Msajili wa Hazina Ndg. Lawrence Mafuru hajui au kashasahau lugha ya Taifa ya Kiswahili?

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
Nimesikiliza na nimetazama video za huyu Msajili wa Hazina wakati anatoa taarifa kwa umma juu ya hali ya mzunguko wa fedha nchini ambao unaleta mtafaruku mkubwa ndani ya hii nchi ya watu zaidi ya milioni 50 na ninasikitika kusema kuwa huyu ndugu pamoja na jitihada zake za kutaka kutujuza sisi wananchi kuhusu hii kadhia ya ya fedha lakini mfano mbovu sana wa viongozi wetu.

Inawezekana vipi kuwa mtu mwenye dhamana kubwa kama Lawrence Mafuru aitishe mkutano na vymbo vya habari halafu anatumia zaidi ya asilimia 90 ya maneno yake kuongea maneno mengi ya Kiingreza kilichojaa misamiati migumu ya kiingereza ambacho Mtanzania wa kawaida hawezi kumuelewa? Naamini kabisa kuwa Mafuru nia yake haikuwa kutujuza yanayoendelea bali ni kutughilibu na maneno mengi ya kiingereza ambayo hayaeleweki.

Hili tatizo nimeliona sana kwa viongozi wetu wakiwepo Bungeni, wakiongea kwenye runinga au radio na mbaya zaidi mpaka miswada na sheria zetu nayo inaandikwa kwa kiingereza ambacho asilimia kubwa ya watanzania hawaelewi na inafanana sana mikataba mibovu ya kilaghai ya wakoloni.

Nikirudi kwa huyu Ndugu Lawrence Mafuru, je hajui kuongea Kiswahili fasaha cha kueleweka au mbwembwe ya kutaka kutuvuruga na kutughilibu tusielewe haya mambo nyeti ya kitaifa?

Wito kama tumefikia hatua ya kuwapa madaraka wasiojua lugha ya Taifa bas serikali iajiri watu kutoka BAKITA kwenye kila idaya ya serikali ili mawasiliano awe mopes kwa na wananchi

Na kama imeshindikana naomba Ndugu Magufuli toa agizo kuwa hawa watu wa serikali waongee kwa kikswahili ili wananchi wapate kuwaelewa na wasiojua Kiswahili wapelekwe kwenye kozi maalum ya kujua hii lugha ya Taifa (kwa gharama zao)

Ushahidi wa ghilba ya Lawrence Mafuru huu hapa:

Nani alikwambia ukimbie umande? :D:D:D By the way, kiswahili hakina misamiati ya kutosheleza kuelezea hayo mambo ya kitaalam aliyokuwa anayazungumzia.
Mfano neno 'liquidity' kwa kiswahili ni 'maji maji' kwa hiyo kama angezungumza kwa Kiswahili lugha ya taifa angesema kuwa
'benki nyingi zina kosa hewa (suffocate) kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, kitu ambacho kwa Mbongo wa kawaida angesema kuwa kama benki zinakosa hewa kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, si waende DAWASCO? :(:(:(
 
endeleeeni tuuu
 
huyo jamaa namjua sana, nilisoma naye o'evel ni bishow fulani hivi, hiyo tabia ya kuongea na kuchomeka maneno ya kiingereza ni tabia yake. Kwa ujumla kwake imekuwa kilema. Ila sishangai kwani hata mkui hawezi kuongea kiingereza kilichonyoka lakini kila mara anachomeka maneno ya kiingereza. Hicho ni kilema cha nchi yetu, ili mtu awakoge watu kuwa ni msomi wakati anaongea anachombezana vijimaneno vya kiingereza. Ukitaka kucheka anza kuongea naye kiingereza cha kunyooka, mbona utamuonea huruma jinsi anavyovuruga.
 
Hayo ni mambo ya kitaalamu, kaeleza kutokana na taaluma yake aliyochukua muda mwingi na garama kusoma... sasa yule ambaye wakati anaenda shule yeye ndio anavuta shuka kumrithisha bwana usingizi amsaidieje?
acha hizo ww, hiyo ni mikogo ya kilimbukeni tu. Kama unaongea na watu wa kawaida unatumia kiswahilo fasah na mifano mirahisi, labda tena ikibidi uweke maneno machache ya kitaalam ambayo sio ya kiswahili. Lakini sio unatoa ufafanizi kwa 95% ya hadhira inayotumia kiswahili halafu unakuta ufafanuzi wako una 60% ya maneno ya kiingereza. Naita ya kiingereza na wala sio ya kitaalamu. Ulimbukeni na mikogo sio poa.
 
Press conference yake imeeleweka vizuri tu wala hakuna mwandishi wa habari aliyelalamika kuwa hajaelewa kilichosemwa.

Na ujumbe alioutoa ndiyo huyo ambayo kila mmoja ameusikia au kuusoma kupitia media mbalimbali.

Labda kama una lako binafsi dhidi ya huyu jamaa.
 
Nani alikwambia ukimbie umande? :D:D:D By the way, kiswahili hakina misamiati ya kutosheleza kuelezea hayo mambo ya kitaalam aliyokuwa anayazungumzia.
Mfano neno 'liquidity' kwa kiswahili ni 'maji maji' kwa hiyo kama angezungumza kwa Kiswahili lugha ya taifa angesema kuwa
'benki nyingi zina kosa hewa (suffocate) kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, kitu ambacho kwa Mbongo wa kawaida angesema kuwa kama benki zinakosa hewa kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, si waende DAWASCO? :(:(:(

wewe hujui kiswahili ndio maana unadhani hakina misamiati ya kujitosheleza. pia kumbuka misamiati kwenye lugha inakua kadri mizizi ya lugha inavyotumika. hebu tuondelee mning'inio wa ukoloni. kwa taarifa yako mimi sikukimbia umande, huko ilikozaliwa lugha ya malkia nimepita vya kutosha. mswahili fakhari yangu kiswahili
 
Aiseeeerr
 
Hayo ni mambo ya kitaalamu, kaeleza kutokana na taaluma yake aliyochukua muda mwingi na garama kusoma... sasa yule ambaye wakati anaenda shule yeye ndio anavuta shuka kumrithisha bwana usingizi amsaidieje?
Ina maana msajili wa hazina wa France,uholanzi,ujerumani,China huwa wanachomekea vijineno vya ngeli kwenye risala zao.

Halafu mtoa thread siyo anajisemea yy Bali akina mama,baba,wazee wengine ambao hawakupitia mnaposema elimu ya uchumi

Halafu kingine usikariri mfano mtu aliyesomea sayansi kuanzia o level mpaka chuo ,mambo ya elasticity nk ukimuambia hatoelewa sabb alipita nayo kushoto
 
huyo jamaa namjua sana, nilisoma naye o'evel ni bishow fulani hivi, hiyo tabia ya kuongea na kuchomeka maneno ya kiingereza ni tabia yake. Kwa ujumla kwake imekuwa kilema. Ila sishangai kwani hata mkui hawezi kuongea kiingereza kilichonyoka lakini kila mara anachomeka maneno ya kiingereza. Hicho ni kilema cha nchi yetu, ili mtu awakoge watu kuwa ni msomi wakati anaongea anachombezana vijimaneno vya kiingereza. Ukitaka kucheka anza kuongea naye kiingereza cha kunyooka, mbona utamuonea huruma jinsi anavyovuruga.
Hakuna post iliyonivunja mbavu kama hii...
Khaaa, we jamaa uko vizuri kwenye sekta ya kudiss na kupakaa!
 
Mambo ya kuchukua pesa huku na kupeleka kule, we we na mm tusiumize vichwa tuwaachie Binge ndilo lenye mamlaka ya mwisho kisheria. TRA hana mamlaka ya kuweka pesa kisheria. Anatakiwa skusanye na kupeleka BoT ambayo ndiyo mhazini wa serikali tayari kwa matumizi ya maendeleo n.k. Ni BoT pekeyake anayeweza kuweka pesa kama akiba kwa serikali (forex ). Kuweka fixed/ ac kwa TRA kunainyima serikali kufanya matumizi, hivyo kulazimika kukopa kwanye tasisi ya pesa kwa njia ya T/Bills mwisho wake serikali kulipa faida hadi 30% . na hapo utakuta pesa hizo ndizo alizoweka TRA. Kwa maana nyingine serikali inakopa pesa zake yenyewa. Hugo jamaa wa hazina amepotosha sana wutu.
huyo jamaa namjua sana, nilisoma naye o'evel ni bishow fulani hivi, hiyo tabia ya kuongea na kuchomeka maneno ya kiingereza ni tabia yake. Kwa ujumla kwake imekuwa kilema. Ila sishangai kwani hata mkui hawezi kuongea kiingereza kilichonyoka lakini kila mara anachomeka maneno ya kiingereza. Hicho ni kilema cha nchi yetu, ili mtu awakoge watu kuwa ni msomi wakati anaongea anachombezana vijimaneno vya kiingereza. Ukitaka kucheka anza kuongea naye kiingereza cha kunyooka, mbona utamuonea huruma jinsi anavyovuruga.
 
Ina maana msajili wa hazina wa France,uholanzi,ujerumani,China huwa wanachomekea vijineno vya ngeli kwenye risala zao.

Halafu mtoa thread siyo anajisemea yy Bali akina mama,baba,wazee wengine ambao hawakupitia mnaposema elimu ya uchumi

Halafu kingine usikariri mfano mtu aliyesomea sayansi kuanzia o level mpaka chuo ,mambo ya elasticity nk ukimuambia hatoelewa sabb alipita nayo kushoto
Kuna baadhi ya nchi lugha yao imekamilika kwenye mambo ya kitaalamu lakini lugha yetu bado ni maskini, na ndio maana hadi leo wanaendelea kukopa maneno ya kiarabu kama "MUBASHARA" hiyo unapoelezea huwezi kukwepa matumizi ya maneno ya taaluma husika.
 
acha hizo ww, hiyo ni mikogo ya kilimbukeni tu. Kama unaongea na watu wa kawaida unatumia kiswahilo fasah na mifano mirahisi, labda tena ikibidi uweke maneno machache ya kitaalam ambayo sio ya kiswahili. Lakini sio unatoa ufafanizi kwa 95% ya hadhira inayotumia kiswahili halafu unakuta ufafanuzi wako una 60% ya maneno ya kiingereza. Naita ya kiingereza na wala sio ya kitaalamu. Ulimbukeni na mikogo sio poa.
Mtaumia sana. Wanje alipokuwa mbunge alikuwa Kiswahili fasaha kabisa!!
 
wewe hujui kiswahili ndio maana unadhani hakina misamiati ya kujitosheleza. pia kumbuka misamiati kwenye lugha inakua kadri mizizi ya lugha inavyotumika. hebu tuondelee mning'inio wa ukoloni. kwa taarifa yako mimi sikukimbia umande, huko ilikozaliwa lugha ya malkia nimepita vya kutosha. mswahili fakhari yangu kiswahili
Mkuu ebu mpe mifano ya maneno
Liquidity na suffocation kama lugha ya kibenki kwa Kiswahili.
 
Back
Top Bottom