HNIC
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 1,898
- 2,195
Nimesikiliza na nimetazama video za huyu Msajili wa Hazina wakati anatoa taarifa kwa umma juu ya hali ya mzunguko wa fedha nchini ambao unaleta mtafaruku mkubwa ndani ya hii nchi ya watu zaidi ya milioni 50 na ninasikitika kusema kuwa huyu ndugu pamoja na jitihada zake za kutaka kutujuza sisi wananchi kuhusu hii kadhia ya ya fedha lakini mfano mbovu sana wa viongozi wetu.
Inawezekana vipi kuwa mtu mwenye dhamana kubwa kama Lawrence Mafuru aitishe mkutano na vymbo vya habari halafu anatumia zaidi ya asilimia 90 ya maneno yake kuongea maneno mengi ya Kiingreza kilichojaa misamiati migumu ya kiingereza ambacho Mtanzania wa kawaida hawezi kumuelewa? Naamini kabisa kuwa Mafuru nia yake haikuwa kutujuza yanayoendelea bali ni kutughilibu na maneno mengi ya kiingereza ambayo hayaeleweki.
Hili tatizo nimeliona sana kwa viongozi wetu wakiwepo Bungeni, wakiongea kwenye runinga au radio na mbaya zaidi mpaka miswada na sheria zetu nayo inaandikwa kwa kiingereza ambacho asilimia kubwa ya watanzania hawaelewi na inafanana sana mikataba mibovu ya kilaghai ya wakoloni.
Nikirudi kwa huyu Ndugu Lawrence Mafuru, je hajui kuongea Kiswahili fasaha cha kueleweka au mbwembwe ya kutaka kutuvuruga na kutughilibu tusielewe haya mambo nyeti ya kitaifa?
Wito kama tumefikia hatua ya kuwapa madaraka wasiojua lugha ya Taifa bas serikali iajiri watu kutoka BAKITA kwenye kila idaya ya serikali ili mawasiliano awe mopes kwa na wananchi
Na kama imeshindikana naomba Ndugu Magufuli toa agizo kuwa hawa watu wa serikali waongee kwa kikswahili ili wananchi wapate kuwaelewa na wasiojua Kiswahili wapelekwe kwenye kozi maalum ya kujua hii lugha ya Taifa (kwa gharama zao)
Ushahidi wa ghilba ya Lawrence Mafuru huu hapa: