilizopita, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo alisema, halmashauri haikuuza UDA licha ya Simon Group Limited kudai kununua.

Kwenye mkutano huo ambao pia uliohudhuriwa na Isaya Mwita Charles, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Kubenea alisema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu.

“Kwanza tunataka mtambue halmashauri haikuuza UDA kwa kuwa, Simon Group Limited wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi kufanya biashara. Haturudishi fedha hizi mpaka tufanye hesabu, tujue kampuni hii imepata faida kiasi gani.

“Hata katika mradi wenyewe wa UDA-TR, kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011, uliosimamiwa na Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa hisa za UDA, haukuwa halali,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu

“Watu hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa,” amesema Kubenea.
Code:
 
Hatari hapo Wanunuzi wa hisa ni watu wazito nijuavyo mimi kukiuka utaratibu ni kuvunja sheria,kama mchakato ulizingatia utaratibu wanunuzi Wanahaki lakini kama kunawajanja walipiga dili itakuwa kazi maana Dar imeshikwa na Ukawa hakuna mchezo ukiongeza na safu ya utawala basi mbivu zitajulikana tu ingawa muda unasonga
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu hakuna ushahidi wa kuthibitisha kampuni ya Simon Group ni wamiliki halali wa UDA, yule msajili wa hazina Lawrence Mafuru anadai kwamba hii kampuni ni wamiliki halali wa UDA, lakini mpaka sasa hivi ameshindwa kuweka hadharani ushahidi (documents husika) kuonyesha kwamba UDA sasa inamilikiwa na Simon Group.

Wakati huo huo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ameweka ushahidi wake wa kuonyesha kwamba:
1. Kikao cha hao walioamua kuuza hisa za UDA kilikuwa haramu kwa kutohudhuriwa na madiwani wa Jiji na pia kiliendeshwa bila kupata Baraka za madiwani wa Jiji. Kwa maneno mengine hawa watu hawakuwa na uwezo wa kisheria kuamua kuuza hisa za UDA.
2. Hisa za UDA zilishushwa thamani yake kinyemela mpaka sasa hivi aliyeamua kushusha thamani ya hisa za UDA hajulikani.
3. Hata baada ya thamani ya hisa za UDA kushushwa kilicholipwa ni robo tu ya bei za hisa zile. Kingine cha kustaajabisha Idd Simba kalipwa pesa nyingi shilingi 320 million kuliko pesa zilizolipwa kununulia hisa shilingi 285 million ambazo ni sawa na robo ya thamani ya hisa baada ya kushushwa bei kinyemela.
4. Mlipaji Mkuu wa Serikali hatambui uuzwaji wa hisa za UDA.

Hivi ndivyo nchi ilivyoukuwa inaliwa na kuibiwa na mafisadi, sasa hapa itakula kwao vibaya. Hii ndio mifisadi JPM aliahidi kuwa atalala nayo sahani moja. Yetu macho. Haiwezekani UDA imeuzwa bila kushindanisha kupata bei ya soko, mauzo yanafanyika chini ya meza.

Madiwani wa Dar, watangaze tu kuwa UDA ni mali yao, hakuna uuzaji wowote wa kihalali uliopata kutokea. Wanaodai vinginevyo waende mahakamani, wakadhubutu kumhongo DPP. Majizi makubwa.
 
WildCardJF-Expert Member
#25 Jul 13, 2011
Joined:Apr 22, 2008 7,47217 38
Watanzania uendeshaji wa mashirika ya umma umetushinda siku nyingi. Tulishindwa TBL, tukashindwa TCC, tukashindwa CRDB, THB, NBC, tukashindwa NMC, mashirika ambayo wateja wake sio wa kutafuta. Wanakuja wenyewe. Sasa hivi tumeshindwa TANESCO, tumeshindwa DAWASA/DAWASCO. Acha tu UDA iondoke. Hebu fikiria kituo kama kile cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo kinavyoendeshwa na mapato yanayopatikana pale! Kama mfumo wa uendeshaji mashirika ya UMMA ni huu tulionao na uongozi wa NCHI ni huu, Bunge ni hili, acha tu UDA iende inakokwenda. Mashirika ya UMMA yanatafunwa sana. Hayana mwenyewe
tumezoea kuita shamba la bibi , sijui hili tuliite shamba la babu au!!
 
Hii nchi naanza kupata hisia kuwa hata 50% ya watu wake wakifa wote hakutakuwa na hasara kwa dunia.
Yaani hizo million 350 alizowekewa Iddi Lion kwenye akaunti yake binafsi ndizo 51%!?
Tatizo la msingi hapa ni SGL ni nani hasa, natabiri serikali ikishindwa kuujulisha umma leo isije kushangaa mbeleni akajulikana baada ya mtafaruku usio wa lazima.
Ina maana thamani ya shirika zima pamoja na barabara ya mwendo kasi pungufu ya million 700? Iam sincerely humbled.
 
SERIKALI imetetea uuzwaji wa hisa za Shirika la Usafirishaji nchini (UDA) kwa Kampuni ya Simon Group na kwamba, kampuni hiyo inamilika hisa hizo kihalali.

Lawrance Mafuru, Msajiri wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliiuzia UDA hisa kihalali.

Utetezi huo unawapa pumzi Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Ridhwan Kikwete, mtoto wa rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa Mbunge wa Urambo Magharibi ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa wana hisa kwenye kampuni hiyo.

“Bodi ya UDA iliyokuwepo muda ule ilikiuka taratibu za uuzaji wa hisa za serikali bila ya Baraza la Mawaziri ambalo lenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya uuzwaji wa hisa kuamua kuuza hisa hizo,” amesema Mafuru.

Anaeleza kuwa, Bodi ya UDA iliamua kuuza hisa kwa Kampuni ya Simon Group baada ya kuona shirika hilo linayumba hivyo lilihitaji muwekezaji ili kulifufua.

“Baraza la Mawaziri chini ya mwenyekiti wake ambaye ni rais halikukaa kikao cha kufanya maamuzi ya kuuza hisa na kwamba, baada ya bodi kuona serikali inachelewa kutoa maamuzi ikaamua kuuza hisa za serikali,” anasema.

Amefafanua kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ndilo lililouza hisa zake kupitia Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji hilo kwa kushirikiana na wajumbe wenzake watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji.

“Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na jiji, lilipokea fedha kutoka Kampuni ya SGL kwa ajili ya manunuzi ya hisa zake na kwamba kwa sasa jiji halimiliki UDA, ” amesema.

Amedai, UDA linamilikiwa kihalali na Kampuni ya SGL ambayo inahisa asilimia 51 iliyouzwa na jiji pamoja na serikali ambayo ina hisa ya asilimia 49.

“Aliyeuza hisa za UDA kwa SGL ni Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wajumbe wengine watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji, sasa kama Masaburi hakuwa Meya halali wa jiji basi hisa hazikuuzwa kwa kampuni ya SGL,” ameeleza.

Akieleza mwanzo wa ugawaji wa hisa za UDA kutoka kwa serikali kwenda Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema, serikali iliona bora igawe hisa za asilimia 51 kwa jiji hilo ambalo UDA linapofanya kazi zake.

“Mnamo mwaka 1974 serikali ilianzisha shirika la UDA, mwaka mmoja baadaye serikali iliamua kugawa hisa ya asilimia 51 kwenda kwa jiji la Dar es Salaam na yenyewe kubaki na asilimia 49 ambazo inazo hadi sasa,” amesema.

Hivi karibuni Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Baraza la Halmashauri ya Jiji hilo lilikana kuitambua Kampuni ya SGL kuwa, mmiliki halali wa UDA.

Kwa mujibu wa maelezo yao, Masaburi alichukua jukumu la kuuza hisa za jiji kwa Kampuni ya SGL bila kulishirikisha baraza la madiwani la kipindi ambacho uuzaji ulipofanyika.

Siku tatu zilizopita, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo alisema, halmashauri haikuuza UDA licha ya Simon Group Limited kudai kununua.

Kwenye mkutano huo ambao pia uliohudhuriwa na Isaya Mwita Charles, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Kubenea alisema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu.

“Kwanza tunataka mtambue halmashauri haikuuza UDA kwa kuwa, Simon Group Limited wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi kufanya biashara. Haturudishi fedha hizi mpaka tufanye hesabu, tujue kampuni hii imepata faida kiasi gani.

“Hata katika mradi wenyewe wa UDA-TR, kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011, uliosimamiwa na Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa hisa za UDA, haukuwa halali,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu

“Watu hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa,” amesema Kubenea.
mahali popote penye mikono ya nani liu hakuna kesi nyie bwabwajeni tuuuuuuuuuu........... mtanyamaza na kusahau
 
Back
Top Bottom