Msajili, ifute CCM kuiokoa nchi kwenye janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msajili, ifute CCM kuiokoa nchi kwenye janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamayu, Nov 24, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Mapinduzi na "Green Guard"

  Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, 2010, tumekuwa tunasikia na kushuhudia vijana wa CCM kwa jina la ‘Green Guard' waliopewa mafunzo ya kijeshi wakiwatisha na kuwapiga wananchi na kuwaumiza, mfano kule Mara kuna dada mmoja alikatwa mkono na panga. Viongozi wa CCM walibariki matumizi hayo ya nguvu ili kufikia lengo lao la kisiasa – ‘ushindi wa kishindo' au ‘ushindi ni lazima' na kuongoza dola ya Jamhuri ya Muungano bila kukemea vitendo hivyo.

  Katiba inasema:
  Ibara ya 20
  (2) ...haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:
  (a) Kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa

  [Maswali ya Msingi: kuanzishwa na kutumika kwa ‘Green Guard' na matendo yao tuliyoyashuhudia sio kuvunja katiba? Kama ndio, kwa nini Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, hakifuti chama cha mapinduzi mpaka sasa? Je, naye si anavunja katiba kwa kutokifuta CCM na anapaswa kujiuzulu au kufikishwa mahakamani?]
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Unamaanisha CCM ijifute yenyewe? Tendwa ni kada wa CCM!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Lakini john tendwa anasikia kupitia hapa?.....au tutumie njia nyingine
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kila Mtanzania mwenye akili timamu anajua kwamba CCM sasa imelewa madaraka, baada ya takriban nusu karne ya utawala wa chama hicho (pamoja na TANU hapo mwanzo) imesha lewa madaraka, haijali wananchi na umasikini wao, viongozi wake wamedidimia katika kupanga dili za kifisadi kuliko maendeleo ya watu.

  Sasa hivi inatumia nguvu za dola kuminya nguvu ya umma ambayo waziwazi inaonekana kuja juu dhidi ya udhalimu unaofanywa na CCM. Katika chaguzi za Meya, inafanya kila mbinu kunyang'anya na wanaonyang'anywa eti wafumbe midomo.

  Walijariubu Mwanza ilishindikana, na wameahirisha ili watafute mbinu mpya. Kigoma wameshindwa. Mbeya wamepora kijanja. Arusha wamepora kavukavu bila hata ya aibu, na matokeo yake ni hayo!!

  Natoa witu kwa Msajili wa vyama kukifuta chama hiki kabla ya kuipeleka nchi kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe.

  Please Msajili, do that, na utakuwa umeliokoa taifa. Wanayng'anye mafisadi hawa usajili, halafu ufanyike uchaguziu wqa haki bila ya serikali yao (CCM) kuusimamia.

  Haiwezekani wote tunaonekana kwenda na upofu na kutumbukia kwenye korongo ili hali kuna watu wanaoweza kukwepesha janga hilo.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kesi ya nyani kula mahindi unampa ngedere awe hakimu na nguruwe awe wakili wako sio?
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  aifute CCM wakati yeye mwenyewe ni kada number moja!! Ivuga umenena.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani katika CCM hakuna hata mmoja mwenye akili timamu ya kuiokoa nchi hii?
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM imekaa kidikteta tu na hakuna tofauti na Mugabe! Kwanza kuwa na Rais kama JK ni aibu kubwa sana kwa nchi hii!!!!
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  tendwa mnafiki hana uwezo huo, wa kuifuta ni sisi kwa vitendo, wana arusha wameonyesha njia na ujasiri wao ni wakuigwa
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweli ni aibu! Yaani tunakosa kitu kama umeme huku eti yuko tayari kumpa huyo nanii wake mabilioni ya bure! Kweli nmchi hii inatawaliwa kibwege!
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono iwapo itawezekana hii. Tunakwenda shimoni kwa sababu ya CCM na wao hawaoni, wanakalia ufisadi tu.
   
 12. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama msajili we Vyama umemsikia KIkwete Leo ameshangaa jinsi ambavyo kule kuwa na vurugu kwenye uchaguzi wa Ccm kiasi cha kutishana kwa silaha na watu kuumizana , Mbona husemi tamko kutoka kwako? AMA wewe matamko Yako ni ya upande mmoja .

  Huu ni ujumbe. Muhimu sana kwa Tendwa Kama msajili wa Vyama kuwa watu wanataka kuuana kwa silaha Lakini wewe uko kimya Kama hakuna jambo, hii unaweza kuvikemea Vyama binging wewe?
   
 13. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  mwenzangu utalijua jiji mwenzangu andazi utanywea togwa mwenzanu hehe huu ni mpasho mwingine toka chama cha mipasho ....najinafaasi najinafasiiii
   
 14. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  ...mzee Tendwa kuna washiri Nzega wameshikia bastola,je haujawasikia?...
   
 15. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tendwa "nalifanyia uchunguzi" ndo kauli zao
   
 16. Root

  Root JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,854
  Trophy Points: 280
  Tendwa alikuwa anatingisha njiti
   
 17. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tendwa ni aibu ya wasomi nchini.
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tendwa hawezi kurupuka ni msomi na mtu makini kosa gani CCM wamefanya huezi fananisha na Chadema wao walikuwa wanafanya mauaji na ni hatariii kwa usalama wa nchi.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  anatumika
   
 20. kelao

  kelao JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2012
  Messages: 4,831
  Likes Received: 1,228
  Trophy Points: 280
  mbwa hawezi kumn'gata bwana wake
   
Loading...