Silence does not constitute acceptance na ipo case law on that.Kuna mambo mengine yanapotokea inabidi uhoji kama akili zimezidi akili au ni kitu gani tena. Hivi kweli Msajili na wale wote ambao wanakubali Lipumba kurudia cheo chake ni kwamba hawajali kabisa kuwa maneno yana nguvu na maana? Lipumba ni miongoni mwa viongozi wabovu waliowahi kutokea - namuweka kundi moja na yule fulani - na ubovu huo naweza kusema sasa umekamilika.
Mtu mzima unaposimama kuchukua msimamo na ukamaanisha kuuchukua msimamo huo ni lazima uwe na ujasiri (nilitaka kutumia lile neno la Kiingereza lenye maana ya mipira) wa kuisimamia. Hii ni kweli hasa kama msimamo huo una matokeo ya kitaifa kabisa.
Ati kwamba Lipumba aliandika barua ya kutengua barua ya kujiuzulu na hivyo basi barua ile ya kujiuzulu haikuwa na nguvu tena! Sijui ni genius gani huyo anayetaka watu wakubali uongo kuwa ni kweli. Barua ya Lipumba kujiuzulu iliweka ni siku gani kujiuzulu huko kunaanza, haikusema kunasubiria sijui maamuzi ya chombo gani kingine. Angalau hivi ndivyo ambavyo nimeweza kuamini baada ya kusoma 'ushauri, maoni na maagizo' ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Sasa kama Lipumba alimaanisha uamuzi wake ule, na akaweka manyanga chini, barua yake ya "kutengua" ilikuwa ikiwa imechelewa. Mtu mwenye utimamu wa akili hawezi kutengua barua ya kujiuzulu wakati alisha effect kujiuzulu huko. Barua yake ya kujiuzulu ingekuwa inasubiri maamuzi kama Lipumba angeendelea kubakia ofisini na kufanya kazi zake kama kawaida akisubiria "chombo" kingine kuridhia uamuzi wake.
Kama Mwenyekiti wa Taifa wa chama alijua kwa hakika kabisa kuwa muda wa kikao hicho cha chama haukuwepo na asingeweza kusubiri na akaamua kuachilia ngazi na hivyo kueffect kujiuzulu kwake. Sasa baada ya kuongoka hawezi kuandika kutengua barua ya kitu ambacho tayari kimefanyika.
Mtu anapofunga ndoa na akapewa zile baraka za mwisho na kutangazwa ni "mume na mke" hawezi kugeuka na kusema anataka kutengua uchumba! Uchumba ulishapita ipo ndoa. Lipumba alipojiuzulu alijiuzulu in fact siyo kwa kumsingizia. Sijui msajili aliwahi kuona precedence ya wapi ya mtu kutengua kujiuzulu kwake nafasi yake baada ya kuiacha hiyo nafasi na kwenda kwenye shughuli nyingine!
Baraza Kuu lingeweza kumrudisha Lipumba kama lingetaka kwa kusema kuwa halikuridhia; lakini ukimya wake ni kuridhia tosha kwa sababu Lipumba alishaondoka na kukiachilia kiti cha Uenyekiti. Sasa unamrudisha vipi kwa kusema ati "alitengua". Ina maana hakuuacha uenyekiti wakati sote tulishuhudia kwa maneno yake (alipozungumza na waandishi wa habari) na alipohojiwa akiwa Kigali kuwa ameondoka Uenyekiti tuliingiwa na viwavi jeshi kwenye akili zetu kuwa hatukumuelewa?
Msajili tafadhali bana!
TAHARIRI YA ZAMAMPYA