Msajili futa vyama vyote vya siasa, tuanze upya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msajili futa vyama vyote vya siasa, tuanze upya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bantugbro, Sep 19, 2009.

 1. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ...

  Imefikia wakati sasa nchi yetu inahitaji msukumo mpya, msukumo wa kifikra na kiuongozi (kila siku huwa tunalilia uchaguzi lakini matokeo ya uchaguzi mara zote huwa tunayafahamu hakuna jipya!).

  Nchi yetu pendwa imegubikwa na matatizo mengi ya kimaendeleo na kila kukichwa tunazidi kupatwa na matatizo lukuki na mapya (kmf. ufisadi uliokithiri, migogoro ya kisiasa haswa visiwani, viongozi uchwara n.k) kwa kweli sioni lini nchi hii itapata ufumbuzi wa japo robo tu ya matatizo haya. Unafuu hautapatikana kamwe katika kizazi hiki kama maamuzi makubwa na madhubuti hayatachukuliwa sasa!!!.

  Mtoa maamuzi hayo lazima aelewe kwamba maisha yake na familia yake yatakuwa hatarini lakini pia akumbuke kwamba atakuwa ameisaidia nchi hii pamojah na watu wake na hakika jina lake daima halitafutika vichwani na katika roho zetu kama mwokozi wetu.

  Napendekeza msajili wa vyama vya kisiasa avifutilie mbali vyama vyote vya kisiasa ikiwamo CCM na atangaze usajili mpya pamoja na masharti mapya (kmf. kutenganisha biashara na siasa, uzawa mbele, kuhakiki vyanzo vya mapato na matumizi ya vyama vyote, kuondokana na Takrima p.i.k Rushwa n.k). Kwa maamuzi hayo atakuwa amelipiga bao bunge letu ambalo kila kukicha tumekuwa tukilipigia kelele kuwa tunataka katiba mpya bila mafanikio yeyote!. Naomba afanye hivyo kabla ya uchaguzi mkuu ujao!

  Kwa maamuzi hayo ya kijasiri nchi hii itabidi iingie katika kipindi cha mpito ambapo serikali iliyopo madarakani itabidi iachie ngazi na iundwe ya mpito (siju ni jeshi au la, walau lakini tutakuwa pengine!) na ndipo tufanye uchaguzi mkuu mpya na vyama vipya!.

  Nadhani mpaka hapo tutakuwa tumeshajua nini cha kufanya, (wananchi wa kawaida, wasomi na wanaharakati wenye uchungu na nchi hii) ninauhakika kabisa tutaanza katika ukurasa mpya pamoja na katiba mpya na hata hayo maendeleo haitakuwa ndoto ya alinacha tena.

  Amani iwe Kwenu.
   
  Last edited: Sep 19, 2009
Loading...