Msajili apokea malalamiko ya Mwigamba

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]
mwigamba.jpg
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi, jana alipokea barua ya malalamiko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha Samson Mwigamba ya kuomba muongozo juu ya mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya chama hicho.
Akizungumza na Tanzania Daima, Jaji Mutungi alisema kuwa ameyapokea malalamiko hayo na kwa sasa anajiandaa kuanza kuyafanyia kazi.
Jaji Mutungi alisema kuwa suala hilo litafanyiwa kazi haraka na atahakikisha kutoa majibu hayo ndani ya kipindi kifupi.
“Ni kweli ofisi yangu imepokea barua hiyo na kwa sasa najielekeza kuanza kuyatekeleza na ninaahidi kumaliza utekelezaji kwa haraka na kisha kutoa mwongozo wa suala hilo.
Alisema kuwa hawezi kuweka wazi ni muda gani suala hilo litachukua lakini alisisitiza kuwa utekelezaji wake utakuwa ni mfupi kutokana na uzito wa suala hilo.
“Inaweza kuchukua wiki moja, mbili au hata tatu lakini kikubwa ni kuhakikisha tunayafanyia kazi yale yote yaliyowasilishwa katika meza yetu tena kwa haraka sana,” alisema.
Mwigamba aliomba mwongozo huo ujikite kwenye kipengele kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
Alisema Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) kinasema kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Alibainisha kuwa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasomeka kuwa kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena, mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi, huku akibainisha kuwa sentensi kuhusu ukomo wa uongozi imeondolewa.
Alisema sio kweli kwamba CHADEMA haijawahi kuwa na katiba ambayo ina ukomo wa uongozi, na kwamba katiba ya 2006 haikuandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele huku kipengele 5.3.2 (c ) kikiwa hakijawahi kujadiliwa
 
ni malalamiko ya MASIKINI MKULIMA AU NI YA SAMSON MWIGAMBA , AU WOTE WAWILI ?
 
Mwigamba, pambana kupigania haki yako watanzania wapenda amani na demokrasia wapo pamoja na wewe.
 
Chadema ni kikundi cha wanaharakati, kwa vyovyote vile issue sensitive kama katiba ya chama lazma wata overlook kwa sababu hawajajijengea viongozi, wana wafanyabiashara, hawajajijengea watendaji, wana wachumia tumbo.
 
Mwigamba, pambana kupigania haki yako watanzania wapenda amani na demokrasia wapo pamoja na wewe.

sijakuelewa una zungumzia watanzania gani ,labda kama kuna tanzania nyingine lakaini kama ndo hii ya mwl . Nyerere ya wasio penda wala rushwa na wasaliti,wabakaji,wauza pembe za ndovu na uuwaji watoa kucha, walipua mabomu yaani dah yapo mengi hadi nachoka ,hapa umechemka labda kama unawasemea waleeeee wenzio.
 
ha ha wanafiki vp hujamshauri na msaliti mwenzako zitto kuhusu majina ya akaunti za uswizi yameibiwa au panya alitafuna
 
Mwigamba, pambana kupigania haki yako watanzania wapenda amani na demokrasia wapo pamoja na wewe.

Tusidanyanyane kwa hili ni ngumu sana kwa mtu binafsi kushindana na Taasisi halafu Ukashinda ila ni Rahisi sana kwa taasisi kushinda kama itashindana na Taasisi Mwigamba nw is no longer again kwa Ushauri wa Wazi tu kuomba Msamaha ni busara sana kuliko kujifanya unajua hata kama upo sahihi. Hata hivyo lazima ujue unashindana na nani pia. Mfano Chadema ni Chaguo la Mungu sasa Mwigamba anataka kushindana na Mungu this is radiculous.
 
Iyo tunaita njaa kali, tena itamtokea puani hivi unafikiri wanachama ndo wanataka hata kumuona huyo Mwigamba kwanza tulivyo na hasira nae hatutaki hata kumuona kwenye chama chetu. Mtake msitake Mbowe ndio Mwenyekiti wetu kwa hiyo hizo ndoto mlizonazo za kufikiri kuna mtu wakukaa pale badala yake ondoeni kwani hazipo. Na wala msifikiri kuwa Mbowe ndo anautaka huwo uwenyekiti ila ni wanachama ndo tunamlazimisha kukaa hapo.

Mwigamba, pambana kupigania haki yako watanzania wapenda amani na demokrasia wapo pamoja na wewe.
 
Tusidanyanyane kwa hili ni ngumu sana kwa mtu binafsi kushindana na Taasisi halafu Ukashinda ila ni Rahisi sana kwa taasisi kushinda kama itashindana na Taasisi Mwigamba nw is no longer again kwa Ushauri wa Wazi tu kuomba Msamaha ni busara sana kuliko kujifanya unajua hata kama upo sahihi. Hata hivyo lazima ujue unashindana na nani pia. Mfano Chadema ni Chaguo la Mungu sasa Mwigamba anataka kushindana na Mungu this is radiculous.
You are the stupidiest man alive, leave God away from dirty politics
 
Chadema ni kikundi cha wanaharakati, kwa vyovyote vile issue sensitive kama katiba ya chama lazma wata overlook kwa sababu hawajajijengea viongozi, wana wafanyabiashara, hawajajijengea watendaji, wana wachumia tumbo.

mumrecruit mwigamba lumumba fc.atawasaidia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom