Msajili: Vyama vya Siasa vinavyopinga muswada, vinapotosha na kufanya propaganda

neym8990a

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
244
196
Msajili wa Vyama Vya Siasa amevitaka vyama vilivyoitisha mkutano wa kuupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kuacha propaganda za kupotosha muswada huo kwa sababu hatua zote za mchakato wa maboresho walishirikishwa.

Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kufanyika mkutano wa vyama 15 vya siasa ambavyo pamoja na mambo mengine, vilitangaza kuupinga hadharani Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa vikidai unatengeneza kaburi la vyama vya siasa na demokrasia nchini.

Akijibu hoja za viongozi wa vyama hivyo kwenye mahojiano yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alidai kilichosemwa na viongozi hao ni upotoshaji na kutengeneza propaganda za uongo.

Alisema lengo la serikali katika sheria mpya ni kuhakikisha vyama vya siasa nchini vinapata sheria bora inayokwenda na wakati ambayo itatoa nafuu kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na kwa mujibu wa katiba za vyama vyao.

Alisema hakuna kipengele ambacho kinampa mamlaka msajili kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.

Kwa mujibu wa Msajili, ameshangazwa kusikia marekebisho hayo yanakwenda kuua au kukandamiza vyama vya siasa wakati siyo kweli kwa sababu vyama hivyo vilitoa maoni yao wakati wa mchakato wa maoni mpaka hatua ilipofikia.

“Sasa kama wanaona muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa unakwenda kuua au kuvikandamiza vyama kwa nini walitoa maoni yao?.

Alisema kilichofanyika kwenye muswada huo ni maboresho ya kawaida ambayo vyama na serikali wamekuwa wakifanya kwenye sheria au katiba zao kuhakikisha wanapata sheria bora.
 
Kuna watu hawana uzalendo kabisa kwa taifa. Wadau wamesema maoni yao yamepuuzwa sehemu kubwa, Wewe una ng'ang'ania sheria kandamizi! Kesho Watanzania wakikosa pa kusemea,yakitokea machafuko!? Ulaaniwe Wewe na uzao wako na waliokutuma. Ama unaogopa kauli ya "no free lunch"!? Nawe unajiita msomi unakuja na majibu mepesi kwa hoja nzito!?
 
Kuna watu hawana uzalendo kabisa kwa taifa. Wadau wamesema maoni yao yamepuuzwa sehemu kubwa, Wewe una ng'ang'ania sheria kandamizi! Kesho Watanzania wakikosa pa kukemea,yakitokea machafuko!? Ulaaniwe Wewe na uzao wako na waliokutuma. Ama unaogopa kauli ya "no free lunch"!? Nawe unajiita mdomo unakuja na majibu jepesi kwa hoja nzito!?
wewe unaona hayo n majibu mepesi? swala n kwamba muswada wa marekebisho ni kitu ambacho huwa kinafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kujenga na kurekjebisha sheria kama alivyosema kuhakikisha wanapata sheria bora na vyama vya siasa vimeshirikishwa katka utoaji wa maoni yao kwahyo hizi mambo za kusema ni uonevu n propaganda tu za upotoshaji

na always theres no free lunch my friend.. ww unayependa free lunch itakukost bro..
 
Tusijitoe ufahamu sote ni Watanzania, tunajenga nchi moja. Democrasia mfumo vywama vingi Ni msaada mkubwa mkubwa kwa "Checks and Balance"
Kwa taarifa yenu mnamharibia sana Rais kwa Kuja na mswada wa hovyo namna hiyo. Dunia ipo Dynamic, Sio Static.
 
Huyu nae ni kama Chandarua za kizamani. A.K.A kabudi, sijui kama wanachokipigania wanaelewa wanakolipeleka taifa, kama wasomi.. Na usomi wote huo hadi macho nje nje.
Eti.. " lengo la serikali katika sheria mpya ni kuhakikisha vyama vya siasa nchini vinapata sheria bora inayokwenda na wakati ambayo itatoa nafuu kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na kwa mujibu wa katiba za vyama vyao.
Ni lini serikali ya CCM, iliwahi fikiri hilo? Umwenyekiti wa chama kimoja tu, pasua kichwa, leo muwe na huruma nao, wakati huo wakishrehekea BD zao mahabusu!!

Mnavyo wahangsisha hivyo kana kwamba si binadamu, mnaweza je kuwaamulia u-nafuu wao? Mwisho wa unyanyasaji huu upo karibuni.
You can fool some people sometime, but you can't fool all people all the time, so, some of them will see the light, na watausimamia ukweli, na sio matumbo.
Ni kama sauti ya nyikani huy u hapa chini

Tundu Lissu, naku-miss.
 
A devil can cite a scripture for its own purpose, that to say msajili ana malengo na mswada huu!

Haiwezekani wabunge washiriki kwenye kutunga mswada alafu watoke nje kuupinga?

Lakini nadhani wanasiasa wa Tanzania hasa walioshika nafasi nyeti hawaabudu na wala hawajafundiswa uamunifu kwa kauli na hata matendo?

Tunakosa imani nao sana maana wanesema hivi kesho wanabadili mananeno na hata matendo!
 
wewe unaona hayo n majibu mepesi? swala n kwamba muswada wa marekebisho ni kitu ambacho huwa kinafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kujenga na kurekjebisha sheria kama alivyosema kuhakikisha wanapata sheria bora na vyama vya siasa vimeshirikishwa katka utoaji wa maoni yao kwahyo hizi mambo za kusema ni uonevu n propaganda tu za upotoshaji

na always theres no free lunch my friend.. ww unayependa free lunch itakukost bro..
Wanalalamika maoni yao kupuuzwa wewe. Taaluma inapo kosa msaada kwa taifa, Kabudi anathibitisha hilo.
 
Watu wa aina ya huyu msajili sio tu ndio chanzo cha matatizo lakini ni aibu kuwa na raia wa aina hii kwa nchi inayotaka kujinasua kutoka kwenye shimo la umasikini.
Mtu mzima tena bila aibu anajibu hoja nzito kwa majibu mepesi, Eti kwa nini wametoa maoni yao....huyu sio tu ni mpuuzi bali ni mjivuni, kwani kutoa maoni si lilikuwa ni takwa la kisheria na je hayo maoni yakizingatiwa?
Hivi anakumbuka maoni ya wananchi kwenye rasimu ya katiba mpya? Nyinyi mmepeleka mapendekezo watu wakatoa maoni yao na hamkuyazingatia hata kidogo kwenye huo mswada wenu.
Tatizo sio lake ila huyo aliyemteua ndio ndio chanzo cha haya matatizo, yeye aendelee kutetea ujinga wake kwa kisingizo eti hii ni sheria bora .
 
Viongozi wa kudumu wa vyama hawataki kujenga utamaduni wa kupokezana uongozi ndani ya vyama vyao...bila shaka inabidi kuwe na namna ya kuwashinikiza wasiwe madikteta ndani ya vyama....
 
wewe unaona hayo n majibu mepesi? swala n kwamba muswada wa marekebisho ni kitu ambacho huwa kinafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kujenga na kurekjebisha sheria kama alivyosema kuhakikisha wanapata sheria bora na vyama vya siasa vimeshirikishwa katka utoaji wa maoni yao kwahyo hizi mambo za kusema ni uonevu n propaganda tu za upotoshaji

na always theres no free lunch my friend.. ww unayependa free lunch itakukost bro..
Mkuu hii serikali inapenda kuonea watu wake, kwa historia rejea maoni yaliyotolewa na TUCTA kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Viongozi wa kudumu wa vyama hawataki kujenga utamaduni wa kupokezana uongozi ndani ya vyama vyao...bila shaka inabidi kuwe na namna ya kuwashinikiza wasiwe madikteta ndani ya vyama....
Sema tu mnataka kupandikiza wanaccm ndani ya vyama vya upinzani ili kuua upinzani
 
Kuna watu hawana uzalendo kabisa kwa taifa. Wadau wamesema maoni yao yamepuuzwa sehemu kubwa, Wewe una ng'ang'ania sheria kandamizi! Kesho Watanzania wakikosa pa kusemea,yakitokea machafuko!? Ulaaniwe Wewe na uzao wako na waliokutuma. Ama unaogopa kauli ya "no free lunch"!? Nawe unajiita msomi unakuja na majibu mepesi kwa hoja nzito!?
Wanajisahau sana kuwa kuna maisha baada ya teuzi.
 
Hahaha vyama vya siasa waombe huo muswaada usifike bungeni. Muswaada ni wa ccm, na watakaoupugia kura za ndio ni ccm, spika atakayeupitisha ni wa ccm, rais atakaye usign ni wa ccm. Na utawafaa wa ccm. Maana msajili wa vyama ni wa ccm.
 
Eti
"... lengo la serikali katika
sheria mpya ni kuhakikisha vyama vya
siasa nchini vinapata sheria bora
inayokwenda na wakati ambayo itatoa
nafuu kwa vyama vya siasa kuendesha
shughuli zao kwa uhuru na kwa mujibu wa
katiba za vyama vyao. "

Huo ubora na unafuu anaouzungumzia hapa ni upi?

Acheni udhalimu jamani, hizo ofisi mnapita tu, mtahukumiwa kwa matendo yenu.
 
wewe unaona hayo n majibu mepesi? swala n kwamba muswada wa marekebisho ni kitu ambacho huwa kinafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kujenga na kurekjebisha sheria kama alivyosema kuhakikisha wanapata sheria bora na vyama vya siasa vimeshirikishwa katka utoaji wa maoni yao kwahyo hizi mambo za kusema ni uonevu n propaganda tu za upotoshaji

na always theres no free lunch my friend.. ww unayependa free lunch itakukost bro..
Kwahiyo kusema kwamba mswad huo ni mzuri haya ni majibu mepesi??kwanza hata wadau hawajashirikishwa kwenye huo mswada.marekebisho kadhaa yamekuwa yakifanyika null and void,kwa dalili zinavyoonekana,mswada ushapitisha bila ya bunge kupitisha.,bunge la Tz ni kama mbwa anayebweka hana meno.
 
Wasomi wetu wanaendelea kuliangamiza Taifa kwa maslahi binafsi ya kutetea matumbo yao, historia ni mwalimu bora, watayajutia matendo yao siku moja.
 
Awache kutufanya sisi watanzania ni mapoyoyo au hatujui kusoma au kuandika
msajili wa Vyama Vya Siasa amevitaka vyama vilivyoitisha mkutano wa kuupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kuacha propaganda za kupotosha muswada huo kwa sababu hatua zote za mchakato wa maboresho walishirikishwa. Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kufanyika mkutano wa vyama 15 vya siasa ambavyo pamoja na mambo mengine, vilitangaza kuupinga hadharani Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa vikidai unatengeneza kaburi la vyama vya siasa na demokrasia nchini.
Akijibu hoja za viongozi wa vyama hivyo kwenye mahojiano yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alidai kilichosemwa na viongozi hao ni upotoshaji na kutengeneza propaganda za uongo. Alisema lengo la serikali katika sheria mpya ni kuhakikisha vyama vya siasa nchini vinapata sheria bora inayokwenda na wakati ambayo itatoa nafuu kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na kwa mujibu wa katiba za vyama vyao.
Alisema hakuna kipengele ambacho kinampa mamlaka msajili kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa Msajili, ameshangazwa kusikia marekebisho hayo yanakwenda kuua au kukandamiza vyama vya siasa wakati siyo kweli kwa sababu vyama hivyo vilitoa maoni yao wakati wa mchakato wa maoni mpaka hatua ilipofikia.
“Sasa kama wanaona muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa unakwenda kuua au kuvikandamiza vyama kwa nini walitoa maoni yao?.

Alisema kilichofanyika kwenye muswada huo ni maboresho ya kawaida ambayo vyama na serikali wamekuwa wakifanya kwenye sheria au katiba zao kuhakikisha
wanapata sheria bora.
 
Back
Top Bottom