Msajili ajipanga kuanza uhakiki wa CCJ wiki hii

Taarifa ambazo nimezipata kutoka vyanzo vya uhakika toka ofisi ya msajili vinadokeza tu kuwa presha kubwa ambayo wananchi kwa kutumia mtandao wa simu wametoa kuanzia wiki iliyopita. Msajili ameonesha nia ya kutotaka mgongano na kwa kutumia hekima ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa CCJ leo na hatimaye kuafikiana kuanza uhakika katika mikoa minne ili kuweza kujiridhisha kuwa CCJ ina wanachama inaosema inao ili hatimaye kukipatia usajili wa kudumu.

Tunamshukuru Msajili kwa hatimaye kuepusha mgongano uliokuwa utokee huko mbeleni pasipo ulazima na hekima imetumika. Ni matumaini yangu katika uhakiki huo watafanya kwa haki, kwa wazi na kwa kutumia vipimo vile vile ambavyo vimetumika kwa vyama vingine pasipo kukibebesha CCJ mzigo ambao chama kingine hakikutakiwa kubeba kilipojaribu kupata usajili wa kudumu.

Tayari habari hizi zimeshagusa mamia ya watu mbalimbali nchini ambao wanasubiri kwa hamu usajili huu wa kudumu. Wakati huo huo timu za kuandika Katiba ya Kudumu ya CCJ pamoja na mambo ya Ilani, na utaratibu wa kupata wagombea ziko kazini ili kuhakikisha tu pindi CCJ ikipata usajili wa kudumu, mkutano mkuu wa kwanza wa taifa kufanyika ili hatimaye kupitisha Katiba mpya na kujipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Habari ndiyo hiyo.

Ni habari njema lakini itakuwa njema zaidi pale atakapotoa cheti cha usajili wa kudumu katika muda muafaka. Kama sikosei alisha wahi sema kuwa akikuta kuna mwanachama amekufa basi hatakipa usajili. Ni matumaini yangu kuwa kwa muda huu wote baada ya kukaa na majina ya wananchama wa CCJ ofisini kwake haujafanyika mchezo mchafu wa kuwafuatilia hao wanachama kichinichini na kuwanunua ili waikane CCJ pindi watakapokuwa approached na msajili wakati wa uhakiki ili kuhalalisha malengo yao ya kukinyima usajili wa kudumu CCJ. Maana kwa CCM hili pia lawezekana.
 
CCM na serekali yake wapo Very very advance subirini mtajioneya wenywe .

Mkuu rejea posting yangu iliyopita,unaposema "CCM" wengine kwetu means CCM-Something=CCJ,Umenipata?Ila kama kweli kauli yako ikasimama kuwa CCM=CCM until uchaguzi...Then sina shaka nitakubaliana kuwa for a certain one party is is more advanced than the other,maana siwezi kuona njia nyingine yoyote ya kusema "advaced" other than the fact if ccm stays the same na ccj goes and scramble for whatever is left on upinzani.
 
bahati mbaya sana sijui kinachoendelea na hiki chama, naomba mlioko bongo mtusaidie kama hiki chama si mtoto wa ccm.....si unajua aliyegongwa na nyoka hata akiona unyasi tu anaruka...ccm imetuchosha jamani, Mungu asaidie iki chama na watu wake wote waondoke siku moja kama ilivyokuwa KANU kenya...kama si hivyo, basi itakuwa habari njema.
 
By DAILY NEWS Reporter, 31st May 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 48

THE government said today that it has no plans to fast track full registration of Chama Cha Jamii (CCJ), due to lack of funds to finance the exercise.

The Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs), Mr Phillip Marmo, said the office of the Registrar of Political Parties is currently operating on a budget allocated to it for the 2009/2010 financial year.

He said that CCJ was not going to get any special treatment. “It will be treated just like any other party, including those which have applied for full registration much earlier and have not yet been given a go ahead,” Mr Marmo explained.

“It is unfair to blame Mr Tendwa for any delay. This is not a personal issue, but rather a question of how the office operates on the basis of available resources,” he said.
 
Mkuu umeshapitia ile thread ya "Tendwa kuendelea na uhakiki"?Ama keshavihakiki hivyo vyama vingine Marmo anavyodai "vilikuja kabla ya CCJ"?Tatizo mara vyama vingine mara fedha,mtakoma mwaka huu,naona mmekaliwa pabaya...Teh teh teh!
 
Wee subiri tu siku Tendwa atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya KUVUNJA SHERIA. Atashangaa hao CCM ndiyo kwanza watamuondoa na kumuweka mwingine wakati na yeye akienda kuchukua kitanda cha Mzee wa magari Mekundu aka Liyumba balaa.....
Nafikiri tunakokwenda, kuna wengi sana watashitakiwa kwa kuvunja SHERIA au KATIBA. Kwa sasa hivi wanajiona wako juu ya sheria ila kuna siku watakuwa watu wa kawaida, na watajuta kuzaliwa.
 
Hongera CCJ presha yenu tumeiona na haijawahi kutokea hapa nchini kweli nyinyi ni chama cha upinzani. Nimeanza kuona matunda ya Itikadi
 
By DAILY NEWS Reporter, 31st May 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 48

THE government said today that it has no plans to fast track full registration of Chama Cha Jamii (CCJ), due to lack of funds to finance the exercise.

The Minister of State in the Prime Minister's Office (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs), Mr Phillip Marmo, said the office of the Registrar of Political Parties is currently operating on a budget allocated to it for the 2009/2010 financial year.

He said that CCJ was not going to get any special treatment. "It will be treated just like any other party, including those which have applied for full registration much earlier and have not yet been given a go ahead," Mr Marmo explained.

"It is unfair to blame Mr Tendwa for any delay. This is not a personal issue, but rather a question of how the office operates on the basis of available resources," he said.

Mkuu kama wakuu wa juu ndo tamko lao jua kwamba CCJ will not get reg on time
 
Hivi kumbe kuna vyama viliomba usajili kabla ya CCJ. kuna mwenye taarifa ni vyama gani hivyo na viliomba usajili lini? But hii sasa naiona imekaa kisheria na kuna loophole ambayo ofisi ya msajili inaweza kuitumia.

Kama vyama vikipata usajili wa muda vinapewa limit ya siku ya kuwa vimeomba usajili wa kudumu la sivyo vinatupiliwa mbali. Kwanini hakuna sheria inayomuongoza msajili kuwa chama kikiwasilisha maombi ya usajili wa kudumu msajili lazima atoe jibu within specified time limit.

Ingawa hii ni mada nyingine napenda kupata ufafanuzi au kueleweshwa mgao wa ruzuku kwa vyama utakuwa ni shilingi ngapi ? Au uta base kwenye nini hasa kwa vyama vipya visivyokuwa na wabunge.

Nauliza hivi sababu wasi wasi wangu naona tusije tukawa na ma politic enterprenuers amabo wanalenga kwenye ruzuku tu mara baada ya uchaguzi na vyama vyao vinakufa
 
Mkuu kama wakuu wa juu ndo tamko lao jua kwamba CCJ will not get reg on time

No no no! CCJ ni chama tofauti na vyama vingine na kimekuja na itikadi. Hakuna kitu kitakachoizuia CCJ isisajiriwe and believe me wanajua muda watakaosajiriwa!

Unataka kwenda morogoro, mabasi ya abood yako kibao wewe unasubiri mpaka hammer yako ije kutoka japan? wewe lengo lako sio kwenda moro bali kwenda kuwaringisha washikaji!
 
Nilikuwa najiandaa kwenda kupumzika saa kumi na nusu hizi za alfajiri wakati vinzi karibu na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa vinadokezakuwa leo mchana msajili amepanga kukutana na uongozi wa CCJ.. Nadhani itasaidia kuepusha hisia mbaya baina ya pande hizi mbili na masuala ya umuhimu wa kitaifa yataweza kupatiwa suluhu ya haraka ili hatimaye kila mmoja afanye anachotakiwa kufanya katika kuendeleza demokrasia na hatimaye kulipatia taifa uongozi unaostahili wenye ajenda isiyo na utata.

Nalala kama sungura.!! see u later inshallah.

Mbona chama hiki kinanguvu sana hata kabla ya kusajiliwa tuambie nani wapo nyuma ya pazia la chama hiki, na chanzo cha mabilioni yake kwani mnataka kumkopesha msajili wa vyama vya siasa, au kuna nguvu toka mataifa mengine?
 
Imekula kwa msajili na CCM yake mwaka huu. Ole wake asiisajili CCJ! ndo hapo atakapo jua maharage ni mboga! maana CCJ wamejipanga kweli si utani. We fuatilia issue zao tu. Huwezi kuniambia kuwa yule mweyekiti wao Kyabo ndo ananguvu hivi! Mimi ninachomuomba msajili atumie busara ili uchaguzi usivurugike!
 
Imekula kwa msajili na CCM yake mwaka huu. Ole wake asiisajili CCJ! ndo hapo atakapo jua maharage ni mboga! maana CCJ wamejipanga kweli si utani. We fuatilia issue zao tu. Huwezi kuniambia kuwa yule mweyekiti wao Kyabo ndo ananguvu hivi! Mimi ninachomuomba msajili atumie busara ili uchaguzi usivurugike!

Napenda iwe kama unavyosema wewe, lakini nadhani wote mnajua mambo ya hawa jamaa... lets just hope this time its different...najua watafanaya kila njia CCJ isishiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.. wanaweza kukubali too late na ikawa haina maana kwa CCJ..
Lets wait and see..
 
Tendwa apondwa kwa kutoisajili CCJ


na David Frank, Arusha

CHAMA cha Mawakili Tanzania (TLS) Mkoa wa Arusha, kimemkosoa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kwa kukataa kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ) kwa madai ya kutokuwa na fedha za kuhakiki wanachama wake walioko mikoani. Mawakili hao wamemtaka Tendwa kukisajili chama hicho na vyama vingine bila ubabaishaji kwa kile walichoeleza kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa kusajili vyama kwa madai ya kutokuwa na fedha kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria.

Wamesema kitendo cha msajili huyo cha kuweka visingizio kadhaa vya kukisajili chama hicho kinaweza kumtia matatizoni kwa kushtakiwa kwa kutofuata sheria kwa kuwa hakuna sheria inayomtetea kwa hilo.

Tamko lao la Mei 28 mwaka huu lililosainiwa na Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Arusha, Duncan Oola, limebainisha Tendwa ana wajibu wa kusajili na kutoa hati ya usajili wa kudumu kwa chama hicho na vingine vilivyowasilisha maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa kisheria.

“Tunachukua fursa hii kumkumbusha msajili huyo kwamba kama cheo chake kinavyojieleza chenyewe, kazi yake ya msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Sura Na. 258 (R.E. 2002) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na 7 ya 2009 ni kusajili vyama vya siasa,” inaeleza sehemu ya tamko hilo.

Aliongeza kuwa kifungu cha 8 (5) cha sheria hiyo kinatamka wazi kwa lugha ya Kiingereza kuwa lugha iliyotumika katika kifungu hicho ni ‘shall’ na siyo ‘may’ kwa maana Msajili hana hiari kukubali au kukataa kusajili chama ambacho kimetimiza masharti ya kisheria ya kupewa usajili ama wa muda au wa kudumu.

Tamko hilo liliongeza kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatakiwa kupokea na kushughulikia maombi ya usajili wa muda na wa kudumu wakati wote kwa kuwa sheria haijatenga kipindi maalumu cha kuwasilisha maombi ya kupewa usajili huo na kwamba sheria haijatamka muda ambao msajili anaruhusiwa kutopokea maombi ya usajili wa chama cha siasa.

Tamko hilo lilisema kuwa msajili anawajibika kuahirisha shughuli zote ambazo si za msingi ili kushughulikia maombi ya usajili wa chama cha siasa ikiwa ni pamoja na maombi ya Chama Cha Jamii kwa kuwa ndiyo kazi yake ya msingi.

Aidha, lilisema Tendwa anawajibika kuomba au kutafuta fedha za kumwezesha kutimiza majukumu yake ya msingi bila kutafuta visingizio kwani kutofanya hivyo ni kukwepa wajibu wake wa kisheria unaoweza kusababisha ashtakiwe kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria iliyotajwa hapo juu.

Hivi karibuni vyombo vya habari vilimnukuu msajili huyo akiwaambia viongozi wa muda wa CCJ kuwa hana fedha za kuzunguka kufanya uhakiki wa wanachama wake na kwamba kwa sasa ana majukumu mengine muhimu ya kufanya.

CHANZO: Tanzania Daima

hahaha....CCM bwana! Kazi kweli kweli! Siku CCM inaondolewa madarakani...sijui hiyo siku itakuwaje. Yani furaha yangu itakuwa kubwa mno! itakuwa zaidi ya Obama kushinda urais marekani!
 
Majibu ya Marmo yamenifanya tangu leo nianze kuitazama CCJ kwa jicho la tofauti. Sababu alizotoa Marmo hazina mashiko kabisa, ni kama vile mtu anayebisha jambo ambalo yeye mwenyewe anajua ni kweli kabisa. Marmo angetoa sababu nyingine lakini sio suala la fedha.

Sasa najiuliza ikiwa CCJ ni sawa na vyama vingine tu kibao, kwanini CCM wanaiogopa CCJ, mbona tafiti nyingi tu za kisayansi i.e REDET & Co wamesema CCM na JK wako juu. Hofu ya CCM na serikali itoka wapi?. Hii ndio imenifanya nianze kufuatilia habari za CCJ kwa umakini zaidi
 
ni jambo la busara kama msajili ameamua kufanya hiyvo, si kwa CCj tu bali kwa waTZ wote wapenda demokrasia. kwa muda uliobaki mpaka uchaguzimkuu, CCJ haiwezi kuleta upinzani mkubwa wakiruhusiwa kushiriki, bali wakinyiw haki ya kushiriki ndio uchaguzi utavurugka...
 
Waziri Marmo: CCJ haitashiriki uchaguzi






headline_bullet.jpg
Asema hakuna fedha za kukihakiki



Marmo(16).jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.



Serikali imezima ndoto za Chama Cha Jamii (CCJ) chenye usajili wa muda kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, kusema kwamba hakitapata usajili wa kudumu kabla ya uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, ambao aliuitisha kuzungumzia utekelezaji wa sera za serikali ya Awamu ya Nnne tangu iingia madarakani baadfa ya uchaguzi mkuu wa 2005, Marmo alisema chama hicho hakiwezi kusajiliwa kabla ya Uchaguzi Mkuu kwa vile serikali haina fedha ya kugharimia mchakato utakaofanikisha usajili huo.
Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, vyama vyenye usajili wa kudumu ndivyo tu vinaruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana, Marmo alisema CCJ haina sababu za msingi kumlaumu Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwa kushindwa kuhakiki wanachama na kutoa usajili wa kudumu kwa chama hicho.
Hata hivyo, Marmo alisema serikali inaendelea kuhakiki nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na CCJ kwa Msajili, kwa kuwa hatua hiyo haihitaji fedha.
Alisema CCJ ni miongoni mwa vyama sita vilivyoomba usajili na bado havijapata.
Alivitaja vyama vingine vilivyoitangulia CCJ kuomba usajili kuwa ni National Coalition Democratic Movement (NCDM) kilichopatiwa usajili wa muda Machi 2, mwaka huu; Democratic National Congress (DNC) kilichopata usajili wa muda Desemba 2, 2008.
Vingine ni Democratic Movement (DM) kilichopata usajili Machi 5 mwaka juzi, Movement For Democratic and Economic Change (MDEC), kilichoomba usajili wa muda Machi 3, mwaka jana; CCJ, kilichopata usajili wa muda Machi 2, mwaka huu na Chama cha Ujamaa na Kujitegemea (CCUK) kiliomba usajili wa muda Januari 20, mwaka huu.
Alisema CCJ iliomba usajili katikati ya bajeti ya mwaka 2009/2010 na kuongeza kuwa hakuna fedha kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo ya usajili kwa sasa.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ipo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Hivi karibuni CCJ kilimpa Tendwa wiki moja, kusahihisha kauli yake kwamba hana fedha za kuhakiki wanachama wake katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kukipa usajili wa kudumu, vinginevyo kitamchukulia hatua, ikiwamo kumfikisha mahakamani.
Msemaji wa CCJ, Fred Mpendazoe, alimtaka Tendwa kuzipitia fomu na nyaraka walizowasilisha katika ofisi yake na kutoa usajili wa kudumu, ili kukiwezesha chama hicho kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwa upande mwingine, Marmo alisema gharama halisi za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani bado hazijajulikana.
Alisema gharama hizo huenda zikajulikana na kutangazwa baada ya kuvunjwa kwa Bunge, Agosti mwaka huu.
Awali serikali iliahidi kuzitangaza gharama hizo Aprili mwaka huu, lakini haikufanya hivyo.
Marmo alisema serikali imechelewa kutangaza gharama hizo kwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hajatoa baraka zake kwa kuzisaini.
Gharama hizo zitatumiwa na vyama pamoja na wagombea wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Tangazo la gharama hizo linatakiwa kutolewa katika gazeti la serikali wiki hii, ili kutoa nafasi kwa wananchi, vyama vya siasa na wadau wa masuala ya siasa kuzijua.
"Kila kitu kipo tayari na kinachosubiriwa ni saini ya Pinda ili ziweze kutangazwa kwenye gazeti la serikali ambalo linatolewa kila Ijumaa," alisema.
Kanuni za gharama za uchaguzi zilijadiliwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya saisa, pamoja na wabunge ambapo walitoa maoni yao.
Gharama hizo ni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea na kampeni kwa nafasi za urais, ubunge na udiwani; kanuni hizo ni sehemu ya sheria ya gharama za uchaguzi iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom